Msaada wa haraka wadau wa MMU, Hali ni mbaya sana!!

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,401
92,736
Nawasalimu wadau wote wa MMU.
Namuuguza mama yangu mzazi sasa yapata wiki ya pili baada ya kumfanyia vipimo vya xray pale Hindu mandal majibu yameonesha kwamba anasumbuliwa na tatizo la moyo kuwa mkubwa, pili upungufu wa calcium yaani mifupa kuanzia kiunoni kuja chini imesagiga, na mishipa yake ya damu imesinyaa.

Sasa basi ile dozi aliyopewa Hindu Mandal inabidi atumie siku 14 lakini bado haijamsaidia lolote zaidi ya kuwa kwenye maumivu makali sana mpaka kufikia kulia, sijkuwahi kumuona mama yangu akilia kwa ugonjwa.
Sasa nahitaji msaada kwa member yeyote anaemfahamu specialist wa magonjwa hayo wa Muhimbili Hospital ili nifanye utaratibu wa kumuona leo hii, kumbukeni siwezi kwenda kichwa kichwa muhimbili kwani kuna mgomo wa madaktari.
N:B. Nimeiweka hii thread hapa kwa sababu nahitaji msaada wa haraka leo hii, mods naomba muiache hapa hapa.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Pole sana mkuu,
Hapa hutatoka mikono mitupu kwan ni wengi wanapita humu,
Vuta subira watakuja!!
 
Pole sana Matola

Ngoja waje wanaojua madaktari pale muhimbili
Mungua akutangulie katika kila jambo
 
Am still waiting, nimeshatuma gari imfuate mama nyumbani kwake, hapa mtaani kuna X Dr mmoja wa Muhimbili ni mlevi sana ndio kuna dogo ananisaidia kumtafuta kwenye vijiwe vya pombe saa hizi, nikimpata huenda akanisaidia pia
 
Ohh pole sana Matola pamoja na mama.
Hopefully atapata msaada anaohitaji ASAP!!
 
Urudi kwa daktari au nenda na hayo majibu kwa specialist wa magonjwa ya moyo au nenda pale Dar group.
 
Hebu M-PM Dr. Riwa anaweza kukupa ushauri, labda ano rafiki zake wenye utaalamu huo.................Pole sana mkuu
 
Urudi kwa daktari au nenda na hayo majibu kwa specialist wa magonjwa ya moyo au nenda pale Dar group.
Dar Group ndio Hospital anayotibiwa mama yangu siku zote, na alishawihi kulazwa pale mwaka jana mwezi wa 7 kwa tatizo la moyo kuwa mkubwa ila sasa hivi ndio xray imeonesha magonjwa kuongezeka.
Sihitaji tena Hospital za kufanyana dili, nahitaji Specialist niko tayari kutumia mpaka my last coin. Hapa nahitaji information za kumpata specialist au namba za simu.
 
Mi simjui doctor lakini pia jaribu kutafuta osteocare na cardioace ni dawa zinazowasaidia wagonjwa wa moyo pia ni kama multivitamin madoctor mi si mtaalumu sana ila ndugu yangu anatumia mfano osteocare ina calcium nyingi,
 
Dar Group ndio Hospital anayotibiwa mama yangu siku zote, na alishawihi kulazwa pale mwaka jana mwezi wa 7 kwa tatizo la moyo kuwa mkubwa ila sasa hivi ndio xray imeonesha magonjwa kuongezeka.
Sihitaji tena Hospital za kufanyana dili, nahitaji Specialist niko tayari kutumia mpaka my last coin. Hapa nahitaji information za kumpata specialist au namba za simu.

Matola
Kwa nini usi PM dr klinton kule jukwaa la siasa, atakusaidia ths mkuu
 
pole sana mkuu mungu atakupigania mama apone, endelea kumtanguluza mungu kwa kila jambo,
 
Vuta subira Kaka. Wataalamu watakuja muda si mrefu. Usi panic.
 
Pole sana best nenda Taasisi ya moyo pale kinondoni leaders mtafute dr masao ndiye specialist wa ugonjwa wa moyo atakusaidia kwani amemsaidia mama yangu alikuwa na tatizo la moyo mkubwa 2007 amepona tangu 2008 ukimuona uwezi kuamini kwani anamiaka 65 ni dr mzuri sana tena wanahuduma nzuri pale na dawa poa but kuna masharti yakufuata kama kuacha kula chumvi.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom