Msaada wa haraka sana

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
Tafadharini sana,
Nilimtumia mtu pesa mwezi wa July (CRDB),nikamtaarifu akasema sawa ila inaonekana (labda hakwenda kuangalia benk).
Leo ananitafuta anasema SIKUWEKA hela!!!!!!!!!

tatizo langu ni kwamba,kuna namna naweza kupata statement ya benki ukizingatia "pay slip" nimepoteza na nili-deposit dar es salaam na kwa sasa nipi mwanza????
 
yap mbona simple? kama una uhakika uliweka hiyo pesa mwambie aende branch yake hapohapo mwanza akaombe bank statement ya mwezi July af acheck transactions zote za mwezi huo!
 
Dah pole sana ndugu yangu wee mwambie huyo uliyemtumia hela akacheck na benk yake wampe statement ya mwezi July maana haiwezekani uweke hela mwezi July then mtu aseme leo hajaziona ina maana hajawahi kuitoa hela toka wewe ulipomuwekea?? Au ulimkopesha anatafuta jinsi ya kukwepa kukulipa deni lako??? Mwambie afatilie statement kuanzia July mpaka Seotember atapata ukweli
 
Mkuu, inawezekana huyo jamaa anakuchanganya tu, au kweli hiyo pesa haikuingizwa kwenye hiyo akaunti.
Mbaya kuliko ni wewe kutupa pay-in-slip!! too bad, kwenye statement pesa ikionekana haikuingia inakula kwako!
Imeshanitokea NBC, na last week jamaa yangu imemtokea tena. Kuna baadhi ya wafanyakazi si waaminifu. Wanakuchunguza kama hauna tabia ya kuchukua pesa mara kwa mara au kuangalia salio, ukienda au ukituma mtu kuweka hawaingizi kwenye akaunti yako,...wanajikopesha! Nilituma mtu akaenda kuniwekea kiasi cha 5.6M, baada ya siku kadhaa nikaenda kuchukua kiasi flani cha pesa (nikiwa na uhakika kuwa salio langu la zamani ukijumlisha na pesa iliyowekwa inatimia pesa nayohitaji) To my astonishment nikaambiwa salio halitoshelezi!!, kufuatilia hiyo 5M haionekani! Bahati nzuri pay-in-slip iko kwenye file, imegongwa mhuri na sahihi ya teller aliyepokea!!!! Walinipa hiyo pesa na yule jamaa naskia wamemtoa dirishani!!
My take: Tuwe makini sana na pesa, tunza receipt zote za malipo, huo ndy ushahidi wako!
 
Back
Top Bottom