Mba kichwani (Dandruff): Fahamu Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Mhafidhina

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
549
22
1595193740733.png

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI:
Wanajamii natumaini hamjambo.

Naomba mnisaidie ni dawa gani nzuri kwa ajili ya Mba. Nimejaribu kutumia dawa mbali mbali ikiwa ni pamoja na shampoo pamoja na kuosha nywele mara 3 kwa siku lakini bado naona mba haziiishi.

Naomba mnisaidie ni dawa gani nzuri kwa ajili ya Mba.

Asanteni.
---

Amani kwenu wote.

Ninakerwa sana na tatizo la kuwa na mba kwa kiasi kikubwa kwenye nywele za kichwani. Hii ni tangu nikiwa mtoto mdogo. Nimejaribu njia mbalimbali bila mafanikio;
  • Nimejaribu dawa mbalimbali, kuna zile dawa za cream/za kupaka kama vile Candisdat na nyinginezo
  • Nimejaribu dawa fulani wanauza kwenye vichupa imeandikwa "Dawa ya Mba", ni ya kijani, na naona nia jamii ya Spirit/Alchols..
  • Mwishoni mwa mwaka jana niliamua kunyoa upara kwa wembe kama mara tano mfululizo huku nikitumia dawa hizo, lakini tatizo lipo palepale.
Mba ni kwa kiasi kikubwa sana, hata nikikuna kichwa kidogo tuu unamwagika, I hate this.
Pia huwa napatwa na fungus miguuni lakini siyo wakati wote, kuna kipindi tuu huwa wanatokea, then wanaisha, na wanatokea tena kipindi fulani.

Nitashukuru sana kama kuna mtu ananisaidia kupata ufumbuzi wa hili, linaniudhi sana.
Asanteni.
---
Hivi wadau mba ni nini? Kitu gani husababisha mba za kichwani? Mfano mimi nina nywele fupi na ninajitahidi sana usafi lakini bado mba wananisumbua na kichwa huwa kinaniwasha nikijikuna na kitana unabaki ungaunga unaoashiria ni mba..je nifanye nini?
---
Habari ya asubuhi wana JF kwa wanaofahamu dawa za mba wa kichwani tuelekezane, pili nimeamka sikio likiwa linaniuma sana nashindwi kuelewe tatizo nimelia au la maana hata sielewe kwa mwenye uelewa na hayo mambo mtueleze mimi ni mgeni nimefungua jana account na nimeona watu wanatoa ushauri mzuri asanteni karibuni

UFAFANUZI WA KINA WA TATIZO LA MBA KICHWANI (DANDRUFF):

Mba ni ugonjwa wa ngozi unaowapata watu wengi na kusababisha kuwepo kwa vipande vidogo vidogo vyeupe vya ngozi kama ukurutu, ambavyo huweza kukudhalilisha, kuwasha na kuuma muda mwingine. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa matunzo mazuri ya ngozi na kichwa.

Kisayansi, kawaida ngozi hujimenya seli za ngozi ziliyozeeka, na hizi seli hupotea bila kugundulika. Vipande vidogo vya mba vinasababishwa na ongezeko la seli za ngozi katika kichwa, ongezeko hili husababisha pia ongezeko la seli za ngozi zilizozeeka kutolewa. Seli hizi zikikutana na mafuta kwenye nywele na kichwa, pamoja zinaonekana na kufanya mba. Mba huchangia sana kukatika kwa nywele na kufanya nywele zisiwe na afya nzuri au kukua vzr.

UTAGUNDUAJE KUWA UNA MBA
Kubanduka kwa ngozi ya kichwa kwa kasi(Kubanduka huku kuna ambatana na kuwashwa kwa ngozi ya kichwa, ambapo inapelekea kuwepo kwa vipande vidogo vidogo vyeupe vya ngozi(ukurutu) kwenye kichwa, nywele na mabega.

AINA ZA MBA KICHWANI
Kuna aina mbili za mba katika kichwa:
- Mba wa kawaida/ wastani aina hii inaweza kutibika kwa matumizi ya shampoo, na tiba asili za kutengeneza nyumbani kama vile mafuta ya nazi na juice ya alovera, castor oil, juice ya limao n.k

- Mba mkali au uliokithiri, aina hii ya mba katika kichwa inaambatana na kuwashwa kwa kichwa, kuvimba na uwepo wa mba wenye urefu sawa na nywele za kichwani. Mba katika hatua hii unaweza kutibika kwa dawa zilizoshauriwaa na wataalamu wa afya.

MBA UNASABABISHWA NA NINI?
Hakuna chanzo maalumu kinachojulikana cha mba katika kichwa, ila zipo sababu ambazo zinatajwa na watu kuwa vyanzo vya mba kichwani. Miongoni mwa visababishi vya mba katika kichwa ni kama:
  • Uchafu: usafi duni wa kichwa na nywele ni moja ya sababu za kuwa na mba kichwani, ni vema kusafisha kichwa na nywele mara tatu mpaka nne kwa wiki au mara moja kwa wiki kama nywele zako ni ndefu
  • Kutumia mafuta ya mgando kichwani ambayo yanapelekea kuganda kichwani na kuleta mba
  • Pia unapokwangua mba ndio unapozidi kutapakaa au kusambaa
Vyanzo vingine vya mba kichwani vinatajwa kuwa:
  • Utumiaji wa vipodozi vya nywele sana kama vile gelly za kulainisha nywele.
  • Kuwa na ngozi kavu sana kichwani (spray mchanganyiko wa maji na mafuta kila inapobidi)
  • Kutumia vitu kama chanuo, brash, kitana pamoja na mtu mwenye mba
  • Utumiaji wa hali ya juu wa “chlorinated swimmimg pools”.
  • Utumiaji wa bidhaa zenye chumvi au maji ya chumvi kwenye nywele

MATIBABU YA MBA KICHWANI
  • Mba unaweza kupotea ghafla bila matibabu au unaweza kuhitaji kutunza kichwa na nywele kwa kutumia shampoo isiyo na viambata sumu. Mara nyingine mba katika kichwa unaweza kuchukua wiki nyingi kutibika. Baadhi ya matibabu ya mba wa kichwani yanaweza kuwa ya tiba asili au tiba ya kisasa.
  • Inashauriwa zaidi kutumia tiba ya asili kutibu mba wa kichwani, mojawapo wa tiba hizo za asili ni kama:
  • Mafuta ya nazi original na juice ya kutengeneza ya alovera. Juisi ya alovera inatumika pamoja na shampoo ya kuosha kichwa na nywele na mafuta ya nazi kwaajili ya kulainisha ngozi na nywele.
  • Juice ya limao, juice ya limao ina citric acid inayoweza kushambulia fangasi zinazosababisha ukurutu wa ngozi ya kichwa na pia inasaidia kupandisha juu ngozi zilizokufa juu na kuweza kuzisafisha kwa urahisi.
NB: Kamua limao na upate juice ambayo itatumika kusugua kichwani kisha suuza na maji,fanya hivi kila ukitaka kuosha nywele.
Castor oil original (paka kila asubuhi kwenye ngozi ya kichwa iliyo safi)

UTAJIKINGA VIPI USIPATE MBA
Ni vema kchukua hatua ili kuzuia mba kichwani ili usifikie hatua ya hatari zaidi, Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayoweza kufuatwa ili kupunguza au kutokomeza kabisa mba kichwani:
  • Kula kawaida, mlo wenye afya ulio jumuisha matunda na mbogamboga kwa wingi. Punguza vyakula vyenye mafuta, sukari na chumvi kwa wingi.
  • Safisha kichwa na nywele zako walau mara tatu mpaka nne kwa wiki au mara moja kama nywele zako ni ndefu na suuza kwa maji mengi.
  • Epuka vitu vyenye chemicals nyingi kwenye nywele (Tumia vitu vya asili kwa nywele zako kama mafuta ya kupika nyumbani ya nazi, juice ya aloevera, castor oil au juice ya limao kutibu nywele zako).

USHAURI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU:
Kwa suala la mba, nikushauri kitu kimoja. Kila siku uogapo, safisha kwa maji ya kutosha nywele zako. Acha povu la sabuni kama dk 2 hivi. Then suuza, paka povu mara ya 2. Ni vizuri kuwa na medicated soap. Tumia family soap.

Kwenye saluni unaponyoa, hakikisha anafuta vizuri mashine, epuka kuchangia kitu kama chanuo nk.

Kwa uelewa wangu, na uzoefu pia, mba ni matokeo ya uchafu kwa kiasi fulani.

Kuhusu dawa ya fangasi wa miguu, kamwe usivae soksi mara 2. Uwe na pea kama kumi hivi.

Pamoja na hilo tumia dawa hii 'Clotrimazole Cream USP- CLOB' Ni nadra kuipata na mara nyingi famasi wanakupambikia kwani Clotrimazole zipo aina nyingi. Fangasi itakuwa history.
---
Ponda ponda majani na mizizi ya ufuta kwa pamoja. Chemsha ndani ya maji halafu chuja

Matumizi:
Suuza nywele kwa maji hayo kila unapomaliza kuoga jioni.

Kitunguu thaumu na siki ya tufaha (apple)
    • kitunguu saumuumu 3 vikubwa
    • siki ya tufaha (apple cedar).700ml
Ponda vizuri vitunguu saumu tia kwenye siki, koroga vizuri tia kwenye chupa ya bilauri (siplastik) weka kwenye mwanga wa jua muda wa wiki 1.

Matumizi:
Utajipaka kichwani huku ukisugua mara1 kila siku kwa muda wiki 1, baadae utatumia kujipaka mafuta ya zeituni (olive oil) kwa muda wa wiki 1.

Ndimu au siki
Juisi ndimu au siki kijiko1cha chakula weka kwenye glasi 1 ya maji ya kawaida.

Matumizi:
Paka kwenye nywele baada ya saa 1 oshanywele fanya hivi wiki mara 1.

Tui la nazi
Baada kuosha nywele zako vizuri, malizia kwa tui la nazi.

Mbegu za ndimu na pilpili manga
Pondaponda kwa pamoja kwa kipimo sawa

Matumizi:
Paka dawa hii kila siku jioni.
---
papaya.jpg



Mbegu za papai tiba ya mba
Pia mapapai yaliyoiva yanatibu mapunye (ringworm), mabichi yanatibu msukumo mkuu wa damu (high blood pressure), mapapai yanatumika kama mkuyati (aphrodisiac), yanatumika kama kituliza maumivu (analgesic), mbegu za mapapai zinapunguza maumivu ya tumbo (stomachache).

Mba au mabaka mabaka kwenye ngozi ni miongoni mwa mambo yanayosababisha ngozi kukosa muonekano mzuri na hata kumfanya mhusika mwenye matatizo kujikuta akijikuna kila wakati.

Kitaalamu mba ni aina mojawapo ya magonjwa yanayoambukizwa na fangasi ambao husababisha muwasho.


Wanawake wengi wanakumbana na matatizo haya ya mba, kutokana na kupaka aina ya vipodozi vinavyowaletea athari katika ngozi zao.

Unapokumbana na tatizo la namna hii ni vizuri kujipaka dawa zinazofaa badala ya kutafuta krimu ambazo ni hatari zaidi. Mbegu za papai ni tiba nzuri na ya asili ambayo haiwezi kukuletea madhara zaidi.

Jinsi ya kuondoa mba kwenye ngozi ya uso.

Mbegu za papai ni dawa ya asili inayoweza kutibu ngozi yako na kukuondolea tatizo la kuwashwa au mabaka yanayokukabili.

Namna ya Kutumia kama ni Dawa Mbegu za Papai.
Unachotakiwa kufanya ni kuzipondaponda na kujipaka kwenye eneo lililoathirika na mba. Hii itasaidia kuondoa ugonjwa huo na kuiacha ngozi yako ikiwa safi na yenye afya nzuri.

