Msaada: Njia ya mkojo inatoa usaha, napata maumivu makali wakati wa kukojoa

thomas_360

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
1,459
1,428
Habarini wandugu,, mim ni kijana wa kiume, tangu jana naona njia ya mkojo inaniuma na kuna wakati inatoa maji maji ya usaha nashindwa kujua nini tatizo, maana napata maumivu wakati wa kukojoa natumaini nitakuwa nimeeleweka na ninahitaji msaada wenu
 
Nashukuru kwa ushahuri...ila mchangiaji uliyeniuliza hospital sizijui naomba usinielewe vibaya..nn maana yakuwa na hii forum?? Kuna vitu vingine unavipata hata kabla hujaenda mahali husika zaidi
 
Habarini wandugu,, mm ni kijana wa kiume, tangu jana naona njia ya mkojo inaniuma na kuna wakati inatoa maji maji ya usaha nashindwa kujua nini tatizo,, maana napata maumivu wakati wa kukojoa..natumaini nitakuwa nimeeleweka na ninahitaji msaada wenu

UGONJWA WA KISONONO (GONORRHOEAE) NI NINI?

Kisonono ni ugonjwa kati ya magonjwa ya
zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya
Neisseria gonorrhoeae, bakteria ambao
hukua na kuzaliana kwa haraka katika
sehemu zenye unyevunyevu na joto
mwilini kama kwenye shingo ya kizazi kwa
wanawake (cervix), mirija ya kupitisha
mkojo au shahawa (urethra), mdomoni na
kwenye puru.

Maambukizi mengi kwa
wanawake hutokea kwenye shingo ya
kizazi (cervix). Asilimia 75 ya ugonjwa wa
gono hutokea kwa watu wenye umri wa
miaka 15 – 29, wanawake walio katika
umri wa miaka 15 -19 na wanaume walio
katika umri wa miaka 20 – 24 wako
kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa
huu.

Ugonjwa huu huambukizwa vipi?
Ugonjwa huu huambukizwa kupitia
vitendo vya ngono kupitia uke, njia ya haja
kubwa (anus), kupitia mdomoni (oral sex).
Ugonjwa unaweza kujitokeza kwenye
sehemu za kujamiana, kwenye mdomo na
kwenye puru (rectum).

Ugonjwa wa gono
huonekana sana kwa vijana, watu wenye
maisha duni kiuchumi, watu wanaoishi
mijini, watu weusi na watumiaji madawa
ya kulevya.
Dalili za ugonjwa wa kisonono
Dalili za ugonjwa wa kisonono huanza
kujitokeza kuanzia siku ya 2 hadi ya 7
baada ya mtu kupata maambukizi na
huweza kuchelewa kwa wanawake.
Dalili ni kama zifuatazo;
Kwa wanaume:

Kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa
(burning sensation)
Kutokwa na majimaji ya njano au
meupe au ya kijani kutoka kwenye
uume yanayoambatana na maumivu
makali sana
Wakati mwengine maumivu au kuvimba
kwa korodani (swollen testicles)
Maambukizi yakiwa kwenye puru
(rectum) huambatana na maumivu
wakati wa kujisaidia haja kubwa,
kuwashwa sehemu za haja kubwa, na
hata haja kubwa inaweza kutoka
ikiambatana na damu, hii inatokea kwa
wanaume na wanawake.


Kwa wanawake:

Dalili kwa wanawake huwa si nyingi
lakini wanawake wengi hawaonyeshi
dalili zozote
Maumivu au kuhisi kama kichomi
wakati wa kukojoa
Kuongezeka kwa kutoka majimaji
kutoka kwenye tupu ya mwanamke
ambayo ni ya njano au
yamechanganyika na damu
Kutokwa na damu kupitia tupu ya
mwanamke kabla ya hedhi kufika.
Kutokwa na damu baada ya kujamiana
au baada ya tendo la ndoa
Kichefuchefu
Homa (fever)
Kutapika

Vipimo vya ugonjwa wa kisonono’


Swab for culture – Kipimo hiki
hufanyika maabara kwa kupandikiza
bakteria baada ya kufuta sehemu za siri
kwa kutumia swab ili kuona kama kuna
bakteria wanaosababisha gono.
Polymerase Chain Reaction (PCR) –
Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) ya
bakteria, ni ghali sana.


Tiba ya ugonjwa wa kisonono ni nini?

Tiba ya gono inahusisha na tiba ya
ugonjwa wa Chlamydia kwani mara nyingi
magonjwa haya huambatana kwa
pamoja.Tiba hutegemea na umri wa
mgonjwa na kama mtu ni mjamzito au la.
Tiba ya gono ambayo sio sugu iliyo
kwenye shingo ya kizazi (cervix), urethra
na
puru, dawa zinazotumika ni aina za
cephalosporin dozi moja pamoja na dawa
za aina ya macrolide antibiotics (mfano
azithromycin) na za jamii ya penicillin
(mfano doxycyclin) ili kutibu ugonjwa wa
chlamydia.
Mara nyingi kwa wale chini ya
miaka 18 na wanawake wajawazito,
hutibiwa kwa kuchomwa sindano.
Fuata
ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa
hizi kwani dawa nyingi zina madhara kwa
wajawazito (mfano doxycyclin).

Ushauri
nasaha hutolewa kwa wapenzi wote
wawili na ni vizuri wapenzi wote wawili
kutibiwa hata kama mmoja hana dalili za
ugonjwa huu.
Madhara ya ugonjwa wa
kisonono

Kutoweza kuzaa kwa mwanamke (tasa)
au kutoweza kutungisha mimba kwa
mwanamume (infertility)
Huweza kuathiri moyo (heart valves),
ubongo,ngozi nk ambayo ni hatari sana
kwa mtu yoyote.
Madhara kwenye sehemu za maungio
au jointi (joint inflammation)
Kwa wanawake wale ambao
hawajatibiwa wanaweza kupata
ugonjwa wa PID (Pelvic Inflammatory
Disease) ambao huongeza asilimia ya
mwanamke kuwa tasa.


Wale wanawake ambao ni wajawazito
na wameambukizwa gono wako
kwenye hatari ya mimba kutoka au
kuzaa mapema kabla mimba haijatimiza
umri wake (preterm labor).
Kwa wale wanaoambukizwa gono
kipindi cha kukaribia kujifungua,
wanaweza kuwaambukiza watoto wao
na hivyo watoto kupata ugonjwa wa uti
wa mgongo (meningitis), kuwa kipofu
(blindness), homa ya mapafu
(pneumonia) na ugonjwa wa mifupa
(septic arthritis).

Kinga ya kisonono
Kutumia kondomu wakati wa
kujamiana.
Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
Kuacha vitendo vya ngono kama
matumizi ya vifaa vya ngono hasa kwa
wanawake mfano vibrators nk.


Kwa wanawake wajawazito – Hakikisha
unahudhuria kliniki mapema ili upate
kuchunguzwa na kupatiwa tiba
muafaka kama utagundulika na
ugonjwa wa gono au ugonjwa
mwengine wowote.

Wanawake wajawazito wanashauriwa
kujifungulia hospitali ili kama mtoto
ameathirika na gono apate matibabu ya
haraka baada ya kuzaliwa kuepusha
kuwa kipofu.
Epuka kufanya ngono na mtu
aliyeambukizwa gono.


“Kumbuka ya kwamba hakuna kitu kama
ngono salama kwani huwezi kujua kama
wewe au mwenzako wakati wa kujamiana
ameathirika au la, au una michibuko au
umekatika kwenye ngozi au la kwani
michibuko mengine inaweza isionekane
au kugundulika kwa urahisi.
Njia pekee na
nzuri ni kuacha au kujikinga na vitendo
vya ngono”.
Mtu aliyepata gono awali
anaweza kupata tena.
 
Habarini wandugu,, mm ni kijana wa kiume, tangu jana naona njia ya mkojo inaniuma na kuna wakati inatoa maji maji ya usaha nashindwa kujua nini tatizo,, maana napata maumivu wakati wa kukojoa..natumaini nitakuwa nimeeleweka na ninahitaji msaada wenu
Utakuwa una U. T. I kali sana nakushauri ufike hospital mapema kwa uchunguzi huo
 
Powerceff ndo tiba hapo.kama imeanza kutoa usaha ,kuna uwezekano ikawa kisonono au gono
 
UGONJWA WA KISONONO (GONORHEA) NI NINI?

Kisonono ni ugonjwa kati ya magonjwa ya
zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya
Neisseria gonorrhoeae, bakteria ambao
hukua na kuzaliana kwa haraka katika
sehemu zenye unyevunyevu na joto
mwilini kama kwenye shingo ya kizazi kwa
wanawake (cervix), mirija ya kupitisha
mkojo au shahawa (urethra), mdomoni na
kwenye puru.

Maambukizi mengi kwa
wanawake hutokea kwenye shingo ya
kizazi (cervix). Asilimia 75 ya ugonjwa wa
gono hutokea kwa watu wenye umri wa
miaka 15 – 29, wanawake walio katika
umri wa miaka 15 -19 na wanaume walio
katika umri wa miaka 20 – 24 wako
kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa
huu.

Ugonjwa huu huambukizwa vipi?
Ugonjwa huu huambukizwa kupitia
vitendo vya ngono kupitia uke, njia ya haja
kubwa (anus), kupitia mdomoni (oral sex).
Ugonjwa unaweza kujitokeza kwenye
sehemu za kujamiana, kwenye mdomo na
kwenye puru (rectum).

