Msaada: Uvimbe wa wanawake kwenye kizazi

Dr Kaisi hapractice siku hizi, alipatata stroke, anafundisha tu.

Kupata stroke ni rahisi kutokana na kuchungulia chungulia nyeti za mama zetu. Bahati yake angepata kichaa kabisa.:wink2:

Hakika watu kama wewe mnapaswa kuombewa. Yaani watu wanajadili suala nyeti halafu wewe unatukana kiasi hicho? Unafikiri dr. anapenda kuchungulia hivyo vitu? si ni katika harakati za kugundua na kuwaponya magonjwa yao?
Nadhani mods mmechoka siku hizi!
 
Hi Jamani, mambo vipi? Shost wangu kaambiwa anao uvimbe kwenye kizazi, ametumia dawa, hakuna majibu mazuri. Ameambiwa yalazimu operesheni. Ila kuna tetesi kwamba akifanyiwa operesheni tu hatapata mtoto tena! kuna ukweli katika hilo? Je, wapi pazuri au daktari gani mzuri kwa operesheni za namana hiyo? Naomba kutoa hoja!!

Mimi sio doctor, ila naona haina ukweli kuwa hataweza kubeba mimba,labda kama atatolewa kizazi. Ila kama ni operation ya kutoa uvimbe tu atapata mtoto baada ya operation. Kwa mfano uvimbe-ambao ni fibroids huwa zinatokea kwenye kizazi ni lazima afanyiwe operation ndio ata abebe mimba, kwa sababu asipotolewa na akabeba mimba inaweza kutoka au wakati wa kujifungua atapata taabu sana. La muhimu ni kumuona daktari na pia aende haraka akachekiwe saratani ya shingo ya uzazi, wanafanya bure pale ocean road, inatibika ukiwahi. Mtie nguvu asipanic atapona.
 
Hi Jamani, mambo vipi? Shost wangu kaambiwa anao uvimbe kwenye kizazi, ametumia dawa, hakuna majibu mazuri. Ameambiwa yalazimu operesheni. Ila kuna tetesi kwamba akifanyiwa operesheni tu hatapata mtoto tena! kuna ukweli katika hilo? Je, wapi pazuri au daktari gani mzuri kwa operesheni za namana hiyo? Naomba kutoa hoja!!

pole sana dawa ipo wala si lazima ufanyiwe oparation sitairusha hewani nitakuelekeza ukitaka nitumie PM na namba yako ya cm
 
pole sana ndug nina jamaa yangu naye alikuwa na matatizo hayo alikaa hosp miezi 6 bila mafanikio yoyote mwisho wakamfanyia operation na kutolewa kizazi
 
pole sana ndug nina jamaa yangu naye alikuwa na matatizo hayo alikaa hosp miezi 6 bila mafanikio yoyote mwisho wakamfanyia operation na kutolewa kizazi

Mhhh mkuu mbona pressure naona inazidi??ina maana hiyo kitu inatibika kwa 50/50??
 
Ajaribu pia kwa Dr. Byabato wa natural therapy pale Sinza kwa Remi, nina dada yangu alitakiwa kufanyiwa operation ya Fibroids pale Agakhan, amekuwa akiipospond operation hiyo kwa muda wa miaka mitatu sasa -si kwamba hakuwa akiumwa no yeye ni mwoga kila akiingizwa theater anazimia kwa woga anarudishwa. Last moth hali ikazidi kuwa mbaya akaandikiwa operation.......siku ambayo alitakiwa kureport Agakhan for Operation ya kesho yake asubuhi; alikwenda kwa Dr. Byabato akapimwa na kugundulika kuwa HAKUWA NA FIBROID!!! ilikuwa ni Romatism ya misuli ya Uzazi. Akapewa dawa za wiki mbili---- Amekwenda kucheck Agakhani ule uvimbe umepungua from 16cc to 4 cc na bado hajamaliza dozi.
 
Dada angu anajihisi analo tatizo la kuota nyama kwenye kizazi au uvimbe au fibrous, je dalili zake ni nini? Na husababishwa na nini? Kuna dawa tofauti na operation?
 
