Msafara wa CCM wapata ajali Chunya.

Brightman Jr

JF-Expert Member
Mar 22, 2009
1,225
232
Habari za kuaminika nilizopata sasa hivi kutoka katika kijiji cha Matundasi wilayani Chunya Mbeya ni kwamba mwanachama mmoja wa CCM amefariki dunia kwa ajali ya gari aina lori na wengine wengi wakiwa wamejeruhiwa vibaya. Chanzo cha ajali waliokuwemo humo wanasema ni kitendo cha dreva kuongea na simu na huku akiwa ameachia usukani wa gari hilo ambalo lilikuwa katika mwendo mkali na kulikuwa na kona eneo hilo. Misafara hiyo ya wanachama ni kwa ajili ya kukutana mjini Chunya kufanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali ambao majina yao yamepitishwa na NEC-CCM hivi majuzi.
 
tuwaombee wapiganaji,aliefariki Mungu amlaze pema peponi na majeruhi wapate kupona mapema kuendeleza harakati za kuendelea kushikilia dola
 
Makafara kuelelekea 2015 yameanza kutolewa rasmi! Ee Mola tunusuru.
 
tuwaombee wapiganaji,aliefariki Mungu amlaze pema peponi na majeruhi wapate kupona mapema kuendeleza harakati za kuendelea kushikilia dola

Hapo kwenye
red; wenzako wakikusikia kazi unayo. Kama ilivyo UFISADI, hilo neno halipo kabisa kwenye msamiati wa chama chenu. Hiyo ni "habari mpya".
 
Makafara kuelelekea 2015 yameanza kutolewa rasmi! Ee Mola tunusuru.

Kama nakumbuka vizuri ,haya mambo ya kubeba watu kwenye malori Yaliisha pigwa marufuku kuwa yanahatarisha maisha ya watu.sasa inakuwaje CCM wanabeba watu kwenye malori na Trafiki wanawachekea?Hizi sheria ziko kwa ajili ya akina nani?
 
Ukiwa muongo, usiwe msahaulifu..........ajali itokee Chunya Mbeya , police wa-confirm Tanga we lazima utakuwa Mwanga tu

Nasisitiza mie si mwongo! Hivi uongo kwa tukio kama hili inasaidia nini? Police ninaosema ni wa kutoka Mbeya ilikotokea ajali na wala si vinginevyo. Kumbuka habari hii nimeipata kwa wahanga wenyewe walio katika msafara huo.
 
Yaani Magamba hawajaacha Kusafirisha watu Kwa Malori!! Policeccm Mnafanya nini!! Kila siku watu wanakufa kutokana na kupakiwa kwenye Malori!!!
 
Wakafie mbali magamba hao!!! Tunavyochapika na maisha, wao bado wanaendekeza uccm!
 
Lorry? Ok, Mungu awaponye majeruhi na tumwombee alofariki ili Mungu ampumzishe kwa amani mbinguni. Kama ni kweli!!!!!!
 
poleni sana wafiwa na majeruhi

Mkuu Jackbauer, tuwambie wanamagamba waache kuendekeza njaa na tamaa ya kuvaa njano na kijani, malori yatawamaliza!! Mungu hapendi dhuruma tunayofanyiwa na Chama Chenye Magamba tz.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom