Msaada wa ushauri

Song'ito

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
348
147
Habari wana jamvi,
sina hakika kama ninapost kwenye jukwaa sahihi ila nina shida ambayo ningependa mawazo ya wanajamvi wenzangu humu.
Kifupi mimi ni mwajiliwa wa chuo fulani cha binafsi hapa tanzania ambapo nafanya kazi kama mkufunzi msaidizi (assistant lecturer), ni nina shahada ya uzamili (MSc) katika sayansi ya komyuta toka chuo kikuu cha dar es salaam. Nimekuwa nikifanya kazi kwa nguvu na kujituma nilipokuwa kazini hadi kufikia hatua ya kusifiwa na utawala. Mwaka jana nilipata nafasi ya kwenda masomoni nje ya nchi kwa shahada ya uzamivu (phd) ambayo watu baki walinitafutia... kozi ilikuwa partial sponsered na hicho chuo cha nnje... Nilipotaka kuondoka kama kawaida niliomba likizo ya masomo na chuo kilikubali vzr na kuahidi kunilipa kama mfanyakazi maana nina familia hapa nchini (tulikubaliana kimkataba kabisa)..
Siku chache kabla ya safari yangu, chuo kilinigeuka ya kuwa hakinilipi kwa kuwa ninapata hela huko niendapo.... nikaona si mbaya niende mengine yatajulikana hukohuko... Kufika huko maisha yakawa magumu kwa sababu ya partial scolarship ukiachilia shule ngumu pia... watoto na jamaa wakaanza kuufukuzwa shule na kuhangaika hapa nchini... mbaya zaidi nilipaatwa na matatizo ya kuumwa ambapo nilipopimwa nilikutwa na tatizo kubwa la kiafya ambalo lilinifanya nisiweze kusoma vyema...
Nikarudi nchini na kueleza haya mawili kwa mwajili... cha ajabu mwajili ananilazimisha nirudi shule nikatibiwe huko ulaya kwa kuwa kuna matibabu mazuri... kutokana na hali ya ugonjwa sikuona vyema kurudi na nilimwomba ushauri hata professor wangu wa huko majuu juu ya hili nae alikubali kuwa kwa kazi zilivo ngumu na demanding ni heli nipumzike...
Shida ni kuwa mwajili ametishia kutokunirudisha kazini, je hii ni sahihi wakuu? na nn nifanye mana nimechanganyikiwa huku familia ikinitegemea pia.... uwezo wa kupata kazi upo ila kama wote mjuavyo si rahisi na haiwezi kuwa kwa muda mfupi.... naomba ushauri wenu wakuu kwa wale wenye uzoefu wa mambo haya
 
Pole sana mwalimu.
ushauri wangu, kama uko dar uende wizara ya kazi, labour department. Iko pale akiba. Hapo uende na papers zako zote ikiwa ni pamoja na salary slip ya mwisho na barua ya kukuruhusu kusoma. Hapo unaonewa tu, komaa hadi kieleweke.
isitoshe, muajiri kama mlikuwa na mkataba wa kupeana matibabu, anahusika wakati wote ukiwa nchini.
 
Pole sana mwalimu.
ushauri wangu, kama uko dar uende wizara ya kazi, labour department. Iko pale akiba. Hapo uende na papers zako zote ikiwa ni pamoja na salary slip ya mwisho na barua ya kukuruhusu kusoma. Hapo unaonewa tu, komaa hadi kieleweke.
isitoshe, muajiri kama mlikuwa na mkataba wa kupeana matibabu, anahusika wakati wote ukiwa nchini.

asante sana mkuu king'asti... asante kwa ushauri mzuri!! nitafanya hivo..
 
Back
Top Bottom