Msaada tafadhali

Rubi

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
1,615
326
Naomba msaada wa jinsi ya kutibu miguu inayopasuka wengine wanaita machacha, wengine wanaita makegete. Please
 
Pole sana. Niliwahi kuwa na tatizo kama hilo nilipokuwa mtoto. Jitahidi kuyasugua(safisha miguu kwa dodoki gumu au kipande cha jiwe ukiwa umepaka sababu) safisha hivi angalau mara mbili kwa siku. Pendelea kuvaa raba na soksi ili miguu ipate joto. Jitahidi kufanya hivi kwa muda mrefu na dumisha usafi wa miguu. Na kama upo mikoa ya baridi kama mbeya na iringa jitahidi sana kutovaa viatu vya wazi.

Hope itakusaidia. Guidance!
 
ukweli mtupu
 
Ras asante sana kwa ushauri wako ila kwa upande wa usafi wa miguu ni kitu ambacho nakizingatia sana. na binafsi sikuwahi kuwa na tatizo hilo ila naona imeanza kunitoklea kwa sasa pengine ni kwa sababu zifuatazo sehemu ninayoishi wakati huu wa kiangazi kuna baridi sana na vumbi jingi na jua kali na pia ni mpenzi sana wa kuvaa viatu vya wazi ila sikuwahi kuwa na tatizo hilo kabla ni sasa tu ndo naliona.

Nakumbuka wakati fulani niliwahi kuishi Njombe kule nako kuna baridi ila sikuwahi kupasuka miguu ila watu waliokuwa wapasuka miguu hayo machacha walikuwa wapenda kupaka mafuta yale yanayotokana na zile mbegu za nyonyo sijui jina lingine, yalikuwa yanawasaidia ila huku niliko hata dalili ya hizo mbegu sijawahi kuziona.

Nitazingatia kuvaa viatu vya kufunika mara nyingi iwezekanavyo.
 
Bila shaka uko Dodoma. Huko ni balaa, miguu huwa inapasuka hata ngozi pia.

Pendelea kupaka mafuta mazito kama ya nivea na vaseline.

Kuna siku niliona mafuta dukani dawa ya hayo magaga, inaitwa something like "skin doctor" na picha ya box lake ni ya mguu wenye hayo magaga. Kwa kuona box inaonekana ni dawa nzuri. jaribu kuitafuta.

Pia kuna dawa ya tube inaitwa "fung nil" nayo box lake lina picha ya hayo makenye aka magaga.
 
Ras asante sana kwa ushauri wako ila kwa upande wa usafi wa miguu ni kitu ambacho nakizingatia sana. na binafsi sikuwahi kuwa na tatizo hilo ila naona imeanza kunitoklea kwa sasa pengine ni kwa sababu zifuatazo sehemu ninayoishi wakati huu wa kiangazi kuna baridi sana na vumbi jingi na jua kali na pia ni mpenzi sana wa kuvaa viatu vya wazi ila sikuwahi kuwa na tatizo hilo kabla ni sasa tu ndo naliona.

Nakumbuka wakati fulani niliwahi kuishi Njombe kule nako kuna baridi ila sikuwahi kupasuka miguu ila watu waliokuwa wapasuka miguu hayo machacha walikuwa wapenda kupaka mafuta yale yanayotokana na zile mbegu za nyonyo sijui jina lingine, yalikuwa yanawasaidia ila huku niliko hata dalili ya hizo mbegu sijawahi kuziona.

Nitazingatia kuvaa viatu vya kufunika mara nyingi iwezekanavyo.

Karibu. Nadhani chanzo hapa ni hayo mazingira uliyoyasema nimeyahighlight hapo juu. Amini nakuambia mimi mwenyewe nilikuwa naishi Mafinga (Iringa)kipindi hicho miaka ya 1986. Nilisumbuliwa sana na hilo tatizo vile nilikuwa sivai raba na kuna baridi na vumbi. Lakini baada ya kugundua hiyo siri sijawahi tena pata tatizo hilo kwani baadae niliishi mikoa ya baridi kama Mbeya na Arusha bila tatizo. Si lazima uzae raba ila pendelea kuvaa kiatu kinachofunika mguu mzima. Natumai utapona tu. Wana jamii wengine watakupa ushauri zaidi. Pole sana. Guidance.
 
Jaribu kufanya pedicure (unaweza kuloweka tu miguu nyumbani kwa muda mfupi kisha kusugua) mara kwa mara. Angalia pia chanzo. kama una tabia ya kuvaa open shoes au carpet ya gari ni ya nyoya unakuwa unakanyaga vumbi. angalia hizo possibillities.otherwise vaa viatu vya kufunika mara nyingi na ujitahidi kupaka mafuta.Kila la kheri
 
Nafikiri mpaka kuleta swala hili kwenye JF utakuwa umeshajitahidi na kusumbuka katika kujaribu ondoa hili tatizo. nakushauri uende kwa Daktari wa magonjwa ya ngozi. Kuna Shangazi yangu ( marehemu kwa hivi sasa) alikuwa na tatizo kama hilo lakini lilikuwa zaidi ya la kawaida . Kwake ilkuwa miguu inapasuka mpaka kutoa damu na kusikia maumivu machungu mno. Baada ya kujitahidi sana alikuja kuonana na Daktari huku Dar (baada ya kushindikana wakati yeye akiwa Morogoro) na baada ya kuja kwa vipindi kadhaa alipata nafuu na kupona kabisa. Bahati mbaya sijui Daktari aliyekuwa anakuja kumuona na ni muda mrefu umepita lakini narudia muone Daktari wa magonjwa ya ngozo au ikibidi hata nenda Ocean Road Hospital ukaone madaktari wa pale kama matatizo ni makubwa kuliko yale ya kawaida. "the ealier the better".
 
Hili tatizo limeanianza kiasi mwezi sasa naona tu naanza kupasuka miiguu hasa kipindi hiki baada tu ya kiangazi kuanza. before sikuwa nalo ila pia huwa nina aleji sana na vumbi kitu ambacho kimenifanya niwe makini sana na usafi wa mazingira ninayoishi pamoja na mwili wangu kujitajidi kuondoa vumbi vumbi kila iwezekanavyo. Hivyo nitazingatia ushauri wenu na bia nimeonelea nibadili stail kila siku najitahidi kuisugua miguu na kipande laini cha jiwe na kabla ya kulala nahakikisha nasafisha miguu vizuri na kuloweka kwenye maji ya chunvi kwa muda kidogo najaribu pia kuipaka ndimu au limao kabla ya kulala. nitafanya hivi kwa mwezi nione kama kutakuwa na matokeo mazuri.
 
Wakuu asanteni nyote kwa ushauri wenu mzuri. nitauzingatia ukizingatia miguu ndio reception ya pili baada ya uso hasa kwa akina sie inabidi ipendeze. mbarikiwe naamini JF hakuna kinachoshindikana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom