Msaada/Ushauri wana JF

Jeff

JF-Expert Member
Sep 26, 2009
1,293
199
Naamin humu JF ndio kila ki2,wapendwa naomben ushauri kuhusu hili,wiki kadhaa zilizopita niliapply nafasi ya kazi Nairobi,ambayo tangazo lake nililiona humu JF,walinitumia email ya kwanza kunitaarifu kuwa wameipata application yang na wamereview imepita kwenye hatua ya kwanza hivyo wanaendelea na process,wiki hii wakanitumia tena email wanasema wameconfirm kunipa kaz hivyo na wakanipa terms and conditions za kampun na wakaniomba niaccept initial offer,kinachonishangaza ni kwamba hawajaniita kwenye usahili/interview na kwenye barua yao wanasema ksh 1000 kwa ajili ya registration ya course fupi ya international certificate of nutritionist,sasa nashindwa kuamini,au ni shemeji zetu wale wa nigeria? Hiv unaweza kupata kaz bila interview? Hasa professinal jobs? Nishaurin wandugu
 
sidhani kama inawezekana kupata kazi bila walau phone interview. lakini hiyo ya registration fee ni utapeli kabisaa! haina tofauti na zile za ku-apply for scholarship na kutakiwa kulipa $ 45 for application processes!waambie hiyo kshs 1000 wakate kwenye ur 1st salary kama hawatajali
 
ndio unaweza kupata kazi bila kuitwa kwenye usaili. Kuhusu wewe kutoa ksh 1000 ndipo wac wac wangu ulipo. Fuata ushauri wa kuwaambia wakate kiasi hicho cha pesa kwenye mshahara wako.
 
Naomba uhamini kuwa huo ni wizi mkubwa, usitoe kitu kabisa, hao ni shemeji zetu 100%
 
ndio unaweza kupata kazi bila kuitwa kwenye usaili. Kuhusu wewe kutoa ksh 1000 ndipo wac wac wangu ulipo. Fuata ushauri wa kuwaambia wakate kiasi hicho cha pesa kwenye mshahara wako.

sawa jaluo,nitafanya hvyo,cha ajabu hawajawah hata kunipigia cm,wanatuma email tu
 
shemeji tizama na pia kuwa makini mdau wangu maana kama hujui kusoma hata picture unashindwa kuelewa,plz tambua cku hz watu wamekuwa wakijitajirisha sana kutokana na utapeli wa kuwapatia vijana kazi!plz plz plz shemeji be careful!
 
Interview zingine hufanyika kupitia simu na unaweza usijijue kuwa unakuwa interviewed.
Hiyo lakini inategemea na kazi husika. Hapo kwenye swala la pesa ndio balaa. Waulize kama utakuwa unasoma huku unafanya kazi na hvyo mshahara wako kuwa unaingia kama kawa au?
 
pia angalia sana usije kutoa details zako zozote za bank

eti wamenipa namba zao za cm,ili nitume hiyo pesa kwa M-pesa,na namba zinaonekana ni za hapa bongo sio za kenya,majambaz yapo kila kona! Duuuh,nataka niwapigie niwahoj
 
Usitume pesa rafiki yangu, utatapeliwa bure.. Hiyo ni kampuni gani itakuppatia kazi bila interview kisha ikuitishe pesa za training.. chunga aise. weka hapa email adress yao tuishugulikie.
 
sorry ma friend, naomba ufahamu kua ktk ulimwengu huu kuna interview tunazozifahamu(zilizozoeleka) na pia kuna addition interview ambazo ni internally organized so usiogope kupata kazi bila interview, make inawezekana iyo ni moja wapo ya interview yao ya kukupima wewe imani yako.......!!!!, kwa iyo naomba uwaamini na ujiamini, apo utapata unachokitaka...........!!!!!!!!, uo ndo ushauri wangu, thanks na usikate tamaaaaa
 
Back
Top Bottom