Msaada wa mawazo plz

Prodigal Son

JF-Expert Member
Dec 9, 2009
1,067
700

Ningeomba mnishauri ndugu zangu nafasi ya hawa watu kama mtu anataka kuoa au kuolewa. SHANGAZI, BABA MDOGO/MKUBWA PAMOJA NA WATOTO WAO.

Kwa kifupi Baba ameshatangulia mbele ya haki na kwa mila za huko kwa akina XPIN mtoto wa kwanza wa kiume ndo anatakiwa achukue nafasi ya Ubaba,ndio nilikabidhiwa ubaba.

Niliowataja hapo juu baba ndo aliwasaidia saana wao hata na baadhi ya watoto wao,familia yetu hatuna ule ukaribu nao since walikuwa hawampendi mama, na walikuwa wanamwogopa saana mzee, majuzi tu dada mkubwa akanifuata ( kama baba yake) akaniambia anataka afunge ndoa ikabidi nimpe mama taarifa, Ikabidi yeye awatarifu hao wandugu niliowataja hapo juu, kwa sasa hakuna amani kabisa kila mtu anaongea lake wanamlazimisha dada aende kijijini wazee wa ukoo wakambiwe, wapewe pombe, mahari ilipwe na mambo kibao.

Dada kanifuata ananiambia sasa afanyeje nikamwambia anipe muda kidogo, Baada ya kuwaza saana nimefikia maamuzi haya hatuendi Kijijini,,,, hatutafanya sherehe ya kumwaga badala yaka tutaandaa chakula tu cha jioni na kuepusha maneno harusi yake ataenda wadogo zake tu wa kike,,hao mashangazi na watoto wao nimeona ni jambo la busara kuwa ignore

Naamini hapa Jamvini wapo wazee ( namaanisha watu wenye busara ) naomba ushauri wenu kabla sijamjulisha dada maamuzi niliyofikia.

natanguliza shukrani
 
Unajua hata baba yako walielewana nae kwa sababu alikuwa na kitu mama yako hawakumpenda kwa kuwa walihisi ni kikwazo kwa maslahi yao. Bint aolewe kama amempata mwenza. Fuata taratibu ambazo unaamini ni sahihi kwa mujibu wa kabila lako na dini yako. Ikwezekana tafuta mzee mwenye busara wa kabila lenu na mchungaji washirikishe kwa nyakati tofauti baada ya hapo kaeni kama familia mtapata jawabu.
Tafakari
 
Unajua hata baba yako walielewana nae kwa sababu alikuwa na kitu mama yako hawakumpenda kwa kuwa walihisi ni kikwazo kwa maslahi yao. Bint aolewe kama amempata mwenza. Fuata taratibu ambazo unaamini ni sahihi kwa mujibu wa kabila lako na dini yako. Ikwezekana tafuta mzee mwenye busara wa kabila lenu na mchungaji washirikishe kwa nyakati tofauti baada ya hapo kaeni kama familia mtapata jawabu.
Tafakari

Asante Meku Ringo Ntaufanyia kazi ushauri wako, ubarikiwe
 
Ngoja nijaribu busara zangu hapa;
Prodigal Son, naomba nim-quote baba yangu 'Kama nikiamua kumlipizia kial mmoja ambaye aliniumiza au kutokunijali wakati I was a nobody, basi sina ndugu hata mmoja wa kumsalimia' Ushauri wangu ni kuwa angalia mila zinasemaje, do the minimal (angalia isikuumize sana kiuchumi). Kama ni pombe wape kwa kiasi cha uwezo wako. Final say itoke kwako lakini ukijitahidi kumpa raha dada yako. Waambie tu, si vizuri kuweka bifu kwa sana na ndugu, undugu haununuliwi dukani.
Mwisho wa yote, immediate family yako ndo ifurahike. all the best, ndo complications za uafrika hizo japo zina starehe yake!
 
Ni kwa kuwa umeamaua kuingiza mabo ya mila za kwenu; ingekuwa mimi ningeshikilia msima wangu wa kiimani; Ukiacha zile amabazo hazina madhara kwa wakati tulionao kuna mila nyingine hazitekelezeki kila sehemu. Naunga na wanaosema fanya yaliyo ndani ya uwezo wako! usijiumize!

Afret all this thing is yours!
 
Back
Top Bottom