Msema yote
JF-Expert Member
- Mar 19, 2013
- 448
- 298
Poleni na shughuli za kutwa wana jamii bila shaka mu wazima wa afya, kwa upande wangu ni mzima kiafya ila kimawazo ni tatizo.
Naombeni nianze hivi, nina mchumba wangu alie mjamzto sasa kila atachokula yeye ni kutapika tu, kiukweli nashindwa kuelewa nifanyeje na hii hali inanichanganya sana, nimezungumza nae ili kujua kwa nini inatokea hivo anadai mwenyewe haelewi, hvo nikaamua nimtafute jamaa yangu mmoja hiv anipe ushaur nilivo mweleza akanambia hiyo ni hali ya kawaida kwa wajawazito nikasema ok (kwa sababu sina utaalam na mambo ya mimba), sasa jana mchumba wangu kanambia alienda hospitali kiukweli alionambia yameniogopesha na kunishtua, anadai wamemwambia kwa mwili alio nao ni lazima ajifungue kwa oparesheni, pia wamemwambia akiwa na mawazo sana anaweza pata kifafa cha mimba kitu ambacho kinaweza sababisha either mama au mtoto kufariki, vilevile anadai wamemshauri aitoe kwani kwa umbo lake ( mfupi japo si sana) si sahihi kwa sasa kubeba mimba.
Kiukweli napata maswali mengi kichwani bila majibu, maswali kama haya(chini) yananipa shida sana
**Sasa najiuliza ni umbo lipi lilo sahihi kubeba mimba
**Ni kwanini anatapika(mara kwa mara) kila anapokula chochote
**Je ni sahihi atoe hiyo mimba eti mpaka umbo litaporuhusu japo anamiaka 22(umri ambao sina hakika kama atakuwa tena)
**Je ni kweli atajifungua kwa oparesheni kama walivo mwambia.
NAOMBENI MNISAIDIE MAJIBU YA MASWALI YANGU HAPO JUU WAKUU, KIUKWELI SINA AMANI KABISA KWA HILI, TAFADHALI MZAA SI MAHALA PAKE, ASANTENI.