Msaada:Vita ya dunia

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
5,759
5,289
Najiuliza kila siku eti zile vita zinazoitwa vita za dunia(1&2) zilikuaje?? Kwamba kila nchi inakuwa kwenye mapigano?? Unapigana na nani na kwanini?? Au yoyote yule aliye mbele yako halali yako? Pia zillikuwa zinaanza siku moja kwa mpigo au? Maana sielewi elewi wakuu!! Mtu mwenyewe wa 1980s mimi
 

Nadhani hapa haujamsaidia zaidi ya kumfanya aendelee kuwa mjinga, ulipaswa kumjibu kwamba do not underestimate the power of Google, haiwezekani mtu anatumia Internet halafu anakuja na maswali ya kitoto kabisa.
 
msaidieni pengne historia hajawah soma... Pengne ameisoma sana hadi imemchanganya...Pengne hajawah kupata hata m2 wa kumsimulia... Pengne ameamua kuongeza thread....
 
msaidieni pengne historia hajawah soma... Pengne ameisoma sana hadi imemchanganya...Pengne hajawah kupata hata m2 wa kumsimulia... Pengne ameamua kuongeza thread....

pengine hamjaelewa swali langu.Semeni basi nirudie
 
i thnk ths isn't fair. ye kazaliwa miaka ya 80 (may b 1989) we unasema ana 32. after row no1 knows everythin.don' crtcze
 
Nenda Wikipedia utapata maelezo ya kutosha kuhusu vita zote mbili. Kwa kifupi:
1. Vita Kuu ya Kwanza ilikuwa kati ya Ujerumani (na nchi washirika wake wachache) dhidi ya mataifa mengine ya Ulaya. Sababu kubwa ni ushindani wa kibepari na kibeberu. Ujerumani ilitaka makoloni zaidi ya yale iliyopata katika mgawano wa Berlin (Tanganyika, Rwanda/Burundi, na sehemu ya Cameroon ya sasa). Hivyo kwa kujiamini Ujerumani ikaanzisha vita ikiamini ingeshinda na kuongeza makoloni pamoja na sehemu zingine za Ulaya Mashariki (hasa Balkans). Ujerumani ilishindwa ikanyang'anywa hata hayo makoloni iliyokwa nayo.
2. Baada ya kushindwa Ujerumani ilijijenga upya kijeshi na kiuchumi. Ndipo Adolf Hitler alipoanzisha Vita Kuu ya Pili. Mara hii lengo halikuwa makoloni bali kuwa mtawala wa dunia zikiwemo na nchi kubwa za Ulaya kama Uingereza, Ufaransa, n.k. Hii iliambatana vile vile na itikadi kuwa watu wengine kama waaafrika, waarabu, wayahudi, n.k walikuwa na hadhi ndogo ya utu (inferior races)hivyo walistahili kutawaliwa au kuuliwa kabisa na kupisha watu waliokamilika kama Wajerumani na watu wa mataifa ya Skandinavia (Waswidi, Wanorwei na Wadenishi). Hitler aliungwa mkono na watawala wa Italia (Mussolini), Hispania (Franco) na Ureno. Kwa sababu vita vilitishia nchi zingine za magharibi kiuchumi, kisiasa na kijamii, zilijiunga pamoja kumpinga Hitler na washirika wake. Japani vile vile iliingia kwenye vita ili kuchukua maeneo ya Kusini mwa Asia ili kujiimarisha kiuchumi. Baadae Amerika (USA) iliingia kwenye vita ili kuzisaidia nchi za Ulaya zilizokuwa zimeelemewa kwa sababu, kwanza, kama Ujerumani ingeshinda ingekuwa mshindani mkubwa wa Marekani, na pili, Marekani iliona fursa ya kuibuka taifa lenye nguvu zaidi duniani baada ya Ulaya kuchakazwa na vita.

Nchi za Kiafrika zilishiriki katika vita zote mbili kwa kuwa zilikuwa ni makoloni ya nchi za Ulaya zilizokuwa zinapinaga. Hivyo zilipigana hata kwenye makolon na washindi wakachukuwa makoloni ya aliyeshindwa.
 
Back
Top Bottom