Msaada...

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,808
59,336
Hamjambo wataalam!?

Nimechoka kunununua charger mpya kila siku kwahiyo naombeni msaada/mwongozo wa kutatua tatizo langu.Nna kimeo changu(laptop) cha HP 550 kwa miaka miwili sasa,...kinanitesa kweli.Nineshanunua charge mpya mara tatu nikitumia baada ya wiki mbili tatu inaungua na kuyeyukia mbali...literally!

Yani kale kapini kanapata moto mpaka kanaungua/yeyuka!!

Embu nisaidieni jinsi ya kutatua hili tatizo mwenyewe kimya kimya.Ushauri wa kupeleka kwa fundi au kununua mpya mezeeni tu maana ni pesa sina!!
Asanteni......!
 
Kuno short circuit kwenye connection, kupeleka kwa fundi ndo only solution unless unaweza kufungua mwenyewe na kutafuta shoti iko wapi.
 
Power Adaptor ambayo unatumia inabana unapochomeka? kama inakuwa loose lazima isababishe leakage ya current ambayo husababisha heat.... na hatimaye kuungua, kama inabana, na ni recommended kwa hiyo laptop basi peleka laptop kwa fundi....
 
Nahisi huwa wanakubambikia Charger!,
Mimi yangu ni HP 6720 Charger inagonga kazi kama kawa, Jarib uend pale qprint kama upo dar kacheki alaf ongea na vijana.
 
Inabana mpaka wakati mwingine hua nafikiria kwamba inawezekana nailazimisha!!
 
Nahisi huwa wanakubambikia Charger!,
Mimi yangu ni HP 6720 Charger inagonga kazi kama kawa, Jarib uend pale qprint kama upo dar kacheki alaf ongea na vijana.

Hapo pa kubambikiwa hapana....
Ngoja ninunue nyingine kwa mara ya mwisho...
 
Kama wall socket inayosababisha adaptor kuungua ni moja basi hakikisha pia conection za wall socket yako ziko sawa.

Kama adapator inaungua popote pale unachomeka basi inawezekana unanunua/unauziwa adpator isiyo kuwa na mfumo/ kiwango/vipim sahihi wa umeme

Lakini adapator kuyeyuka ni vizuri . Ni preventive measure .In the same case kwenye desktop computer matokeo ni power supply kuungua. Sababu compute haina adaptor.

While ni Tatizo adaptor kuugua lakini pia ni kama security mwasure ya kulinda laptop yako.
 
make sure unapochomeka ina bana kenye machine isiwe loose pia mistake ambayo weng tunafanayani kutumia extension .extension nyingi ni mnovu zinatumia wire laini kwa ndani .ina haribu vitu sana tumia socket ya ukutani ambayo ni nzima.
 
Mtazamaji asante kwa mchango...yani sio tu kwamba nimetumia socket tofauti bali sehemu(nyumba) tofauti na hali ni ile ile.Yani lp hua inapata moto utadhani italipuka wakati wowote.Kuhusu kuuziwa adapter isiyo sahihi mwenyewe hua nahakikisha ni 18.5V na sio zaidi wala pungufu.Wauzaji nao sio mchina kwahiyo nawaamini.
 
make sure unapochomeka ina bana kenye machine isiwe loose pia mistake ambayo weng tunafanayani kutumia extension .extension nyingi ni mnovu zinatumia wire laini kwa ndani .ina haribu vitu sana tumia socket ya ukutani ambayo ni nzima.

Ntakua muangalifu na hilo siku za usoni...ila kwa sasa hivi situmii extension!!
Thanks!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom