Msaada wa kisheria kidogo

nickson1987

Senior Member
Aug 16, 2011
191
24
Naombeni ushauri mimi nilichukua pesa laki nane tu kwa ajili ya biashara, ya chips ila haikunilipa mtaji ulikata wote, ingawa nilikuwa na familia ya watoto watatu, na mke mmoja nime teseka Kwa muda miaka miwili na nusu huku mwenye pesa ana taka pesa yake yote, akanipeleka mahakamani, na mahakamani wamenipa mwenzi mmoja nilipe kweli ni haki kweli! Nisipo lipa nawekwa ndani familia yangu itaishije naombeni ushauri
 
Mkuu,

Ulipaswa kuiomba mahakama ikupe unafuu wa kulipa hilo deni kidogo kidogo mpaka liishe mkuu.

Nina uhakika wangeweza kukuelewa kama ungewasilisha hoja za msingi mahakamani.
 
Mkuu,

Ulipaswa kuiomba mahakama ikupe unafuu wa kulipa hilo deni kidogo kidogo mpaka liishe mkuu.

Nina uhakika wangeweza kukuelewa kama ungewasilisha hoja za msingi mahakamani.
Asante ndgu yang kwa ushauri wako ila kuna watu wameniambia ya kwamba ili niweze kusikilizwa lazima niwe kiasi Kidogo ya sehemu ya hyo pesa halafu nitaongezewa tena muda wa kumaliza deni
 
Asante ndgu yang kwa ushauri wako ila kuna watu wameniambia ya kwamba ili niweze kusikilizwa lazima niwe kiasi Kidogo ya sehemu ya hyo pesa halafu nitaongezewa tena muda wa kumaliza deni

Ndiyo maana nimekwambia uwe na hoja za hoja za msingi za kuishawishi mahakama katika maombi yako mpaka ikubaliane na wewe. Hivyo hiyo ya kutaka kutoa sehemu fulani katika deni lako ni ushawahi mzuri tu siyo mbaya.
 
Back
Top Bottom