Msaada wa kisheria

ossy

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
872
143
heshima yenu wakuu! Naomba ushauri wa kisheria,nilimuuzia jamaa mmoja gari ni siku kama kumi zilizopita,hatukuandikishiana sehemu yoyote,lakini nilimpa kadi ya gari,niliuza nikiwa na lengo la kuagiza gali nyingine,lakini kutokana na bkodi zilivyopanda,nataka nimrudishie hela yake anipe gari yangu,je sheria inasemaje hapo? Hakukukuwa na shaidi yoyote kati yetu! Nawakilisha!
 
Yaani wewe unachotafuta ni kufundishwa namna ya kudhulumu. Cha muhimu ni namna ya kutafuta kuandkishana kisheria ili jamaa amiliki kaw raha zake.
 
ctaki kumdhulumu,nataka kumrudishia pesa yake mkuu!!!!!
 
hapo unatakiwa uinunue tena hiyo gari ndo mwandikishiane kwani ameshaimiliki na ukifanya tofauti ya hapo kulazimisha utakuwa unadhulumu
 
Je sheria za ajira kwa watumishi walioajiriwa serekalini kwa watumishi wanaojiendeleza kimasomo wakijilipia ada na mahitaji mengine je sheria inawapa ulinzii gani? na je kuna haki yoyote wanayostahili kupata kutoka kwa muajiri? naomba msaada na maelekezo
 
heshima yenu wakuu! Naomba ushauri wa kisheria,nilimuuzia jamaa mmoja gari ni siku kama kumi zilizopita,hatukuandikishiana sehemu yoyote,lakini nilimpa kadi ya gari,niliuza nikiwa na lengo la kuagiza gali nyingine,lakini kutokana na bkodi zilivyopanda,nataka nimrudishie hela yake anipe gari yangu,je sheria inasemaje hapo? Hakukukuwa na shaidi yoyote kati yetu! Nawakilisha!
Kalinunue tena kwake (kama atakuwa tayari kuliuza) maana limekuwa la kwake! Usifikiri kama hamjaandikishana na kama hakuna ushahidi wa mtu mwingine basi mauzo si halali! Hiyo kadi ya gari imeendaje kwake na hilo gari limeendaje kwake kama hujampa?
 
Nia yenu ilikuwa nini wakati mnauziana kama haikiuwa mkataba?

Mkuu, jaribu kutafuta jingine au vipi mkubaliane akurejeshee kwa uungwana au ununue kwake na sio vinginevyo.
Ulipaswa ujue kabla bei za gari kwenye soko kabla ya uamuzi wa kuioza hiyo.
 
Je sheria za ajira kwa watumishi walioajiriwa serekalini kwa watumishi wanaojiendeleza kimasomo wakijilipia ada na mahitaji mengine je sheria inawapa ulinzii gani? na je kuna haki yoyote wanayostahili kupata kutoka kwa muajiri? naomba msaada na maelekezo
Soma Standing Orders for Public Service, 2009 utayapata hayo yote!
 
Maadam jamaa kanunua gari, kakupa chako nawe umemkabidhi mpaka kadi ya gari, endapo unalihitaji gari hilo ongea naye biashara akikubali atakuuzia kwa bei ya maelewano.
 
heshima yenu wakuu! Naomba ushauri wa kisheria,nilimuuzia jamaa mmoja gari ni siku kama kumi zilizopita,hatukuandikishiana sehemu yoyote,lakini nilimpa kadi ya gari,niliuza nikiwa na lengo la kuagiza gali nyingine,lakini kutokana na bkodi zilivyopanda,nataka nimrudishie hela yake anipe gari yangu,je sheria inasemaje hapo? Hakukukuwa na shaidi yoyote kati yetu! Nawakilisha!

Kuwa muungwana. Definitely ukienda polisi ukaripoti kuwa gari yako imeibiwa na kadi yake...blaa blaa, jamaa atakamatwa kwa wizi/kupatikana na mali ya wizi. He will be in trouble!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! kama true you were two only in this unprofessional transanction. Kuwa muungwana, mwendee umueleze nia yako kuwa umebadili mawazo. Lakini katika hali ya kawaida, a controversial contract has been concluded between you and him/her.
 
Acha tamaa za fisi wewe gari umeshauza alokuambia mkataba hadi uwe wa maandishi nani? hata ushahidi wa mazingira utamuokoa huyo bwana endapo utahamua kupretend kuwa gari imeibiwa na kadi yake. cha msingi panda dau akikubali fanyeni biashara akikataa sahau. vinginevyo huo sasa utoto kama si dhuluma na hakuna dhuluma iliyowahi kumfikisha mtu mbali utaumbuka.
 
UNAWEZA KUICHUKUA WALA HAMANA UGUMU HAPO SWALA NI KUELEWANA TUU NA MTEJA WAKO,KAMA MLIVYOAMINIANA NA KUUZIANA BILA KUANDIKISHANA NENDA ONGEA NAE KAMA AKIKATAA HUWEZI KUMLAZIMISHA NA AKISEMA UONGEZE DAU HUNA UJANJA FANYA HIVYO ILI UJIFUNZE WAKATI MWINGINE UWE JANUANISM ,AKIKUZINGUA NIPM NINA GARI NZURI ZA BEI yoyote HAHAHA;
 
Back
Top Bottom