Msaada wa kisheria Tafadhali

Nyati

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
2,489
1,813
Wakuu heshima mbele

Mwanzoni mwa mwezi septemba nilikuwa na sherehe ya harusi. Kama ilivyo kawaida watoa huduma mbali mbali walijitokeza kuomba kutoa huduma katika sherehe hiyo. Walijitokeza wanne katika huduma ya Video na picha za mnato. Bei kati ya 400,000 wachini na wa juu 900,000/=.

Wajumbe walikubaliana kuwa yule wa 900,000/- apewe kwa jinsi alivyojinadi kuwa yeye ni professional, pia walidai kuwa gharama ina-determine ubora ya kitu. Alihahidi pia kutoa huduma ya picha za mnato kama offer. Aliahidi kuleta screen mbili ukumbini (live) na kutoa DVD na VHS tapes baada ya wiki moja tu, ahadi zote hizi zilitolewa kwa maneno.

Jamaa akapewa tender bila kuwa na written agreement. Siku ya harusi alifika na kupiga picha za video kama alivyoahidi na screen mbili pia alizileta, picha za mnato alipiga mtu mwingine aliyeletwa naye. Ndani ya wiki moja hivi jamaa alileta picha za mnato ( Yule wa pili). Lakini DVD na VHS zikaanza kuwa hadithi za alinacha, mara hivi mara vile. Mara zote amekuwa akiahidi atatoa siku fulani na siku ikifika ni hadithi kwa kwenda mbele.

Akawa anafuatiliwa ofisini kwake maeneo ya “Sea view” mara kwa mara. Mara ya mwisho akadai kuwa yeye yupo Zanzibar, ndipo mmoja wa vijana pale ofisini kwao akanitaarifu kuwa huyu jamaa alipata tender siku ya pili ya harusi husika, na baada ya kukosa tapes akafuta “overwrite” moja ya tape za harusi yetu, na hivyo kupoteza matukio yote muhimu ya kanisani , na pia ukumbini kama vile utambulisho wa wazazi wa pande zote mbili, kutoa nasaha n.k. Hivyo yeye anayo tape aliyoweka baada ya ile ya kwanza kwisha ambayo ina matukio ya kutoa zawadi, kufungua muziki tu na kuondoka ukumbini. Mtoa taarifa alihadharisha kuwa kuna uwezekano na hiyo akaifuta pia kwani ndizo zake. Yule kijana akalaumu kwa nini alilipwa pesa yote, akasema kuwa huyu ukishamlipa basi umeumia kwani uwa hakujali tena na vile vile ni mtoto wa kigogo hivyo umeumia. Akadai watu wengi kwa kutokujua huwa wanajuta. Taarifa hii sikuiamini hata kidogo, kwani haiingii akilini, lakini siku zinavyozidi kwenda naanza kupata wasi wasi hivi sasa ni karibu mwezi wa pili bado anapiga chenga.

Sasa naomba ushauri kama kuna sheria yeyote inayoweza kutumika dhidi yake (Ikitokea ikawa ni kweli) kwani kama nilivyoeleza pale juu hakukuwa na mkataba wa maandishi, bali makubaliano ya maneno tu ingawa kuna mwanakamati aliyempigia debe kwa sana. Na sasa amesema asimpigiwe simu wala nini bali yeye akiwa tayari atalete hivyo vitu. Naomba ushauri hiki kitu ni cha kweli kabisa wana jamvi.
 
Makubaliano hata ya maneno bado ni mkataba ila ushahidi utakuwa mgumu zaidi. Nadhani pia unaweza ukapata court order upewe tape yako, at least iliyobaki. Au jaribu kuongea na huyo kijana akupitishie hiyo tape bila jamaa kujua.
 
Nashukuru kwa Ushauri, nilikuwa sijui kuwa hata bila maandishi bado kuna mkataba. Ushahidi ni mwingi tu mkuu
 
Kama tender alipewa mbele ya wanakamati..na wanakamati wako tayri kuwa mashahidi..hiyo ni valid contract..unaweza kumshitaki na ukashinda kesi..
kwakuwa atashindwa kukupa dvd inawezekana mahakama ikaamua ulipwe damages...
 
Mkuu, unaushahidi wa kutosha wa kumburuza huyo jamaa mahakamani...mkataba upo na mashahidi wa mkataba huo wapo, events zilizoambatana na utekelezaji wa mkataba huo zinaweza kuwa prima facie evidence vile vile...unaweza ukadai atekeleze (akamilishe makubaliano yenu) i.e specific perfomance of contract au alipe hasara na usumbufu ulioupata kwa kutofanya hivyo...undani wa makubaliano yenu mnajuwa wenyewe na waliohusika lakini jamaa hawezi kukataa(estoped) kuwa kuna specific part of your agreements needed to be completely perfomed...but the onus of proving the contrary will lie on him.
Dai haki yako Mkuu, ila tahadhari na kufanya makubaliano bila ya kuweka kumbukumbu kwa maandishi...kadhalika unapompa mtu tenda hasa independent contractors,lazima uwajuwe vizuri na upate records zake za kazi zake mbili tatu na namna alivyoatekeleza...najuwa mambo ya shughuli yanakuwa na harakati nyingi mpaka vitu vingine mnavi-overlook, lakini uangalifu ni jambo la msingi katika mambo ya fedha na mikataba.
 
Back
Top Bottom