Msaada: Sheria ya ndoa inasemaje juu ya mke akitaka kumuua mumewe?

americana

Member
Sep 4, 2013
84
37
Ndugu zangu, hivi ikibainika kua mwanamke anapanga njama za kumuua mumewe na ikathibitishwa kua ni ili arithi mali na ushahidi ukawa ni wa sms ambazo anawasiliana na ndugu zake kutaka kufanikisha azma yao...sheria inasemaje, je ndoa hiyo ikivunjika mwanamke atakua na haki ya kupata gawio la mali?
 
Hizo sms zikifikishwa tu polisi, itafunguliwa kesi ya jinai.

Penal code inaeleza wazi kuwa kumtishia mtu maisha ni kosa la jinai.

Ila wakati mwingine, polisi huwa inafanya double standard kuangalia, yule aliyemtishia mwenzake maisha ana nafasi gani ndani ya jamii.

Si tumeshuhudia kule mjengoni, mzito mmoja kumtishia yule dogo wa kutoka kule ziwa Tanganyika kuwa atamnyofoa kichwa chake, na hatujaona jeshi lá polisi kumdaka huyo nguli wa mambo ya sheria, angalau tu limhoji, alikuwa ana maana gani kusema, kichwa cha huyo mbunge, kitakuwa halali yake!
 
Unawaza gawio tu! Hiyo ni police case na haihusiani na mambo ya ndoa.

Focus! Kama hamna amani kiasi cha kutishiana uhai hiyo ndoa inasaidia nini?

Hujanielewa kaka, namaanisha nimekuta sms za njama za mauaji juu yangu na zimetoka kwa baba na mama mkwe wangu, nia yao kubwa ni eti nikifa au kutengana nae nitawaachia mali nyingi. Hawajanitishia kuniua ila ni njama za kuniua
 
Aisee huyo mkeo kabila gani,unaugomvi wowote na Huyo mkeo?
 
Hujanielewa kaka, namaanisha nimekuta sms za njama za mauaji juu yangu na zimetoka kwa baba na mama mkwe wangu, nia yao kubwa ni eti nikifa au kutengana nae nitawaachia mali nyingi. Hawajanitishia kuniua ila ni njama za kuniua

Hivi kweli kabisa hapo unataka sheria ikuongoze la kufanya???!!!
Ukikuta sheria inasema umpende zaid na mali zako umuandikishe yeye utafuata???!!!

Au njama zilianza na kukupumbaza akili
 
Piga chini tu hakuna ndoa hapo. Hayo mengine mwachie na upumbavu wake kwani mali kitu gani.
 
Sijawahi kuelewa na sintokaa nielewe ni kitu gani kinatusukuma watu kufikia hatua ya kupanga kuwaua spouses wetu. Marriages sometimes can be very complicated, sidhani kama killing someone is needed.
americana sms za njama ya kuua ni ushahidi tosha and this is no longer marriage issue sort this one out kwanza mambo ya mali sio muhimu kwa sasa.
 
Last edited by a moderator:
Hujanielewa kaka, namaanisha nimekuta sms za njama za mauaji juu yangu na zimetoka kwa baba na mama mkwe wangu, nia yao kubwa ni eti nikifa au kutengana nae nitawaachia mali nyingi. Hawajanitishia kuniua ila ni njama za kuniua
Wewe vipi? Mbna unakuwa mbishi? Kwani kufanya njama za kukuua siyo kosa la jinai?

Hivi hujawahi kusikia watu kukamatwa kwa tuhuma za kufanya njama za kuua, kuiba, nk?

Maji yameshakuwa ya uvuguvugu endelea kukaa ndani ya chungu yatakuchemkia na kukumaliza humo humo chunguni.

Hamna cha sheria ya ndoa hapo bali kula njama za kutaka kuua ni kosa la jinai. So, peleka hilo suala polisi. Kama hutaki basi subiri mpaka watekeleze njama zao, wakishakuua basi uwataarifu polisi.
 
Wasubiri kwanza wakuue ndyo uende police.chekecha akili mapema,gawana mali kabla kifo haijakufikia,peleka sms police
 
Mkuu americana,kwanza si kila kitu kinachotokea katika ndoa ni suala la kindoa.Pili, suala lako ni la kijinai na unapaswa kufuata taratibu za kijinai kulishughulikia. Kusanya nyaraka na ushahidi mwingine ufanye linalotakiwa. Tatu, suala lako ni kubwa na ukichelewa litakugeukia.
 
Last edited by a moderator:
This is police case.
Has nothing to do with law of marriage.
Peleka huo ushahidi polisi...

Swala la kugawana mali si la msingi kabisa kwa sasa kwenye hili swala.
 
hahahaha... mkeo kabila gani/ amekuchoka man ..tafuta ustaarabu mwingine lasivyo uta danja

Mods: Hivi huwa mnatumia vigezo gani kujua account ya mtu haitumiki tena humu JF/ yani mfano mtu akifa hivi..
 
Back
Top Bottom