Msafara wa Dkt. Slaa wazuiwa kwa muda Iringa jioni hii

Status
Not open for further replies.
CCM hawajazoea kuona chama kinafanya kazi wakati wote kujiandaa kuchukua nchi. Kwao ni lazima kazi zisimame, kisha wakurupuke na kutumia nguvu kuzima harakati halali za watu waliochoshwa na ufisadi na hila za ccm....
 
kweli CDM wako juu Mungu awaangazie mzidi kuelimisha wananchi ili kujua nini cha kufanya 2015 ili kuondoa ukoloni wa ccm
 
Hivi mbona zinatumika nguvu na rasilimali nyingi sana kulinda/kuzuia vitu ambavyo havina hata chembe ya uhatarishi kama ingekuwa usalama wa raia na mali zao unazingatiwa hivi kama tunavyoona polisi wanavyotumia rasilimali kiasi hicho kweli ningelipongeza sana jeshi letu kwa kazi nzuri.

Kwenye majukumu yao ya msingi hawafanyi kama inavyowapasa kufanya,kweli tuna safari ndefu sana ya kufikia nchi ya ahadi.

Uhalifu kila kona,wahamiaji wasiokidhi vigezo vya kuwa wahamiaji,usalama wa raia mtaani ni wamashaka lakini hatuoni wakitumia nguvu ile ile wanayotumia kudhibiti vyama vya siasa hasa vya upinzani kutekeleza majukumu yao kama inavyowapasa kuyatekeleza.
 
Nilishuhudia jana hali hii hapa Manispaa ya Iringa; msafara wa CHADEMA ulikuwa shwari na tulivu. Watu wao wote walikuwa katika magari na hakukuwa na umati ulikuwa ukifuata nyuma kwa miguu.

Aidha kwa mbele walikuwa na gari lao la matangazo ambalo halikuwa likirusha/ likitangaza chochote zaidi ya kupiga muziki (wimbo maarufu wa "peoples' power"). Kifupi haukuwa na tofauti na msafara wowote wa harusi.

Lakini kilichotia hofu ni idadi ya polisi wa kutuliza ghasia katika gari zao pamoja na gari ya kamanda wa polisi mkoa iliyokuwa ikifuatilia kwa nyuma.

Polisi hawa walivalia mavazi yao ya kutisha. Aidha polisi hawa waliwekwa ktk maeneo zaidi ya kule msafara wa Dr. Slaa ulikoishia. FFU walijipanga katikakati ya barabara ya eneo la Kihesa katikati ya kituo cha FFU na Majembe.

Na hili lilinifanya nijiulize, "nini hasa lengo la jeshi letu? Je, ni kweli polisi wetu, hasa kamanda wa mkoa wa Iringa hawana uelewa (hata wa kawaida tu, si lazima wasome saikolojia ya binadamu) kuwa hali hii ni kutisha wananchi? Je, si kujenga hofu? Hapa ndipo mwenye busara yoyote atajiuliza hiki kinachoimbwa "tz ni nchi ya amani na utulivu kiko wapi"

Je, huu ni uonezi au hujuma kwa vya vingine vya siasa? Mbona ni kawaida kwa ccm kupokea viongozi wao kwa maandamano?
Ninajiuliza, " nini hasa hofu ya serikali hii?


Ejl
kwa ninin
 
M4C a nonstater, a failure.

Wewe kwa akili yako nguvu zote hizo za MAGAMBA na vyombo vyake vya matisho CDM ni failure? Kwenye mitihani yako uliyopitia shuleni ya kudadavua picha ulikuwa unapata marks ngapi vile?
 
Hii ni message sent and delivered kwa wale wanaoota ndoto kuwa Zitto kuvuliwa madaraka ndo Chadema imekufa, acheni uwoga wasaliti wote wapigwe chini na Chadema itazidi kusonga mbele. Zitto jiandae kurudisha hela ya CCM vinginevyo itakutokea puani maana azimio lako limekwama, watanzania hawadanganyikiiiiii
 
183503302.jpg

May be this is a failure to you. Na CCM Iringa mtakiona cha mtemakuni.

Tunangojea press conference. Hii inatupa tabu kidogo.
Hivi hawa wenye tishet nyekundu wanawatoaga wapi? Wana mafunzo au wanawavalisha tu miwani ya kininja na Viatu vya mtumba na suruali nyeusi ili waonekane na wao ni kama walinzi? Au ndio wanaoitwa Red Brigade?
 
Bila ya hao mapoliccm -- CCM haina kitu kabisa!!!! CCM kwishney. Pamoja na ishu ya zitto wanayoikuza, CCM wameiona nguvu ya dola!!

kama mna ubavu CCM acheni kutumia mapoliccm tuone. Kila saa mbeleko tu!!!
 
hivi ZeMarcopolo et al CDM Si inakufa, na Dr. Slaa hana tena mvuto kwa raia mbona nguvu nyingi hvi kupotezwa tena anakopita? Kwanini tusfanye mengne?
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom