msaada waku,eti aleji test ndio nini?

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
8,307
13,269
kuna mdogo wangu anatokwa na vipele,akimeza dawa za aleji,vinaisha,kisha vinarudi tena!nimempeleka hospital moja wamedai nikamfanyie aleji test kwenye hospital kubwa,mi nipo dar.je hii inaweza kuwa na gharama kiasi gani?
 
Allergy test ni vipimo vya kuangalia ni vitu/vyakula gani ana allergy navyo ili kugundua hicho kinachomsababishia vipele.

Bei sifahamu. . .
 
Ni vipimo vinavyofanywa ili kujua anadhulika na kitu gani, iwe ni chakula au chemicals. Madaktari wa ngozi wanaweza kukusaidia vizuri zaidi. mara ya mwisho kulikuwa na Daktari ana-visit pale Dar group au unaweza kutembelea muhimbili.
 
nendamagomeni karibu na bp petro station kushoto kuna hosp inaitwa ekenywa ni ya dr ole wa muhimbili wana pima hapo
 
Nenda AAAR Hospital kipimo sh.15,000 kama haijabadilika muda wa kusubiri majibu ni dk 20. Pole.
 
Nenda AAAR Hospital kipimo sh.15,000 kama haijabadilika muda wa kusubiri majibu ni dk 20. Pole.

Inachukua kama lisaa kufanya vipimo kwa njia ya ngozi, kwa kupima damu itakua siku kadhaa kutegemea na wanaofanya kazi maabara.
 
Hapo dar zipo dispensari nyingi za kupima iyo kitu, mi nilipimiwa kule RTD, unachomwa visindano vingi vya dawa kwenye mkono, vikoreact kwa kuvimba, wanasoma kwe guide, afu wanakuambia una allergy gani.
 
Inachukua kama lisaa kufanya vipimo kwa njia ya ngozi, kwa kupima damu itakua siku kadhaa kutegemea na wanaofanya kazi maabara.

Asante Lizzy, mi nilifanyiwa ya ngozi nilisubiri kwa muda wa dk 20 tu nikapewa majibu au walinichakachua?
 
Asante Lizzy, mi nilifanyiwa ya ngozi nilisubiri kwa muda wa dk 20 tu nikapewa majibu au walinichakachua?

Hahaha. . . pengine hawakuchukua vipimo vingi. Ila kama ulipata majibu yako na yapo sahihi basi hamna uchakachuzi.
 
Hata ya damu si lazima yachukuwe siku kadhaa.

Ushauri wangu ni kuwa unaweza ukaambiwa una allergy ya vitu kaa 50 hivi, sasa usijilazimishe kuacha na na vyote. Angalia vyenye athari kubwa sana tu
 
Hata ya damu si lazima yachukuwe siku kadhaa.

Ushauri wangu ni kuwa unaweza ukaambiwa una allergy ya vitu kaa 50 hivi, sasa usijilazimishe kuacha na na vyote. Angalia vyenye adthari kubwa sana tu
hilo nalo neno mkuu,kwani wanaweza mwambia alergy yake ipo pale anapofanya mapenzi!c utakuwa mtihani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom