Msaada tafadhali

Lunanilo

JF-Expert Member
Feb 15, 2008
370
13
Heshima yenu wanajamvi.
Naomba tafadhali mtu anayejua maneno ya wimbo wa
"Sisi Tunataka Kuwasha Mwenge"
Sijui ulitungwa lini lakini ni wimbo unaojulikana sana. Nadhani ulitungwa na kikosi cha muziki cha Jeshi Pengine miaka ya mwisho ya sitini au mwanzo wa sabini.
Tulikuwa tunauimba sana JKT.
 
Sisi tumekwisha kuwasha mwenge, tumekwisha kuwasha mwenge
Na kuuweka juu ya mlima, mlima Kilimanjaro x2
Kuwasha mwenge kuwasha mwenge, na kuuweka Kilimanjaro x2

Umulike hata nje ya mipaka yetu ulete tumaini
Pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali ambapo pana chuki,
na heshima ambapo pamejaa dharau.
 
Asante sana Mheshimiwa Eeka Mangi.
Tunaanza kujikumbusha nyimbo za kizalendo huwezi jua siku moja tutahitaji kuziimba katika viwanja vya mnazi mmoja. LOL

Hivi hakuna sehemu inayosema

"Ili wote wauone unavyowaka......?"
 
Kuna ule mwingine:-
TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE

1. Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuwaza wewe, niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

2. Tanzania Tanzania, ninapokwenda safari,
Kutazama maajabu, biashara nayo makazi,
Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu hakika
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

3. Tanzania Tanzania, watu wengi wanakusifu,
Siasa yako na desturi, ilituletea uhuru
Hatuwezi kusahau sisi, mambo mema ya kwetu hakika
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.
 
Halafu pia kuna huu:-
TAZAMA RAMANI

1. Tazama ramani utaona nchi nzuri, yenye mito na mabonde mengi ya nafaka
Nasema kwa kinywa halafu kwa kusitiri, nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania
Majira yetu haya yangekuwaje sasa? Utumwa wa nchi Nyerere ameukomesha.

2. Chemchem ya furaha ama nipe tumaini, kila mara kwako niwe nikiburudika.
Nakupenda hasa hata nikakufasiri, nitalalamika kukuacha Tanzania.
Majira yetu haya yangekuwaje sasa? Utumwa wa nchi Nyerere ameukomesha.

3. Nchi yenye azimio lenye tumaini, ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania
Ninakuthamini hadharani na moyoni, unilinde nami nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya yangekuwaje sasa? Utumwa wa nchi Nyerere ameukomesha.

4. Tazama ramani utaona nchi nzuri...... (endelea kama ubeti wa kwanza)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom