Plato
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 420
- 94
Ndugu,poleni na majukumu.mimi ni mwanafunzi wa UDSM-DUCE.niko mwaka wa tatu ambao ni wa mwisho.nakusudia kumaliza july.
Nasoma Public Administration na ualimu, somo la historia. Ni muhitaji na hulipiwa na bodi ya mikopo. Kuna tatizo kubwa limetokea, sikusaini fomu muhula uliopita na bodi waliasume sipo chuo, hivyo kuniondoa kwenye orodha ya mkopo. Nimefatilia suala hili,lakini uamuzi wa bodi umekuwa niombe upya kwa ajili ya mwaka kesho.
Nakabiliwa na hatari ya kutoona matokeo ya muhula uliopita na kukosa udahili muhula huu.ninapaswa kulipa ada ya mwaka wa mwisho ni nyingi sana. MILIONI MOJA.
Ninatafuta msaada wa mkopo wa fedha hizo. Nikimaliza chuo July naweza kulipa, ama kufanya kazi ili kulipa deni.kwa wenye shule naweza kufanya kazi kulipa deni.naweza kufundisha vizuri historia, GS, na DIVINITY. Nimesoma seminari na kusoma falsafa na teolojia, na nimewahi kufundisha masomo hayo.
Chaguo jingine kwangu ni kuandika barua ya kuahirisha mwaka kurudi nyumbani na kuomba tena mkopo nikipata nirejee kumalizia masomo. Baada ya kukwama kabisa, kabla ya kuandika barua ya kuahirisha mwaka nimeona niwaeleze kuomba ushauri na msaada.
Nitashukuru kwa kila jambo na Mungu atuweke salama, asanteni