msaada wa mawazo tafadhali...

shopping

Member
May 29, 2012
20
10
mi na baadhi ya wenzangu tupo masomoni nje ya nchi, kuna mwenzetu mmoja ana tatizo, ni kwamba jina lililopo kwenye passport yake ni tofauti na majina ya kwenye vyeti vya form 4 & 6. hapa chuoni kafanyiwa usajili kulingana na majina yaliyopo kwenye vyeti vyake, lakni idara ya uhamiaji wamegoma kumpa kibali cha kuishi huku kutokana na majina yake kutofautiana, wao wanadai kwamba inabidi afanye usajili kulingana na majina yaliyopo kwenye vyeti ndo watampa kibali cha kuishi, lakini nadhani km akifanya hivi cheti chake cha mwisho kitatoka na jina hilo lililopo kwenye passport ambalo ni tofauti na vyeti vingine, hili litamletea shida baadae (kuwa na vyeti vyenye majina tofauti)...sasa wadau naomba ushauri wenu ili kuweza kumsaidia huyu mwenzetu, hapa kuna options mbili, aidha kukubali kuwa na vyeti vyenye majina tofauti au kubadili passport, suala ambalo ni gumu...



mchango wako ni muhimu sana lakini usitukane jamani..ahsanteni
 
hamna mtu anayeruhusiwa kuwa na mjina tofauti labda kama ni a.k.a. fanyeni utaratibu wa kuingia mahakamani ili ale kiapo cha majina yapi kati ya hayo atakuwa akitumia. waoneni watu ubalozini kwa msaada zaidi kwani ubalozi upo kwa ajili ya mambo km hayo.
 
Back
Top Bottom