Msaada; Tshs 85Mil, inajenga Ghorofa??

Mkuu hutamaliza hilo jumba! Kama unapo mahala pa kuishi nakushauri we nunua viwanja kwenye prime areas, fanya shughuli nyingine , after three to four years natangaza kuuza! utapata mara 3 ya thamani uliyouzia!
 
Kitakachoamua kama inatosha au haitoshi ni uimara wa msingi, zege la kati na aina ya paa.
Kiujumla jumla tu jibu rahisi ni kwamba mil 85 inatosha, lakini kuwa specific zaidi ni lazima tujue surface area ya ramani yako na ubora utakaochagua.

Ninaposema inatosha nabreak down hivi:
Msingi mil 20
Zege la kati mil 20
Matofali mil 15
Mchanga, Kokoto, Mawe, maji mil 5
Mazagazaga mengine (Ufundi, nondo, mbao, mirunda, misumali) mil 20
Dharura mil 5
Hii nyumba itakuwa haijaezekwa! Kwa hesabu hii haitoshi na kimsingi huo ni mchanganuo lakini uhalisia wake ujenzi wa nanma hiyo ni ghali sana yahitaji moyo na yahitaji chanzo cha uhakika. Mi naona kwanza uwepo wa 85ml cash peke yake ni tatizo kwa sababu mjengo huo utajengwa siyo chini ya miezi 3. Kwa muda huo tu fedha hizo kama jamaa hana chanzo kingine na anaweza kuitumia kwenye dharura na mambo mengine nje ya mipango. Nashauri umtafute mtaalam mshauri atakupa pa kuanzia.
 
Kaka wacha tu nijenge ya kawaida,
Maana nimegundua naweza kujenga ghorofa then hata ukuta wa fensi nao ukawa utata!!
 
Waliozungumzia wachangiaji wengine ni kweli. Mimi najenga Ghorofa moja tuu, 4 bedroom zote ni self contained, two sebule, msikiti/study, Dining Room and Kitchen ni square meter 360. Kusema kweli inategemea na fundi lakini bei sio rahisi hata kidogo.

Msingi material tuu bila ufundi ni Milioni 30 ukiweka 6M ya ufindi unafika kwenye 36M. Kunyanyua kuta sio ghari hata kidogo itakula kama M20, gharama ni kwenye slab ya juu ambapo inakula kama M 30 nyingine. Unaamka kwa M20 nyingine hapo umeshafika 100M. Then unafunika kwa 30M.

Hapo hujaweka dirisha wala kupiga plasta... Lakini baada ya hapo kichwa kinapungua kuuma.

Kujenga ghorofa yataka moyo, lakini walio jenga walijengaje hilo ndio nilokuwa najiuliza. komaa unajenga kaka
 
wadau naomba kusaidiwa mawazo, nina Tshs 100,000,000/= nahitaji kujenga nyumba yenye features zifuatazo: one storey)nahitaji kujua wale wazoefu kahela kangu katatosha?mbali na hayo waweza kunishauri vinginevyo kwenye huu ujenzi kwa budget yangu ya 100,000,000/=
1Ground floorSize in metres
Sitting Room4 * 4
Dinning 3 * 3
Kitchen4 * 4
Laundry2 * 2
Public toilets & bath2.5 * 2
Ground room3.5 * 4
Ironing room2 * 1.5
Car park - two cars connected with house inaweza kuwa pembeni ya nyumba tu
Balcony barazani
Balcony jikoni
2First Floor
Master bed room4.5 * 4
Walk-in Closet3.5 * 2.5
Toilet2.5 * 2.5
Room 13 * 3.5
Room 23 * 3.5
Toilet & Bath2.5 * 2
Study room3.5 * 3
Living room In the midspace remaining
 
Inategemea unataka kujenga wapi na iwapo tayari una kiwanja. Kwa sehemu nyingi za Dar-es-Salaam kiwanja kinaweza kukwapua hela zote hizo usibake na kitu. Na vile vile iwapo kiwanja chako kiko kwenye kilima, fedha zote hizo zinaweza kutumika kujenga msingi tu. Hata hivyo ukiwa na kiwanja kizuri halafu ukapata msimamizi mzuri, fedha hizo unaweza kuzitumia vizuri zikamaliza sehemu kubwa ya jengo lako ingawa zitakuwa hazitoshi.
 
Inategemea na eneo, usimamizi mathubuti, mafundi bora. Ubora wa material kwa mfano roofing materials zina tofautiana sana bei na ubora. Ukipata vyote hivyo na kama ujenzi ni dar, eneo lisilokuwa na complication hiyo hela inatosha kwa kiasi kikubwa.
 
Inategemea unataka kujenga wapi na iwapo tayari una kiwanja. Kwa sehemu nyingi za Dar-es-Salaam kiwanja kinaweza kukwapua hela zote hizo usibake na kitu. Na vile vile iwapo kiwanja chako kiko kwenye kilima, fedha zote hizo zinaweza kutumika kujenga msingi tu. Hata hivyo ukiwa na kiwanja kizuri halafu ukapata msimamizi mzuri, fedha hizo unaweza kuzitumia vizuri zikamaliza sehemu kubwa ya jengo lako ingawa zitakuwa hazitoshi.

kiwanja kipo tayari na kipo dsm
 
Kiwanja unacho?........je ni saizi gani?.....kama una kiwanja kikubwa nakushauri ujenge ya chini kwa hela hiyo....mimi juzi nimepiga msingi wa orofa kama hiyo umekula Tshs 26,500,000

Unit price Amount Cost
Tofali 1,800.00 2950 5,310,000.00
Kokoto 700,000.00 8 5,600,000.00
Mchanga 250,000.00 10 2,500,000.00
Cement 14,500.00 200 2,900,000.00
Nondo 17,800.00 65 1,157,000.00
Mbao 8,500.00 60 510,000.00
Mawe 500,000.00 4 2,000,000.00
Lanscaping 1,000,000.00 1 1,000,000.00
Trenching/setting 1,500,000.00 1 1,500,000.00
Hire of concrete mixer and tramping rammer 400,000.00 1 400,000.00
Nails/Binding wire etc 200,000.00 1 200,000.00
Labour charge 3,461,550.00
Total 26,538,550.00
 
kiwanja kipo tayari na kipo dsm

Uwezekano wa kufikia lengo kwa kiasi kikubwa upo!!

BUT

Fundi na Msimamizi ni muhimu kuliko hata hizo fedha zako! Hii yenyewe inaweza kufanya tofauti ya kati ya 20% hadi 25% ya thamani!

Msimamizi ni muhimu sana mkuu!!!!
 
Kiwanja unacho?........je ni saizi gani?.....kama una kiwanja kikubwa nakushauri ujenge ya chini kwa hela hiyo....mimi juzi nimepiga msingi wa orofa kama hiyo umekula Tshs 26,500,000

Unit priceAmount Cost
Tofali 1,800.00 2950 5,310,000.00
Kokoto 700,000.00 8 5,600,000.00
Mchanga 250,000.00 10 2,500,000.00
Cement 14,500.00 200 2,900,000.00
Nondo 17,800.00 65 1,157,000.00
Mbao 8,500.00
60 510,000.00
Mawe 500,000.00 4
2,000,000.00
Lanscaping 1,000,000.00 1 1,000,000.00
Trenching/setting 1,500,000.00 1 1,500,000.00
Hire of concrete mixer and tramping rammer 400,000.00 1 400,000.00
Nails/Binding wire etc 200,000.00 1 200,000.00
Labour charge 3,461,550.00
Total 26,538,550.00

This is the most accurate calculation kasoro kwenye tofali nadhani wamekula kama 400 yako, labda umetumia zile zenye concrete chipping. Nondo zako ni mm 12 hapo umasave pesa mmno, lakini sijui kama it worth or not inategemea na size ya nyumba. Ukubwa wa nyumba yako ni kama wangu, lakini cost kwangu estimate ni Million 36 include ufundi.
 
Tofani ni za chipping toka kwa KOMBE
 
Back
Top Bottom