Msaada wako utanisaidi kujikomboa na umasikini..

pepekale

Member
Nov 25, 2010
60
50
Heshima zenu wakuu , Kutokana na ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira especially kwetu tulio hitimu vyuo hivi karibuni , Nimeamua niingie kwenye ujasiliamali ili angalau niweze kusukuma gurudumu hili la maisha .Nimepata sehemu mkopo wa milion 25 za kitanzania na nimeona niwekeze kwenye sector ya usafirishaji, hivyo nimeamua kufanya biashara ya daladala katika ​mkoa wa dar-es-salaam. Naomba msaada kwa mtu anayejua wauzaji wa magari(coaster) ambao naweza pata gari kwa kulipa 70% cash na 30% iliyobaki niwe nawapelekea kidogodogo kwa makubaliano maalum.
N.B kwa sasa nipo nje ya nchi nategemea kurudi siku za usoni hivyo msaada wako utanisaidia sana.
Aksanteni ndugu zangu
 
Nashukuru kwa mawazo yako, lakini hujanipa sababu za kuacha na hii biashara na kufanya biashara nyingine.
 
hii biashara kwa sasa itafanywa kwa mfumo wa private public partnership (PPP) na SUMATRA wameshapata makampuni makubwa watakayo contract nayo routes zote za daladala DSM
 
Hilo dala dala utaendesha mwenyewe??? Kama sivyo,jitayarishe kutengeneza kwa kununua spares frequently-they are rekless drivers,hawajali Pesa hyo itatosha???
 
usafirishaji kwa kutumia daladala kwa DSM ni mgum,tunapokwenda daladala hatakuwa na faida kwani unaanzishwa usafiri wa UMMA,Madereva ni tatizo kwa sehemu uaminifu ni mdogo uongo mwingi,ujuzi na uzoefu ni mdogo pia,PM nitakupa ushauri usio wa daladala
 
usafirishaji kwa kutumia daladala kwa DSM ni mgum,tunapokwenda daladala hatakuwa na faida kwani unaanzishwa usafiri wa UMMA,Madereva ni tatizo kwa sehemu uaminifu ni mdogo uongo mwingi,ujuzi na uzoefu ni mdogo pia,PM nitakupa ushauri usio wa daladala

Kwanini usitoe ushauri wako hapa kwa faida ya wote jamani
 
mkuu biashara ya daladala labda uendeshe mwenyewe maana kama utampa mtu akuendeshee na kusimamia akuletee pesa jioni watauza matairi yako mapya watafunga chakavu, watakuibia vitu kwenye engine na kukufungia chakavu na kisha utaambiwa ukatengeneze na ukienda unauziwa vile walivyoiba. pia utakutana na mambo ya leo tangia asubuhi sijafanya kazi kabisa gari ilikuwa inasumbua starter/tulikamatwa na trafiki namambo mengine kibao lakini utakuta jamaa kapiga kazi usiku mzima tena labda hakuzima ijini mpaka siku ilofatia na kapiga hela ndefu na wewe hujapata kitu ila gharama za matengenezo/kodi/ mshahara zako. kaka jikite kwenye uzalishaji na ukisimamia mwenyewe utaajiri wengi zaidi na faida nyingi zaidi. usiogope hata mbuyu ulianza kama mchicha. rejea nchini jipange ingia kwenye sekta za uzalishaji (production) au za huduma lakini sio magari.
 
Labda uipeleke iwe daladala mikaoni ianweza ikalipa. lakini pia simamia wewe mwenyewe. Ikibidi uwe konda kabisa. Pia tafuta dereva mzoefu sana sio wababaishaji ambao mtapata ajali ndani ya wiki moja.
 
Back
Top Bottom