Msafara wa mh. Nahodha Wapigwa Mawe Tunduma-Mbeya

wikolo

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
800
270
Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la leo, msafara wa waziri wa mambo ya ndani mh. Nahodha umepigwa mawe na vijana wa huko tunduma. Kisa ni kwamba vijana hawakufuruhishwa na kitendo cha kumuona waziri akitumia magari ya serikali akiwa katika shughuli za kuimarisha chama chake huko Mbeya. Vijana wanahoji kwa nini rasimali hizo zisitumike kusaidia wananchi wengine kama vile wagonjwa walioko hospitalini? Hivi ndivyo nchi yetu inavyokwenda kwa sasa.

Source: Mwananchi
 
aisee!nasikia wameikimbia tunduma'wangemuuliza kikwete yaliyomkuta pale wakati wa kampeni
 
safi mby ndo 2nataka mikoa yote iwe ivo.ht leo huko mwanza magamba yatakuwa meng pelekeni lori la kokoto
 
Nawashukuru sana hao walioamua kuupopoa mawe msafara huo baada ya kusikia uchungu wa matumizi mabaya ya rasilimali za taifa,anaenda kwenye mambo ya CCM iweje atumie gari la serikali?na hata hivyo hawa watu wameshakinahi,na for sure days are numbered.
 
Haa! Haaa! Nimekumbuka mch. Mtikira alivyo popolewa mawe kule tarime, hivi ccm na serikali wanapata picha gani hapo. Nadhani arobaini ya ccm imetimia.
 
Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la leo, msafara wa waziri wa mambo ya ndani mh. Nahodha umepigwa mawe na vijana wa huko tunduma. Kisa ni kwamba vijana hawakufuruhishwa na kitendo cha kumuona waziri akitumia magari ya serikali akiwa katika shughuli za kuimarisha chama chake huko Mbeya. Vijana wanahoji kwa nini rasimali hizo zisitumike kusaidia wananchi wengine kama vile wagonjwa walioko hospitalini? Hivi ndivyo nchi yetu inavyokwenda kwa sasa.

