msaada

benisrael

Member
Dec 28, 2011
12
5
jamani naomba msaada wa ushauri nina rafiki wa kalamu kutoka ivory cost,ila kwa sasa yuko kwenye kambi ya wakimbizi senegal baada ya kutokea machafuko na wazazi wake wote kuuwawa,
sasa ameniomba nimsaidie kuhamishe fedha za marehemu baba yake kwenda kwenye benki yoyote hapa tz.kwani anadai hana ndugu yeyote anayeweza kuwasiliana naye kwa sasa.
 
Dogo asimuamini huyo mimi natumiwa kila siku barua kama hizo kwenyeeemail yangu, we wachana naye huyo mwizi tu.

Ngojea kama hajaomba umtumie pesa za Remittance Charges.
 
utaibiwa shauri yako awo ni matapeli wa mitandao kaka mi natumiwa nyingi tu
 
Nigerians at work
Na unaingia mkenge kwa miguu miwili

Wake up!
 
Mneanza lini urafiki na mmeonana hana kwa hana? Urafiki wa Karamu??:A S 465::eyebrows:
Ebu jaribu urudi na kisa kingine hapa. Hao ndo wa Afrika wa Kimagharibi MKuu!!
 
Msaidie kimawazo. yaani maongezi yenu yasihusiane na mambo ya bank wa account namba. iwe yake au yako. hata hapa jf alikujaga demu anajiita YAKES hadi alikuwa anapm watu kumbe tapeli. bahati nzuri sijui alikosea akampm invisible wakamshitukia. Muulize nyani ngabu atakuambia. pole sana. Mia
 
Hayo ni balaa, Mi nilikoswa koswa vibaya mnoooo! Ogopa tapeli haooooo!!!!! Hmna cha Mkimbizi wala nini!!!!
 
utaibiwa wewe hao ni watu toka afrika magharibi,kua makini.
hawa hapa kwenye picha.
kls-wmk.php.jpg
 
changa la mcho hilo,mkatae huyo rafiki,mwambie akutumie US$ 1000 kwa njia ya Western Union ili umfungulie Acc hapo Tz,vinginevyo hilo litakuwa Tp tu.Nalog off
 
jamani naomba msaada wa ushauri nina rafiki wa kalamu kutoka ivory cost,ila kwa sasa yuko kwenye kambi ya wakimbizi senegal baada ya kutokea machafuko na wazazi wake wote kuuwawa,
sasa ameniomba nimsaidie kuhamishe fedha za marehemu baba yake kwenda kwenye benki yoyote hapa tz.kwani anadai hana ndugu yeyote anayeweza kuwasiliana naye kwa sasa.

Huo urafiki mmeanza lini? Na iweje akubali fasta fasta akutumie mamilioni?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom