Msaada Tafadhali, Hali mbaya-ofisi chungu!

Sokwe Mjanja

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
576
297
Jamani natumaini mko salama kabisa na wale waungwana waliofunga kwa dhati basi rehema za mwenyezi Mungu ziwatangulie na toba zao zisikike. ndugu yenu nina tatizo moja na linakuwa serious kila muda unavyozidi kwenda. Nimeanza kazi mahali sina muda mrefu sana kuna bwana mmoja subordinate kwa level kama 2 chini ananuka sana wakuu, ninashindwa kumwambia na hata wenzake hawamwambii.

Siku hizi ameanzisha mchezo wa kupenda kujifunza kazi sasa muda wote anataka awe pembeni yangu! Ninapata shida hasa, mwanzoni nilidhani alijisahau akajisaidia ndani ya nguo ila naona ni kila siku na hali inazidi kuwa mbaya. Nguo zake kwa nje sio chafu sana ajabu!

Nashindwa kumwambia maana kwanza ni mgeni mimi kisha ni mtu mzima kanizidi umri na mwenye familia yake huko street. Ninahisi nikimwambia atajisikia vibaya sana na atachukia kazi. Anapenda mno kuendesha gari inapotokea kazi ya nje anakimbilia funguo sasa humo ndani ya gari na vioo vimefungwa kwa kuwasha AC ni balaa, mazingira ya kazi ni muhimu kufunga vioo vya gari kila mara, hadi ninahisi nikishuka kwenye gari ninakuwa na mimi nimeambukizwa harufu!

Nifanye nini wakuu?
 
inatakiwa kila ukimuona
unamuuliza hivi..'nasikia harufu hiyo'?
we husikiii chochote?

ataelewa tu
 
Hahahahaha, Pole sana aisee, Hadi mtu mzima uamue kumuanzishia thread hapa JF I can imagine your despair!
Kwa vile hamna ukaribu nadhani itakua sio sawa umwambie mwenyewe. tafuta mtu one level chini yako, au mchunguze uone yuko karibu na nani hapo ofisini na uongee na huyo mtu.

Kama hayuko karibu na mtu basi ongea nae kwa lugha ya kiutu uzima like: Naomba ubadili deodorant unayo tumia sasa hivi maana harufu yake imenikalia vibaya. Since we share the vehicle and sometimes the office space, maybe you should consider something more classic ili wote tusikerane. Ikibisi mpe zawadi ya deodorant.

If it still doesn't work, then you will have to confront him. Mwambie he needs to improve his hygiene if he wants to stay around you. It is that simple. I know it is hard to say, but you have to say it.
Poleeee
 
inatakiwa kila ukimuona
unamuuliza hivi..'nasikia harufu hiyo'?
we husikiii chochote?

ataelewa tu
Kuna mtu unamwambia hivo wala hashtuki.
Anakwambia yeye hasikii, na ukimuuliza sana
anaishia kukuuliza kama sio wewe mwenyewe.
 
DUhhh, pole sana ndugu yangu. Inabidi utafute mtu mzima mwenye hekima aende kumwambia kwa niaba yako, kama huwezi kumwambi. Mie ningetembea na air freshner, halafu nikiwa karibu naye napuliza, angejua tuu mwenyewe kivyake vyake..Duuhhh, shughuli kwelikweli.
 
kuwa mjasiri muite faragha mweleze,anza hivi,ndugu kwa muda ambao nimeanza kazi hapa mpaka leo nimegundua wewe ni mtu mwenye busara sana,mkarimu na mwenye huruma kifupi unaroho nzuri,kutokana na hayo naona ni vema kuku weka wazi jambo moja ambalo watu wote tunaona si la kawaida na naamini hakuna ambaye amejitokeza kukuambi binafs roho wa mungu ananiambia nisikae kimya kwan nahs namkosea mungu,ndugu huwa unatoa harufu sana emu jarbu kumuona daktar,hii harufu si ya kawaida
 
Hahahahaha, hapo si utakua unamchonganisha na wengine walio kutwa kazini? But I like the approach. Just keep God out of it. Hahahahahaha
 
kuwa mjasiri muite faragha mweleze,anza hivi,ndugu kwa muda ambao nimeanza kazi hapa mpaka leo nimegundua wewe ni mtu mwenye busara sana,mkarimu na mwenye huruma kifupi unaroho nzuri,kutokana na hayo naona ni vema kuku weka wazi jambo moja ambalo watu wote tunaona si la kawaida na naamini hakuna ambaye amejitokeza kukuambi binafs roho wa mungu ananiambia nisikae kimya kwan nahs namkosea mungu,ndugu huwa unatoa harufu sana emu jarbu kumuona daktar,hii harufu si ya kawaida

ha ha haaa huyu mungu mnavyomsingizia hadi baasi
Roho ya mungu ikutume?
 
I can't wait to read Nyani Ngabu on this one, nakumbuka
alianzisha moja ya wanawake, but sikumbuki iliishia wapi.
 
Last edited by a moderator:
Mie naamin jinsi ya kutatua tatizo inategemea sana na ni mtu wa aina gani... As in je ni muelewa na aina ya mtu wa kusikiliza to the extent akawa understanding?
 
...chapa karatasi kumueleza hayo na aipate pasi na kujua imetoka kwako.
 
Is this really an HR matter? zaidi naweza kusema ni Health and Safety...

Anaweza kumwambia halafu akaonekana offensive (wakati kikweli aliye offensive ni anayenuka)

Natumaini akilipeleka HR kuna watu wako trained ku deal na mambo kama haya na watamueleza huyu mtu kiutaratibu na kwa authority ya HR bila kuanzisha vurugu.

Kama kuna HR ya kueleweka lakini.
 
HR kama ya kiswahili utajuta
utasikia yule mgeni anasema eti tunanuka...lol
unajenga maadui ghafla...
 
Anaweza kumwambia halafu akaonekana offensive (wakati kikweli aliye offensive ni anayenuka)

Natumaini akilipeleka HR kuna watu wako trained ku deal na mambo kama haya na watamueleza huyu mtu kiutaratibu na kwa authority ya HR bila kuanzisha vurugu.

Kama kuna HR ya kueleweka lakini.
I get your point... good idea nzuri
(tautology intended, kuonesha msisitizo)
 
Back
Top Bottom