Source: Mwananchi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Shamsi Vuai Nahodha Send JComments Waziri Nahodha apigwa
mawe Mbeya Saturday, 04 February 2012
08:08 ALIKUWA KATIKA ZIARA YA
CHAMA MBEYA, ASHANGAA
VIJANA KUMPIGA, AAGIZA
POLISI WAWASHUGHULIKIE Stephano Simbeye, Tunduma.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha,
jana alionja 'joto ya jiwe'
baada ya msafara wake
kupigwa mawe alipokuwa kwenye ziara ya kuimarisha
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
mkoani Mbeya.Tukio hilo la
tatu kwa viongozi wa Serikali
kushambuliwa mkoani Mbeya,
lilitokea eneo la Soko la Tunduma (Kisimani), wilayani
Tunduma. Habari zilieleza kuwa tukio
hillo lilitokea wakati Waziri
huyo na msafara wake
walikuwa wanapita kuelekea
ofisi za CCM Kata ya Tunduma
ambako alitakiwa kufanya mkutano wa hadhara. Ilikuaje? Dalili za machafuko zilianza
wakati msafara huo unapita
kwa baadhi ya vijana
wanaofanya biashara ya
kubadilisha fedha sokoni hapo
kuanza kujipanga barabarani wakizomea na kupiga miluzi. Wengi wa vijana hao
walisikika wakilaumu kitendo
cha Waziri huyo wa Mambo ya
Ndani kutumia magari ya
Serikali katika msafari wake
wa kichama. "Haya ni matumizi mabaya ya
mali za umma," alisikika
akisema mmoja wa vijana
hao. Vijana hao walianza
kumzomea waziri huyo huku
baadhi wakirusha mawe kabla
ya kudhibitiwa na polisi
waliokuwa wanasaidiana na
walinzi wa CCM maarufu kwa jina la Green Guard. Katika sekeseke hilo vijana
wawili walikamatwa na
kukabidhiwa katika Kituo cha
Polisi cha Tunduma. Hata hivyo, Mkuu wa kituo
hicho ambaye hakutaka
kutajwa gazetini kwa kile
alichoeleza kuwa yeye sio
msemaji wa polisi, alikiri
kuwapokea vijana hao na kueleza kuwa wanaendelea
kuwafanyia mahojiano. Mmoja wa vijana hao
aliyejitambulisha kwa jina la
Yusuf Haonga alisema
wamechukua hatua hiyo kwa
vile Waziri huyo
aliwachanganya kwa kutumia magari ya Serikali akiwa
kwenye ziara ya chama. “Hawa wanatuchanganya,
inakuwaje wanatumia
rasilimali za nchi kwa kazi za
chama. Pesa hizo si
zingetumika kuhudumia
wagonjwa waliolala mahosipitalini badala yake
wanazitumia wao,”alisema
Haonga. Haonga alisema kuwa kitendo
cha Waziri akiwa mtumishi
wa umma kufanya ziara ya
kichama kwa magari ya
Serikali, kiliwakera na
waliamua kumtupia mawe ili kutoa onyo kwa viongozi
wengine wa Seriakali. Hata hivyo, habari zingine
zilieleza kuwa vijana
waliomrushia mawe Waziri
huyo ni wafuasi wa Chadema. Gazeti hili lilishuhudia baadhi
ya vijana wakiwa na bendera
za chama hicho cha upinzani
ambao pia walikuwapo
kwenye msafara huo
uliomalizikia kwenye mkutano huo wa hadhara. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk
Willibrod Slaa alipopulizwa
kuhusu tukio hilo alihoji
"Unataka niseme nini? Mimi
niko Dar es Salaam na tukio
hilo limefanyika Mbeya." Aliendelea, "Ndio kwanza
unaniambia (mwandishi).
Inabidi nijue nini kilitokea na
kama kweli ni vijana wa
Chadema nijue walikasirishwa
na nini." Katibu wa Itikadi na Uenezi
wa CCM, Nape Nnauye
alipoulizwa kuhusu suala hilo
alijibu," Sina taarifa." Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
ambaye pia ni mwenyekiti wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama
mkoani humo, Abbas Kandoro
jana alishindwa kuzungumzia
tukio hilo kwa kile alichoeleza kuwa yuko kwenye safari ya
kikazi jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa mkutano huo
uliohutubiwa na Nahodha,
mwenyekiti wa CCM Kata ya
Tunduma, Daniel Mwashiuya
alisema kuna kikundi cha watu ambacho kimeanza
kupoteza amani ya mji wa
Tunduma kutekeleza
matakwa yao ya kisiasa. Alisema “mazingira
tunayokwenda nayo kwa sasa
si mazuri kwa ustawi wa mji
wetu hivyo Wanatunduma
tujiepushe na kuvunja amani
tuliyoizoea ili isije ikapotea,” alisema Kauli ya Waziri Nahodha Akihutubia mamia ya watu
waliohudhuria mkutano huo,
Waziri Nahodha alisema
hajapendezwa tukio hilo na
kuhoji, "Kama limefanyika
kwangu hali ikoje kwa watu wengine?" Alisema kamwe hawezi
kuacha hali hiyo ya uvunjifu
wa amani iendelee na
kuiagiza polisi mkoani Mbeya
kuchukua hatua haraka dhidi
ya kikundi hicho cha watu aliowaita wahuni. Waziri Nahodha pia amepiga
marufuku biashara haramu ya
kubadilisha fedha katika eneo
hilo. Alisema mtu anayetaka
kuendelea kufanya kazi hiyo
itabidi afuate taratibu
zinazotakiwa ili aweze
kuihalalisha biashara yake. “Sokoni pana biashara za aina
mbalimbali zilizo halali na
haramu, lakini nawaagiza
polisi chini ya Kamanda wenu
wa Mkoa, mkae muangalie
namna ya kurejesha amani mahali hapo. Sasa likizo basi,”
alisema Nahodha. Waziri Nahodha alisikitishwa
na taarifa za kuendelea
kuvunjika kwa amani katika
mji wa Tunduma ambapo
aliwataka wananchi wa mji
huu kuthamini amani iliyojengeka kwa muda mrefu. Aliwataka wasidhani kwamba
amani iliyopo imeshuka
kutoka Mbunguni na kwa
sababu hiyo wao wenyewe
wailinde na kuidumisha kwa
kushirikiana na polisi kwa njia ya ulinzi shirikishi. Historia ya matukio Hili ni tukio la tatu kwa
viongozi wa kitaifa
kuzomewa katika mji wa
Tunduma ambapo mwaka
2010, mke wa Rais, Mama
Salma Kikwete, alizomewa katika eneo hilo alipokuwa
akipita kutokea mkoani
Rukwa katika ziara za
kampeni za uchaguzi. Mwaka 2009, Mwenge wa
Uhuru ulilazimika kubadili njia
ghafla kufuatia dalilili za
uvunjifu wa amani. Tukio jingine ilikuwa ni
Oktoba, 2008, ambapo
msafara wa Rais Jakaya
Kikwete kushambuliwa kwa
mawe kwenye kijiji cha
Kanga, wilayani Chunya. Tukio hilo lilitokea katika Kijiji
hicho wakati msafara wa Rais
ukiwa njiani kuelekea Mbeya
mjini ukitokea mji wa
Mwakwajuni wilayani Chunya
ambako alikuwa amefanya ziara.
Kwa mujibu wa habari hizo
magari sita yaliyokuwa
kwenye msafara huo
yalishambuliwa kwa mawe na
baadaye vijana kadhaa walikamatwa. Ilidaiwa kuwa waliofanya
tukio walikuwa wamejipanga
pembeni mwa barabara na
baada ya magari manne ya
mwanzo kupita, likiwamo la
Rais Kikwete, ndipo mawe yalianza kuvurumishwa. Hata hivyo, ilidaiwa kuwa
wananchi hao walikasirishwa
na kitendo cha kushindwa
kumwona Rais Kikwete baada
ya kumsubiri kwa muda mrefu
ili awahutubia na kusikiliza kero zao.
 
Kama wananchi wanaweza kuhoji rasilimali za serikali kutumiwa na CCM basi ukombozi umekaribia.
 
Ni wana-ccm wachache sana wanaokubalika Mbeya kwa sasa, hasa baada ya saga ya Mwakyembe na afya yake. Sijui kama Mh Nahodha anafahamu hili. Pia kitendo cha waziri kusema watu washughulikiwe ni uchokozi. Waziri anakumbuka fujo za mwaka jana? sio polisi, JKT au JWTZ waliweza kuwatuliza. Kama hakutokeza Sugu leo hii tungekuwa tunaongelea mambo mengine.
 
Ni wana-ccm wachache sana wanaokubalika Mbeya kwa sasa, hasa baada ya saga ya Mwakyembe na afya yake. Sijui kama Mh Nahodha anafahamu hili. Pia kitendo cha waziri kusema watu washughulikiwe ni uchokozi. Waziri anakumbuka fujo za mwaka jana? sio polisi, JKT au JWTZ waliweza kuwatuliza. Kama hakutokeza Sugu leo hii tungekuwa tunaongelea mambo mengine.


if mwakyembe sympathy exceeds they may also stone him
 
safi mby ndo 2nataka mikoa yote iwe ivo.ht leo huko mwanza magamba yatakuwa meng pelekeni lori la kokoto

Taratibu jamani, kokoto hazitasaidia zaidi ya kujeruhi na wananchi wasio na kosa. People's power haitakiwi kuwa expressed kwa kokoto.
 
Hahaa yaani alikwenda mbeya bila mwandosya na mwakyembe? Ilikuwa lazima yamkute tu.
 
anatafuta nini Mbeya wenzake wako Dodoma na Mwanza

Watu wanasema Dar vijana wengi si wakazi wa huko chocho za kukimbilia hawazifahamu wengi wao walienda na mbio za mwenge au malori
 
Back
Top Bottom