Msaada wa kisheria

Mwanantala

Senior Member
May 13, 2010
130
26
Heshima mbele wakuu! Naleta mbele yenu maombi yangu ya mwongozo wa kisheria juu ya mwenendo sahihi wa mashtaka katika hili: Jirani yangu aliomba nimkopeshe shilingi laki moja na nusu mnamo Juni mwaka huu na aliahidi kuzirejesha mara baada ya mshahara kutoka wa mwezi husika kutoka. Nilimpatia pesa hizo kama alivyohitaji. Muda ulipowadia hakutimiza ahadi na badala yake akanidanganya kwamba ameomba mkopo nmb benki na hivyo nimpe laki nne na nusu ili akamilishe taratibu za huo mkopo ambao angetumia sehemu yake kunilipa jumla ya laki sita nilizomkopesha. Nikampa. Cha kusikitisha toka nimpe hela zangu ameanza kuonyesha kunitapeli. NAOMBA WAKUU MNIELEKEZE JINSI YA KUPATA HAKI YANGU.
 
Mkuu, Makubalinao yenu yana ushahidi wowote (maandsihi au mashuhuda?). Kama milnuia kuyafanya kuwa ya kisheria, tumia vielelezo mlivyotumia kukubalina kudaia ikiwemo ushahdi wa kuwa ulimkopesh. Ikishindikana hivyo ndivyo vitakusaidia mbeleni kwenye sheria.
 
Nina mashahidi wa mdomo na sms zake.
 
Nina mashahidi wa mdomo na sms zake.

Duh! sijui kama hizo zitatosha kufungua kesi ya madai madogo (small claims) lakini jaribu kwani kujaribu hakuna madhara. Kwani uko wapi?

Na safari ijayo ukimkopesha mtu hakikisha mnaandikishiana IOU (I Owe You)...
 
Niko Bukoba.
 
Nina mashahidi wa mdomo na sms zake.

Tafuta Wakili yeyote atakusaidia kwa gharama zako ambazo utaomba zirudishwe na mlalamikiwa baada ya wewe kushinda kesi, otherwise unaweza kuingizwa mjini hivi hivi ndugu kama ilivyoanza kuonekana!
 
Asante sana kwa ushauri wako. Nafanyia kazi.
 
Heshima mbele wakuu! Naleta mbele yenu maombi yangu ya mwongozo wa kisheria juu ya mwenendo sahihi wa mashtaka katika hili: Jirani yangu aliomba nimkopeshe shilingi laki moja na nusu mnamo Juni mwaka huu na aliahidi kuzirejesha mara baada ya mshahara kutoka wa mwezi husika kutoka. Nilimpatia pesa hizo kama alivyohitaji. Muda ulipowadia hakutimiza ahadi na badala yake akanidanganya kwamba ameomba mkopo nmb benki na hivyo nimpe laki nne na nusu ili akamilishe taratibu za huo mkopo ambao angetumia sehemu yake kunilipa jumla ya laki sita nilizomkopesha. Nikampa. Cha kusikitisha toka nimpe hela zangu ameanza kuonyesha kunitapeli. NAOMBA WAKUU MNIELEKEZE JINSI YA KUPATA HAKI YANGU.

Gharama ya kudai kiasi hiki inaweza kuwa ni kubwa kuliko fedha yenyewe. muda utakaotumia, usumbufu etc, next time usimkopeshe mtu, usidhamini mkopo anaopewa wala usimuwekee dhamana mtu ambaye sio ndugu yako vinginevyo wema wako utakuponza kama inavyotokea sasa hivi.
 
Hata kam ni ndugu yako mdau,la msingi hakikisha kila kitu unachofanya kinakuwa katika maandishi ya kisheria!
 
Back
Top Bottom