Msaada wa ushauri unatosha kuniokoa katika hili

Sangoma

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
342
162
71ca9ad95104a6e79150fef617993bd6.jpg
Habari za majukumu wapendwa! Nahitaji kupata ushauri wenu wa kimawazo nimenunua eneo dogo tu lenye urefu wa mita 54 na upana wa mita 24 nahitaji kufanya kilimo cha kisasa cha mbogamboga au matunda eneo liko na maji ya kutosha kwa muda wa mwaka mzima plz wenye kuwa na ushauri naomba ushauri wenu nini nifanye katika eneo hili ili niweze kujiingizia kipato,eneo nililopo ni Serengeti mkoa wa Mara kuhusu elimu ni kidato cha nne.
2208d36748377ba5eeab6fc56bcc0b3a.jpg
b02cee4cd1ee0dbb71625156c1b34272.jpg

a91868dbac35399d518241bf96fdf93a.jpg

0aad3036650ccc676e1ee7eec6615520.jpg
82b9b425856aa93fe12dbc4cc547349a.jpg
042d0f93f80dc1e2cc08fbb08bbbc24a.jpg
 
Eneo zuri sana kwa kilimo. Ungeangalia kwanza watu wa karibu yako/wilaya wana upungufu na zao gani. Halafu ndo ukifanyie kilimo.
 
Hongera sana kwa hatua hiyo!, mi nadhani ungeangalia mazingira ya hapo kuhusu kilimo wanacholima then angalia mahitaji ya mazao sokoni alafu pima uzito kwa uwezo wako
 
Kwa msimu huu lima tikiti. Ila tafta mtahlam wa kilimo cha aina hii. Mtahalam simaanishi afisa kilimo. Naongelea mwenye experience ya kilimo kama icho maeneo hyo.
 
Jiulize na utafute majibu ya maswali yafuatayo utapata kitu sahihi cha kufanya. Nini kinahitajika( nitauza nini ?), Nitauza wapi ? Wakati gani kinahitajika ? Gharama zake zipoje? Unaweza kulima mchicha ukapata fedha nyingi kuliko zao lolote ila je ulipo unaweza kuuza mchicha ? Je unaweza kuuza mchicha msimu wowote au ni kiangazi tu,kwa kuwa masika kuna mbogamboga nyingi?
 
Back
Top Bottom