Unaweza kutumia krimu maalum za kuondoa mba hizo, zinapatikana katika maduka ya dawa, lakini unachopaswa kufanya ni kufuata masharti na kupaka kwa umakini kwenye sehemu ilioathirika.

Waweza pia kutumia sabuni maalum ya maji, shampoo, poda na hata baadhi ya losheni zote hizi zinaweza kuisafisha ngozi yako na kuifanya iondokane na muwasho unaokukera na wakati huo kuiacha ngozi yako ikiwa safi na yenye kuvutia. tumia kisha unipe feedBack Mkuu Pumb
---
Osha/ sugua ngozi yako ya kichwa na shampoo iliyoandikwa anti-dandruff, kila unapooga.

Hakikisha unatumia hair food(mafuta special ya ngozi ya kichwa)baada ya kuoga.

Nadhani Unga unatokana na kushare vitana, taulo, kutopaka mafuta au pia kutoiosha na shampoo scalp yako.
pia inawezekana kuwa mafuta unayotumia si bora/ hayaendani na ngozi yako.
---
Maradhi ya Mba Hutokana na ngozi iliyokufa katika kichwa yaani dead cell.
dawa zilizopo ni :

Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe dafi dafi halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

Fenugreek kwa kiswahili inaitwa (Uwatu) lakini imekaa kama rangi yake ni ya brown imekaa kama Vijiwe jiwe vidogodogo kama kuna Hii Uwatu unachukua vijiko 2 vya chai vya fenugreek unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unaziponda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu yoyote.
---
Na mimi pia ninashukuru kwa kutuletea shukrani kwako usikose na kuweka (like) ninakuongezea dawa nyingine ya Mba mkuu Pumb Mba hutokana na ngozi iliyokufa katika kichwa yaani dead cell.Dawa zilizopo ni :


Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe dafi dafi halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

Fenugreek kwa lugha ya kiswahili inaitwa Uwatu . Hii unachukua vijiko 2 vya chai vya Uwatu (fenugreek) unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unaziponda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu yoyote. tumia kisha uje unipe Feedback.


707px-Fenugreek-methi-seeds.jpg

Fenugreek Uwatu.
---
Mpendwa hicho kinachoitwa mba si kila mara kinabeba maana halisi ya mba.Kwa maana halisi ya mba kama zile unazoona kifuani, shingoni au kwenye mashavu zile kila mtu anakuwa nazo kama sehemu ya vimelea vya kawaida kwenye ngozi ambavyo kuonekana kwake kunategemea mabadiliko fulani ktk ngozi. Kwa mfano wakati kuna hali ya hewa ya unyevu unyevu au wakati wa ujauzito au ukitumia kemikali(inaweza kuwa sabuni,cream nk.) ambazo zinapunguza kinga ya mwili/ngozi nk..nk..nk..Unaweza kutumia dawa ya kawaida ya fangasi zikapotea..ila zinaweza kujitokeza tena ikiwa hali ile ya mwanzo itajitokeza tena(maana kumbuka vimelea vyake vipo tu wakati wote)..Aina hii inatumalizia sana hela ktk kununua dawa..tunaibiana sana ktk hilo lakini kiukweli hakuna uwezekano wa kuzimaliza kabisa kutokana na sababu niliyotoa hapo mwanzo..

Hizi za kichwani ndipo panapohitaji unifuatilie vizuri

Tumia mfano huu:

Naelewa unatumia taulo hapo nyumbani..taulo huwa linachafuka,siyo? Ulishawahi kuiuliza linachafuka vipi wakati unalitumia uikiwa umeoga..mwili msafi? Unajua pia ni kwa nini tunapauka ikiwa hatujajipaka mafuta hata kama tumeoga?

Majibu:
Kila wakati ngozi yetu inajitengeneza upya..kwa maana kwamba chembechembe(cells) mpya za ngozi zinazaliwa huku zile za zamani zikipukutika..cells zinazaliwa kutokea ndani ya ngozi kuja juu..kama ambavyo mti unavyotengeneza maganda;kwamba ganda la nje linakuwa kavu/limekufa..kwa hiyo basi cells za juu/nje ya ngozi zinakaa kwa muda mfupi,zinakufa kisha zinapukutika..sasa hizo cells zinazopukutika ndizo kimsingi zinamaanisha ule mpauko au huchangia kuchafua taulo..ukipata mchubuko kidogo kwenye ngozi utaona kijiganda kidogo mfano wa nailoni..kile kimetengenezwa na hizi cells ninazozungumzia hapa.

Kwa upande mwingine,baada ya kuoga vizuri kisha ukakauka bila kupaka mafuta,kutakuwa na kipindi fulani ambapo ngozi itapauka..hii inatokana na kuonekana kwa sehemu ya juu iliyokufa ya hicho kinailoni nilichosema hapo juu..maana yake inakuwa inapukutika ili kuachia cells/kinailoni kipya kukaa pale juu! Lakini huu mpauko baada ya muda huanza kupotea taratibu na ngozi kuonekana ktk hali ya kawaida..hii hutokana na ngozi kujitengenezea mafuta fulani kutoka ndani yanyosukumwa kuja kunawirisha sehemu ya juu ya ngozi..

Sasa tatizo lako nini?
Kama nilivyoelezea ukuaji wa ngozi hapo juu..ninamaanisha ni pamoja na ngozi ya kichwa.Mchakato huo wote unafanyika pia kwenye ngozi ya kichwa sawa sawa kabisa na sehemu nyingine za mwili..Tunapokuwa tunaoga tunaondoa ile sehemu ya ngozi iliyokufa pamoja na uchafu mwingine ktk ngozi yetu..Sasa ktk sehemu nyingine za mwili ni rahisi kuondoa kila uchafu na kisha kujifuta vizuri ili kuacha ngozi ikiwa safi..Lakini hii ni tofauti na ngozi ya kichwa.Kule kuna nywele hivyo si rahisi kuondoa na kufuta uchafu wote(hapa namaanisha zile cells zilizokufa pamoja na uchafu mwingine)..Kushindwa kuondoa uchafu huo kunapelekea kuzidi kuongezeka kwa hizo cells zilizokufa na matokeo yake kunakuwa kama vumbi fulani hivi jeupe..ni rahisi kuliona wakati unachana nywele..Ule muwasho ni matokeo ya huo uchafu..Sasa hapa ndipo watu wanapokosea kuita MBA..kiuhalisia si mba za kawaida ila ni mchakato wa kawaida wa ukuaji wa ngozi!

Sasa mtu mwingine anaweza uliza mbona watu wengine hawana tatizo hilo? Jibu ni kwamba,si kweli kwamba hawana..maana hiyo itakuwa ni kusema kwamba,ukuwaji wa ngozi yao ni tofauti na watu wengine..hapana..kuwezakuwa ukuaji wa wa ngozi taratibu sana..au muda mwingi ngozi ya kichwa chake inakuwa na unyevu au mafuta mafuta(kumbuka nadharia ya kupauka)..lakini hii haimaanishi kwamba cells zake hazifi na kutengeneza uchafu..Lakini pia inawezekana watu wengi tunalo hilo tatizo ila hatusemi hadharani!

Tatizo hili ni kubwa kwa watu wenye nywele ndefu..na ni hakina kabisa kwamba kwa watu wasiofuga nywele kwao si tatizo kabisa..Niseme mapema kwamba si kweli kwamba kuwa na tatizo hili kunamaanisha mtu haogi vizuri..hapana.. Kwa jinsi ngozi ya kichwa ilivyo na nywele inafanya uwepo ugumu wa wa namna bora ya kusafisha ile ngozi.

Mimi mtu angeniuliza afanye nini ili kuondokana na tatizo hili..jibu langu lingekuwa fupi tu..USIRUHUSU NYWELE KUWA NDEFU!! Najua hii si habari njema kwa akina dada na akina mama..lakini huo ndio ukweli wenyewe.

Kwa hiyo @Anne deo kusema una mba sugu mimi nitasema sio..
 
Ni mba gani wanakusumbua vibalango, mashilingi, mapunye au mba hawa tunaopata wakati tunasuka nywele?
 
Ni mba gani wanakusumbua vibalango, mashilingi, mapunye au mba hawa tunaopata wakati tunasuka nywele?

Ni kama vipele vipele hivi halafu vinauma sana. Nimejaribu shampoo mbalimbali lakini haviishi. Vinaptea kwa muda halafu vinarudi tena. Tafadhali naomba msaada wako manake vinakua kama ni mashilingi hivi na hivyo yanafanya nijisikie vibaya sana
 
Mimi nakushauri bora uende uonane na daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi. utapata ufumbuzi wa tatizo lako. Pole sana.
 
Mimi nimetumia mafuta ya kupaka yanaitwa CONFIDENCE, yamenisaidia sana. Umeshajaribu haya?
 
Nenda upatiwe vidonge Grifulvin or Fulconazole umeze mba wataisha. Mafuta ya confidence, virgin hair, sulphur pia yanasaidia.
 
Wana JF naomba kama kuna yeyote anayefahamu matibabu ya mba unaotokea haswa kichwani kwa watoto wadogo. Nini chanzo chake?
 
Dawa ecxactly siijui ila jitahidi kuwaweka safi muda wote kichwa kisikue na nywele ndefu kwa kuanzia
 
Dawa ecxactly siijui ila jitahidi kuwaweka safi muda wote kichwa kisikue na nywele ndefu kwa kuanzia

au awanyoe ubara.kila nywele zikiota.usafi muhimu.tatizo la jamaa wa hivi watoto wao kila kitu anamuachia hg.mia
 
MBA KICHWANI (DANDRUFF)
Ponda ponda majani na mizizi ya ufuta kwa pamoja. Chemsha ndani ya maji halafu chuja

Matumizi:
Suuza nywele kwa maji hayo kila unapomaliza kuoga jioni.

Kitunguu thaumu na siki ya tufaha (apple)
  • kitunguu saumuumu 3 vikubwa
  • siki ya tufaha (apple cedar).700ml
Ponda vizuri vitunguu saumu tia kwenye siki, koroga vizuri tia kwenye chupa ya bilauri (siplastik) weka kwenye mwanga wa jua muda wa wiki 1.

Matumizi:
Utajipaka kichwani huku ukisugua mara1 kila siku kwa muda wiki 1, baadae utatumia kujipaka mafuta ya zeituni (olive oil) kwa muda wa wiki 1.

Ndimu au siki
Juisi ndimu au siki kijiko1cha chakula weka kwenye glasi 1 ya maji ya kawaida.

Matumizi:
Paka kwenye nywele baada ya saa 1 oshanywele fanya hivi wiki mara 1.

Tui la nazi
Baada kuosha nywele zako vizuri, malizia kwa tui la nazi.

Mbegu za ndimu na pilpili manga
Pondaponda kwa pamoja kwa kipimo sawa

Matumizi:
Paka dawa hii kila siku jioni.
 
Ndugu yangu nashukuru sana kuna mabadiliko makubwa. kitunguu thaumu na siki ya tufaa imesaidia sana.
 
Maradhi ya Mba Hutokana na ngozi iliyokufa katika kichwa yaani dead cell.
dawa zilizopo ni :

Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe dafi dafi halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

Fenugreek kwa kiswahili inaitwa (Uwatu) lakini imekaa kama rangi yake ni ya brown imekaa kama Vijiwe jiwe vidogodogo kama kuna Hii Uwatu unachukua vijiko 2 vya chai vya fenugreek unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unaziponda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila taabu yoyote.
 
Jaribu kutumia Selsun Blue shampoo ni maalum kwa mba wa kichwani inaweza saidia.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom