Msaada wa mawazo namna ya kuanzisha chekekechea( english medium)

CHIMPONGO

Member
Feb 6, 2012
43
3
Nimehamia katika mji flani ambao kwa sasa ni makao makuu ya wilaya. katika kuangalia biashara gani naweza kuifanya nimepata wazo la kuanzisha chekechea kwa kuanzia na baadae daycare kwani hakuna huduma hiyo katika haka kamji.
sasa wadau naombeni msaada wenu wa taratibu za kisheria ili uruhusiwe kuanzisha, pia mtaji wangu ni mdogo ka m 6 na nataka nianze kwa kukodi jengo. Je nikiaanda b/plan ni mashirika gani yaweza kunisupport?
 
Mkuu jaribu kuwasiliana na NGO's kama TWAWEZA, Haki Elimu n.k. Lakini pia ni lazima upate vibali kutoka Wizara ya Elimu kupitia Halmashauri ya Wilaya ulipo.
 
Wizara za elimu, maendeleo ya jamii wakishirikiana na idara ya ustawi wa jamii wametoa minimum standards(viwango) kwa vituo/shule hizo zitafute usome kwanza kuhusu majengo,sifa za walimu etc. Ila wazo lako zuri keep it up! Pia ujue day care (watoto wa 3 to 4yrs) zipo chini ya idara ya ustawi wa jamii. Pre primary( watoto wa 5 to 6yrs) iko chini ya wizara ya elimu
 
rafiki yangu alianzisha training college kwa amount hiyo hiyo ya mil 6!!! hakuna haja ya kuzunguka kote huko, usajili chini ya NACTE uligharimu tshs laki 9 ambao ni muhimu kuwa nao ( nimesahau alipopata usajili) ...mengine ss ni wew mwenyew kujua aina ya furniture utakazo tumia n other facilities....Kama hapa dar shule nyingi za nursery /day care watu huwa wanapangisha nyumba nzima then vyumba ndo vinakuwa madarasa...sitting room inatumika kama dining ya watoto n.k NILICHOJIFUNZA MIMI UKIOMBA USHAURI KUHUSU KUFANYA/KUANZISHA BIASHARA WATU WATAKUKATISHA TAMAA KUWA MTAJI WAKO MDOGO NA WENGINE WATAKUBEZA....HIYO HELA INATOSHA SANA CHA MUHIMU NI JUHUDI ZAKO MWENYEWE....I'm telling you from experience
 
Back
Top Bottom