BabaDesi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2007
- 6,032
- 3,944
Shalom. Wanajamvi nawaombeni msaada tafadhali. Natumia Modem ya Voda E220. Nina matatizo mawili makubwa kuhusu kwayo. 1. kuna wakati niliacha kuitumia kwa kama miezi miwili hivi na nilipoanza kuitumia siwezi kuangalia kuingiza bundle la intenet wala kuangalia salio. Hata kuangalia tu salio la kawaida nikienda kwenye ile sehemu ya kubonyeza ili kuongeza ama kujua salio inajiiivuta na mwisho inaniambia 'time out'! Sasa hivi ili kuingiza bundle la internet kwenye modem hii inabidi nifanye hivyo kwa kutuma kutoka kwenye namba nyingine ya voda. hapa nafanyaje wajuzi. 2.Eneo la huku Shamba Makabe ninapoishi Vodacom Internet sio mwao kabisa! Kuna wakati nilikuwa nikiamka usiku wa manane kwa matarajio kuwa itakuwa fast angalau lakini mara nyingi imekuwa slow kuliko hata inavyokuwa mchana! Ninaomba msaada wa kuichakachua Modem yangu E220 ili iweze pia 'kula vichwa' Tigo na Airtel maana uwezo wa kununua Modem zao sasa hivi haupo! Natanguliza shukurani.