Msaada soko la matango na mahindi mabichi

Nimepata wazo hapa wakuu!

Tutenngeneze thread imwe kama Dira ama database as ana attachment.......

Humo tuweke

Nini kinastawi wapi? kwa gharama gani ; chanagamoto gani; msimu gani; kwa msaada wa karibu nani atahusika..................tutapiga mbele kwa kila kitu the same thing tuiweke kwenye mifugo na hata madini ama biashara; ni wazo tu limenijia baada ya kukuta aina hii ya maswali ikijirudia lakini kila siku kumekuwa vitu vipya vya kujifunza kwayo..............mtaniambia namana ya kuliboresha wazo hili lakini naamini litatusaidia.
 
Mkuu Malila nimekukubali! Yaani sehemu zote nzuri kwa kilimo kwanza unazifahamu?! Wewe ni kitu ingine! Lakini mkuu mbona umekomalia sana Alizeti inalipa nini?

Nimemshauri kuhusu alizeti kwa sababu mbili. Moja ni kwa sababu maeneo aliyoyataja alizeti inafanya vizuri na soko lipo kubwa, pili alizeti ukivuna unaweza kuitunza mpaka upate soko zuri. Sababu ndogo iliyo nyuma ya pazia ni kwamba unaweza kufanya usindikaji mdogo mdogo nyumbani kwako. Kwa sisi tunaotaka kuingia ktk food processing b/ness ni vizuri kujua haya mambo. Soko la alizeti pia liko juu.
 
Nimepata wazo hapa wakuu!

Tutenngeneze thread imwe kama Dira ama database as ana attachment.......

Humo tuweke

Nini kinastawi wapi? kwa gharama gani ; chanagamoto gani; msimu gani; kwa msaada wa karibu nani atahusika..................tutapiga mbele kwa kila kitu the same thing tuiweke kwenye mifugo na hata madini ama biashara; ni wazo tu limenijia baada ya kukuta aina hii ya maswali ikijirudia lakini kila siku kumekuwa vitu vipya vya kujifunza kwayo..............mtaniambia namana ya kuliboresha wazo hili lakini naamini litatusaidia.

Tukifanikiwa kuwa na data base ya mambo haya tutakuwa tumepiga hatua moja mbele. Naamini wengi tutakubaliana kuwa kuna mapungufu sana ktk utafutaji wa habari muhimu. Kupitia humo tunaweza kuonyesha wapi pilipili mtama inamea, wapi nyuki wadogo wapo, wapi mbuzi wanaozaa watoto watatu wanapatikana, wapi mdung`wa unapatikana, kinyonga wa pembe moja anapatikana wapi.
 
Haya tuundeni kamati ya utekelezaji basi aidea ikiwa ya moto

Wewe Malila na kupa cheo cha coordinator kwenye hili!
 
website ya wizara ya kilimo ina ramani inayoonyesha nini kinastawi wapi na wapi kunafaa kupanda nini tunaweza kuanzia hapo kutengeneza data base yetu
 
Habari wana jf.
Nina mpango wa kulima mahindi na matango kwa ajiri ya kuyauza kwenye soko la ndani,
Napenda kujua kama kuna anayejua soko limekaaje?I mean ntafanya biashara au itakula kwangu?nimepata shamba maeneo ya Iringa vijijini na nimepanga kuuzia shambani,jee mahindi mabichi na matango naweza kuuzia shambani kwa bei gani?nimepanga kulima hk 10 za mahindi na 10 za matango!
Naombeni msaada wakuu.

Soko ni la uhakika, kwa ushauri wangu bora kufungua viwanda vidogo vidogo vya uzindikaji wa vyakula hivyo ni rahisi hata kusafirisha porducts nchi za nje kwa biashara kuliko kutafuta soko la produce.
 
Haya tuundeni kamati ya utekelezaji basi aidea ikiwa ya moto

Wewe Malila na kupa cheo cha coordinator kwenye hili!

Hii kitu iko vizuri,
Nimerudisha jukumu hili kwetu sote ili tufanikiwe mapema, tukishapata taarifa nyingi kupitia michango ya humu jamvini basi tutatoa summary ya kazi yetu hiyo kwa kushirikiana.
 
