sosoliso
JF-Expert Member
- May 6, 2009
- 8,539
- 9,462
Wana JF naomba mnijuze jinsi ya kusafiri na basi kutoka Dar es Salaam kwenda mkoa mpya wa Katavi.. Pia gharama za nauli.. Au mwenye contacts za mabasi yanayoenda huko na haswa Sumri.. Nimejitahidi kutafuta kwenye net nimewakosa.. So naomba kwa anaejua anisaidie kwa hili.. The sooner the better..
UPDATE
Wakuu ninashukuru kwa msaada wenu.. Nilifanikisha safari yangu kwenda Mpanda kupitia Mbeya Tunduma.. Sumbawanga mpaka Mpaka.. Kuondoka nilipita Tabora na kuunganisha mpaka Dar.. Nilichokiona huko ni kutokuwapo kwa lami kuanzia Tunduma mpaka Mpaka Mpanda.. Japo kuna makampuni yanatengeneza barabara nimeambiwa karibu mwaka sasa hakuna kipande chochote kilichokamilika.. Na vile vile kutoka Mpanda mpaka Manyoni (kupitia Tabora) kote ni barabara ya vumbi japo nako barabara inatengenezwa muda hakuna kipande ambacho kimeshakamilika..
Naambatanisha na picha za Mpanda
View attachment 68686
View attachment 68687
View attachment 68689
Hii ndio nyumba ya Mh. Waziri Mkuu pale Mpanda..
View attachment 68693
Ndio barabara yenyewe hiyo..
View attachment 68695
View attachment 68698
Kamanda anamwaga sera kwenye basi.. Hapo anasikiliza maswali toka kwa abiria.. just an ordinary guy..!
Kweli Mpanda ni CDM kwenda mbele..
Nawacilisha...