Jamani naomba msaada kwa anayejua,mimi nina tatizo la uvimbe kwenye kizazi nilijua hivyo baada ya kuwa nasikia maumivu kuanzia ninapoanza period mpaka namaliza nikaamua kwenda hospital ndio wakaniambia nina uvimbe ,niliandikiwa dawa nikamaliza lakini nikaendelea kusikia maumivu,nikaamua kutumia dawa za kichina hali ikawa ileile,nikapima tena hospitali nyingine bado uvimbe ulikuwepo nikaandikiwa dawa nyingine tena nikazimaliza lakini wapi nikarudi tena kupima wakasema hakuna uvimbe cha ajabu bado nasikia maumivu yani nikianza period mpaka namaliza na baada ya kumaliza kila nikienda kujisaidia haja ndogo nakuwa nasikia maumivu sana na yanaendelea kwa siku nzima mpaka nitumie dawa za maumivu na huwa inakuwa hivyo kwa week mbili tokea nianze period ,nimekuwa mtu wa dicloper sababu ndio pekee zinazonisaidia anayejua dawa plz naomba anisaidie
 
Naomba uende hospitali mapema sana ndugu. Hizo Diclopa hazitatui tatizo kabisa.
Nenda Masana hospital mbezi pale. Wakautoe huo uvimbe.
Mara nyingine ukichelewa sana huwa una develop kuwa cancer ya kizazi. Mungu aepushie mbali, ila uwahi wakautoe.
Hizo dawa za kichina haziyayushi huo uvimbe, ni biashara tu.
Ugua pole.
 
Nina dawa ya asili inatibu uvimbe ktk kizazi,dawa ni nzuri sana kwa mda wa mwezi mmoja tu utakuwa umepona kabisa,hutasikia maumivu wala matatzo ktk kizazi.pia ninachokushauli fanya hima utumie dawa ili upone mara nyingi matatzo ktk kizazi huleta utasa,pia kama kunauvimbe nakushauli utumie dawa za asili maana kwenye hospital watakufanyia upasuaji na watakutoa kizazi.kama utaitaji dawa zipo na utapona kabisa.kwa mengizaidi nitafute kwa.0759217720
 
Nina dawa ya
asili inatibu uvimbe ktk kizazi,dawa ni nzuri sana kwa mda wa mwezi
mmoja tu utakuwa umepona kabisa,hutasikia maumivu wala matatzo ktk
kizazi.pia ninachokushauli fanya hima utumie dawa ili upone mara nyingi
matatzo ktk kizazi huleta utasa,pia kama kunauvimbe nakushauli utumie
dawa za asili maana kwenye hospital watakufanyia upasuaji na watakutoa
kizazi.kama utaitaji dawa zipo na utapona kabisa.kwa mengizaidi nitafute
kwa.0759217720

Nimekuona mahali pengi sana ukitangaza dawa zako huku ukisisitiza kwamba zinaponya kweli,hebu naomba ututhibitishie kwamba hizo dawa hazina madhara na zinafaa kwa matumizi ya binadamu na zimethibitishwa na TFDA kwa kuambatanisha cheti kutoka hiyo mamlaka ya chakula na dawa,usije kutuua bure.
 
Jamani naomba msaada kwa anayejua,mimi nina tatizo la uvimbe kwenye kizazi nilijua hivyo baada ya kuwa nasikia maumivu kuanzia ninapoanza period mpaka namaliza nikaamua kwenda hospital ndio wakaniambia nina uvimbe ,niliandikiwa dawa nikamaliza lakini nikaendelea kusikia maumivu,nikaamua kutumia dawa za kichina hali ikawa ileile,nikapima tena hospitali nyingine bado uvimbe ulikuwepo nikaandikiwa dawa nyingine tena nikazimaliza lakini wapi nikarudi tena kupima wakasema hakuna uvimbe cha ajabu bado nasikia maumivu yani nikianza period mpaka namaliza na baada ya kumaliza kila nikienda kujisaidia haja ndogo nakuwa nasikia maumivu sana na yanaendelea kwa siku nzima mpaka nitumie dawa za maumivu na huwa inakuwa hivyo kwa week mbili tokea nianze period ,nimekuwa mtu wa dicloper sababu ndio pekee zinazonisaidia anayejua dawa plz naomba anisaidie
Pole sana kwa hayo matatizo yako mimi ninayo dawa ya Kutibu Uvimbe kwenye kizazi ninaiuza ukihitaji nitafute kwa Email yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com
 
Uvimbe wa kizazi unaweza kuondolewa kwa operesheni. Utachezea fedha tu hapo na hautatoka. Onana na dr bingwa wa wanawake akupe ushauri unaoeleweka. Pm kama unataka maelekezo ya madaktari wa wanawake.
 
Uvimbe wa kizazi unaweza kuondolewa kwa operesheni. Utachezea fedha tu hapo na hautatoka. Onana na dr bingwa wa wanawake akupe ushauri unaoeleweka. Pm kama unataka maelekezo ya madaktari wa wanawake.

asante leo nimemtembelea doctor wa wanawaek huku arusha nikamwelezea kila kitu akaniambia kuwa inaweza kuwa ni appendex nimepimwa mkojo kisha nikapatiwa dawa nimeambiwa nirudi next week
 
Back
Top Bottom