Msaada wako:Biashara mikoani na Dar

Charles1990

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
249
46
Habari za saa hizi wakuu.Naamini Mungu anasaidia na ataendelea kufanya hivyo.
Jamani nimepata mkopo(1M).Nimesikia mwezi huu kuna mikoa inafanya uvunaji.Nilikuwa na wazo la kuchukua mazao mikoani na kuleta Dar kwa kuuza.
Tatizo ni kwamba sijui namna ya kupata hayo mazao huku mikoani achilia mbali soko.Naombeni msaada kwa mwenye ujuzi zaidi na hii biashara.Namna ya kukutana na wakulima na wanunuzi wa jumla kwa Dar.
Ni mazao gani yataenda haraka na yanayolipa kwa Dar,na mikoa nayoweza kupata hayo mazao.Thanks.
 
kalime mpunga,ukivuna lete dar uuze,vinginevyo donate half of your one mill. to JF forums,mungu atakuzidishia mara mia:dance: the other half unarudisha mkopo ,then unafanya marejesho kidogo kidogo to cover the other half,na kwa kuwa umechangia JF utakuwa unasoma kwa makini zaidi posting za humu,then utapata uwezo mzuri wa kurudisha na kupata hiyo ziada niliyotaja awali ya mara mia.

else hiyo milion irudishe mapema ,jipange then rudi ukakope tena,kimsingi watu wanatakiwa kukopa ili kupanua biashara na siyo kukopa kuanzisha biashara.
 
Thanks bwana mzalendo.Hio product ya mpunga kuipata naona haitakuwa tabu hata kidogo.Hata hapa mkoani nilipo tunalima hii kitu sana.Sasa nikileta hapo Dar nitapata wapi mtu wa kumuuzia mara moja nigeuke?Nitashukuru sana ukinipata hiyo info mkuu.
Kuhusu ku donate jf i promise you nitatoa as soon nitakavyomaliza kulipa deni langu.Naamini halitachukua muda kurudisha nikianza kupambana.
 
Mkuu hongera kwa kuwaza kuanzisha business!wewe fanya kitu kimoja,weka milion yako pembeni,fanya kitu inaitwa market survey kwanza!sikushauri ukauza tandale kwani madalali wanasumbua sana!chukua hapo kama 50,000 nenda mbeya kafanye survey,je mpunga unapatikana?na kama ukinunua ukiuleta huku dar je italipa?Kyela kuna mchele mzuri sana na mbeya pia pale igurusi,au mbozi pia kuna mchele mzuri!unaweza hata usilete huku dar unapiga kambi huko huko!unanunua mpunga unakobolesha then unauza mchele!inalipa lakini sio saaan!ila uhakika wa kupata hela yako upo kwani unauza cash!hakuna dalali hapo!

Kila la heri mkuu.
 
Thanks mkuu avocado.Mkuu mimi nipo Klm,na huku kuna sehemu wanalima mpunga.Naweza kwenda hapo nikafanya hiyo survey,tabu kidogo nitapata katika kuuza.Ingekuwa afadhali kama ningepata mtu wa kununua kwa jumla nikiuleta hapo Dar.Pili sina hakika kama huu mchele wa klm (Mabogini) unapendwa na walaji.Usije ukaniharibikia mikononi.
Hii habari ya kukoboa ni nzuri pia,lakini mkuu hiyo mashine ya kukobolea inakamatika??au ni ya kukodi?
Thanks mkuu.
 
Thanks mkuu avocado.Mkuu mimi nipo Klm,na huku kuna sehemu wanalima mpunga.Naweza kwenda hapo nikafanya hiyo survey,tabu kidogo nitapata katika kuuza.Ingekuwa afadhali kama ningepata mtu wa kununua kwa jumla nikiuleta hapo Dar.Pili sina hakika kama huu mchele wa klm (Mabogini) unapendwa na walaji.Usije ukaniharibikia mikononi.
Hii habari ya kukoboa ni nzuri pia,lakini mkuu hiyo mashine ya kukobolea inakamatika??au ni ya kukodi?
Thanks mkuu.

Sema una mpunga kiasi gani, bei yako ngapi; in short weka tangazo la biashara watu wanunue!!
 
biashara ya chakula in Dar inaendeshwa na madalali
e.g ukienda tandika na mzigo wako wa mchele kutoka kyela unapokelewa na dalali ,then anakupa offer ya bei,ukikubali unauacha mzigo anatafuta wateja,unalipia kodi ya warehouse uliyoshushia mzigo wako,ndo unachukua kilichobakia.
njia rahisi kwako ni kutafuta wateja wako wa moja kwa moja.unatengeneza lebo yako ktk viroba vya 5kg upto 25 kg,then unatafuta soko la supermarket/individuals via facebook/jf etc then unafanya direct sales,kikubwa kwa wateja wa online wanataka uhakika wa Quality ya mchele na reasonable bei.

kila la kheri.
 
Nashukuru sana mkuu.
Hii habari ya kuuza supermarket kuna mheshimiwa mmoja pia huku ndani ameniambia,inaonesha its worth a try.Lakini jambo moja linanipa tabu,haka ka 1m hakitoshi kutengeneza na viroba then nianze kuzunguka kutafuta supermarket zinazohitaji huo mchele(au nawapigia tu simu/nawasiliana nao online?).

Nadhani nifanye kwanza ya kuuzia hao madalali na watu wa jumla then kikieleweka nitaingia kwa hao wa supermarket na wa online nikiwa na package zinazoeleweka.
Au sio mkuu?
 
Back
Top Bottom