Msaada

kuna mdada anajirengesha kwangu ila mimi sina mpango nae
sasa jana usiku katuma sms ktk simu yangu akilalamika kwamba namtesa
ksababu najua ananipenda ndio maana namletea mapozi sasa kibaya zaidi wife ndio mtu wa kwanza kuiona sms ameniwashia moto akinituhumu kwamba nammega yule demu nimejaribu kumuelewesha hanielewi kabisa na ameshaenda kushitaki kwa wazee wangu kwamba mimi sio muaminifu ktk ndoa so jpili natakiwa ktk kikao na wazee.je waunwana mnanishaurije?


Katika kufanya counseling kuna wadada wanaumizwa sana mioyo yao na wanaume/vijana ambao wana-approach wakiwa ndani ya ndoa - wanaficha hawajaoa na kumweka mdada/mwanamke katika hali ya kujiona amepata mpenzi - wanafanya hivyo kwa nia mbali-mbali - wengine just for funny; wengine wakitaka kufanya mapenzi nje ya ndoa kwa tamaa zao; wengine kufurahia udanganyifu wa shetani ndani yao; wengine kukopa hela kwa hao wapenzi wakizua shida kubwa kubwa - kumbe ni utapeli etc.
ULIYEHITAJI MSAADA - uwe mwangalifu sana usiwe ukawa kwenye hili kundi mojawapo. HAIWEZEKANI MDADA AANZE KUKUAMBIA UNAMTESA MOYO WAKE KWA MAPENZI - JAMANI WANAWAKE NI VICHAA AU WANA AKILI TIMAMU?? HUYU DADA AMEKUPA MOYO WAKE NDIO MAANA ANAONA ANATESEKA - au anataka nini kwako??
Tuwe waangalifu sana kwani kile tupandacho kwenye maisha ndicho tutakachovuna. Dada apate namba aanze kutuma message za mateso?? Na kama WIFE wako ameenda hadi kwa wazazi - sio jambo la mara moja - UMEZOEA? USHAURI WA BURE NI KUMWAMINI YESU ABADILISHE MAISHA YAKO NA NDOA YAKO ITAKUWA YA FURAHA - OMBA MSAMAHA KWA HUYO DADA ULIYEMUUMIZA MOYO WAKE NA UMWAMBIE UNA MKE.
Mengi siku nyingine.
 
mwenye njaa hawezi kwenda kwenye restaurant iliyofungwa, inaweza ikatokea kibao cha "closed" kikawa hakionekani, lakini kama kweli pamefungwa akisogea karibu ata jua na kujiondokea zake taratibu...

ukiona umemwambia mtu wewe hauko available halafu anaendelea kujileta ina maana message yako kwake ina walakini...pengine hapo ndipo ulipokosea

kuna wengi tu eti wanabandika message ya 'closed' mlangoni halafu mlango nusu upo wazi, waiter kasimama mlangoni anakaribisha wateja kwa smile, harufu ya pilau hadi mtaa wa pili...

kama alijilengesha na wewe ukakataa kwa maana ya kukataa angekuwa amejianzia zake mbele mapemaaaa

kikao cha kesho si ishu kubwa, ishu ni kuangalia wapi umekosea kama binadamu, kujisahihisha na kufikiria jinsi ya kusafisha doa kwenye ndoa
 
Mimi ni muaminifu 100% ndio maana hata wife cm yangu yuko huru nayo siifichi wala nini nashangaa huyo binti amepataje namba kiukweli waungwana
sijawahi kummega huyo binti
Mkuu, nakupa ushauri wa bure...do anything you want but respect your wife...utakujakugundua baadae ukijampoteza kuwa alikuwa ni muhimu katika maisha yako na kuoana kwenu Mungu alipenda zaidi kuliko mtu yeyote...ukenda kwa wazee nakushauri kuwa mpole na tumia kichwa chako vizuri kufikiri...an aorta of anger will cost your respect kwa mkeo na wakwezo.
 
Mademu wanaotongoza mbona wapo wengi tu, tena wengine wake za watu na wana ujasiri wa ajabu. Na pia kuna mademu wanaoamini kuwa wakimnuia mwanaume lazima wampate, na tena hawakubali kukataliwa, wanahisi itawadhalilisha maana wao ndio waliozoea kukatalia watu na sio kukataliwa. Nina uzoefu na hili la mademu watongozaji, wapo sana na wana uwezo wa kuwa aggressive kinoma.

Kama uliweka msimamo huo wa kumkatalia huyo demu, kuwa imara na endelea nao. Lakini je, ulishamjulisha kuhusu matatizo aliyokusababishia? Mweleze hiyo pia aelewe kuwa kumkatalia kwako kulikuwa na sababu ya maana, na matokeo yameshaanza kuonekana.

Kwenye hicho kikao, sema ukweli wako, kubali ushauri wa wazee, na kata mawasiliano na huyo kicheche. Mwulize mkeo pia akupe mbinu anazotumia kukatalia wanaume maana wenzetu hao wana uwezo na uzoefu wa kukatalia kuliko sisi. Mwombe mkeo ushirikiano wake katika hili maana ni vita yenu mnayopaswa kushinda ili ndoa yenu iendelee kusimama imara.
 
Humu kuna watu wa zamani nini?Hivi namba ya mtu ni siri kweli?Ndio kosa alilofanya huyu bwana anayeomba ushauri?
Mtu hata bila kukupania si kiasi cha kumuomba mtu mliye karibu akakupa,hv kweli kuna mtu ambaye ana uhakika namba yake ni ya siri haiwezi kupatikana kwa kicheche aliyepania?Ni bora kama hamna cha kumshauri mkanyamaza.
Hv ukikataa kwenda kwenye hicho kikao inakuwa nini?Na kama ukienda(of course ni kwenu)Ukasema huna tuhuma na hutaki kujibu itakuwaje,hapo ni sms unatetemeka hivyo,je mamaa angemkuta yuko ndani angekakuta kako half naked kanakunywa maji kakimbilia bedroom?Si angepasuka?Mama zetu hao cool down big boy!
 
Back
Top Bottom