Songea vyote viwili vinakubali, ila wasiwasi upo ktk soko la mahindi mabichi kama mada ya jamaa ilivyo. Mahindi mabichi hayatakiwi kukaa sana yakishafika sokoni,kumbuka kwa mikoani yakishapoteza test yanatupwa. Mikoani watu wanakula vya leo leo.

Ok asante sana kwa wazo lako, ila mimi sikuwa nataka yauzwe yakiwa mabichi nataka ikiwezekana yakauke kabisa na niweke kwenye magunia yawe kwenye sstock je kama nikisema yakaushwe alafu yahifadhiwe na niyapige dawa kabia unaonaje hapo ndugu yangu unadhani itakuwa possible kupata soko la kuuza na kwa sasa hii gunia la mahindi ni kiasi gani??
 
Asante sana mandieta kwa kuanzisha uzi huu na pia shukrani nyingi zimuendee kila aliyeuchangia uzi huu lakini shukrani za pekee zimuendee Mkuu Malila kwa moyo wa uwazi katika kutoa habari, maarifa na chote anachokifahamu. Nami nimekutumia SMS kukuuliza juu ya Matikiti Maji variety ya PETA NEGRA. Natumaini utanijibu!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu asante,

Ngoja niingie chaka, nitafute kwa faida yako na ya wengine. 2014 nitaanza kulima tikiti organic.
 
Mkuu asante,

Ngoja niingie chaka, nitafute kwa faida yako na ya wengine. 2014 nitaanza kulima tikiti organic.

Mkuu shida yetu waswahili hatujui thamani ya organic tungekuwa tunajua hii kitu ni dili sana nje wenzetu wanathamini sana organic products kuna hadi nguo za organic zinazotengenezwa na pamba iliyolimwa organically
 
Kwa mtazamo wangu na uzoefu mdogo katika Food Processing and International Trade suala la certifications (organic, HACCP. Utz, FSMS, BRC, Traceability, mention all others) kwa Africa is more of the Non-Tarrif Barriers (NTBs) to trade kuliko inavyofikiriwa kuwa ndiyo njia ya kukufikisha kwa urahisi kwenye masoko yenye tija. Kwa Mtanzania hata kutimiza matakwa ya TFDA ukapata nembo ya ubora ya TBS haina lolote la zaida (incentive) la kukutofautisha na yule asiyetimiza bidhaa zenu zinapowekwa mbele ya mlaji. Huwa napingana sana na mtazamo wa wengi kufikiria Export market yenye changamoto lukuki wakati local market iko under supply.

Nyongeza ya yote, karibu vitu vyote vinavyolimwa nchini ni conventional organic. Suala la inspection, verification and certification ni nyongeza ya ghalama ambazo ndizo huzaa hizo NTBs. Hizo certifications zote ni mali ya hao hao wasiojua Kilimo Hai (organic farming). Ndiyo wanakuwekea mifumo, wanakukagua, wanakuthibitisha na kukugonga ghalama. Wazungu, katika suala la kilimo na hata matumizi wanajua synthesized products na siyo organic products.
 
Kwa Idodi ukilima matango atanunua nani? Wahehe hawali matango, Hotel zenyewe ziko mbili pale mjini. Idodi lima mahindi,alizeti na mpunga. Matango lima huku kwetu Pwani. Tatizo la Kisaki ni usafirishaji wa haraka wa mahindi yako mpaka kwa mlaji wako ( Morogoro au Dar). Kama si kumwagilia, ni kwamba utakumbana na mafuriko toka Iringa/Dom na Tanga na Moro yenyewe.Kama una uhakika na usafirishaji basi Kisaki sio mbaya.

Kumbuka, jamii yetu ya Kitanzania sio walaji wa Matunda hasa huko vijijini. Je umewahi kuwaona watu hapo Kisaki wanakula Matango kwa kununua? Wanaweza kuwa wanakula sio kwa kuyanunua,bali kwa kuchuma shambani kwao.
Kisaki ni ngumu kwa usafili kwa mazao yanayohitaji kufika haraka sokoni....kisaki lima Ufuta na alizeti
 
Wana jf mimi nipo mkoa wa kilimanjaro wilaya ya same nahitaji kulima matango kama heka 1 je soko lake linaweza patikana wapi?na ni mwez gani nikitoka bei inakua nzuri?
 
Back
Top Bottom