Ugonjwa wa gono
huonekana sana kwa vijana, watu wenye
maisha duni kiuchumi, watu wanaoishi
mijini, watu weusi na watumiaji madawa
ya kulevya.
Dalili za ugonjwa wa kisonono
Dalili za ugonjwa wa kisonono huanza
kujitokeza kuanzia siku ya 2 hadi ya 7
baada ya mtu kupata maambukizi na
huweza kuchelewa kwa wanawake.
Dalili ni kama zifuatazo;
Kwa wanaume:

Kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa
(burning sensation)
Kutokwa na majimaji ya njano au
meupe au ya kijani kutoka kwenye
uume yanayoambatana na maumivu
makali sana
Wakati mwengine maumivu au kuvimba
kwa korodani (swollen testicles)
Maambukizi yakiwa kwenye puru
(rectum) huambatana na maumivu
wakati wa kujisaidia haja kubwa,
kuwashwa sehemu za haja kubwa, na
hata haja kubwa inaweza kutoka
ikiambatana na damu, hii inatokea kwa
wanaume na wanawake.


Kwa wanawake:

Dalili kwa wanawake huwa si nyingi
lakini wanawake wengi hawaonyeshi
dalili zozote
Maumivu au kuhisi kama kichomi
wakati wa kukojoa
Kuongezeka kwa kutoka majimaji
kutoka kwenye tupu ya mwanamke
ambayo ni ya njano au
yamechanganyika na damu
Kutokwa na damu kupitia tupu ya
mwanamke kabla ya hedhi kufika.
Kutokwa na damu baada ya kujamiana
au baada ya tendo la ndoa
Kichefuchefu
Homa (fever)
Kutapika

Vipimo vya ugonjwa wa kisonono’


Swab for culture – Kipimo hiki
hufanyika maabara kwa kupandikiza
bakteria baada ya kufuta sehemu za siri
kwa kutumia swab ili kuona kama kuna
bakteria wanaosababisha gono.
Polymerase Chain Reaction (PCR) –
Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) ya
bakteria, ni ghali sana.


Tiba ya ugonjwa wa kisonono ni nini?

Tiba ya gono inahusisha na tiba ya
ugonjwa wa Chlamydia kwani mara nyingi
magonjwa haya huambatana kwa
pamoja.Tiba hutegemea na umri wa
mgonjwa na kama mtu ni mjamzito au la.
Tiba ya gono ambayo sio sugu iliyo
kwenye shingo ya kizazi (cervix), urethra
na
puru, dawa zinazotumika ni aina za
cephalosporin dozi moja pamoja na dawa
za aina ya macrolide antibiotics (mfano
azithromycin) na za jamii ya penicillin
(mfano doxycyclin) ili kutibu ugonjwa wa
chlamydia.
Mara nyingi kwa wale chini ya
miaka 18 na wanawake wajawazito,
hutibiwa kwa kuchomwa sindano.
Fuata
ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa
hizi kwani dawa nyingi zina madhara kwa
wajawazito (mfano doxycyclin).

Ushauri
nasaha hutolewa kwa wapenzi wote
wawili na ni vizuri wapenzi wote wawili
kutibiwa hata kama mmoja hana dalili za
ugonjwa huu.
Madhara ya ugonjwa wa
kisonono

Kutoweza kuzaa kwa mwanamke (tasa)
au kutoweza kutungisha mimba kwa
mwanamume (infertility)
Huweza kuathiri moyo (heart valves),
ubongo,ngozi nk ambayo ni hatari sana
kwa mtu yoyote.
Madhara kwenye sehemu za maungio
au jointi (joint inflammation)
Kwa wanawake wale ambao
hawajatibiwa wanaweza kupata
ugonjwa wa PID (Pelvic Inflammatory
Disease) ambao huongeza asilimia ya
mwanamke kuwa tasa.


Wale wanawake ambao ni wajawazito
na wameambukizwa gono wako
kwenye hatari ya mimba kutoka au
kuzaa mapema kabla mimba haijatimiza
umri wake (preterm labor).
Kwa wale wanaoambukizwa gono
kipindi cha kukaribia kujifungua,
wanaweza kuwaambukiza watoto wao
na hivyo watoto kupata ugonjwa wa uti
wa mgongo (meningitis), kuwa kipofu
(blindness), homa ya mapafu
(pneumonia) na ugonjwa wa mifupa
(septic arthritis).

Kinga ya kisonono
Kutumia kondomu wakati wa
kujamiana.
Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
Kuacha vitendo vya ngono kama
matumizi ya vifaa vya ngono hasa kwa
wanawake mfano vibrators nk.


Kwa wanawake wajawazito – Hakikisha
unahudhuria kliniki mapema ili upate
kuchunguzwa na kupatiwa tiba
muafaka kama utagundulika na
ugonjwa wa gono au ugonjwa
mwengine wowote.

Wanawake wajawazito wanashauriwa
kujifungulia hospitali ili kama mtoto
ameathirika na gono apate matibabu ya
haraka baada ya kuzaliwa kuepusha
kuwa kipofu.
Epuka kufanya ngono na mtu
aliyeambukizwa gono.


“Kumbuka ya kwamba hakuna kitu kama
ngono salama kwani huwezi kujua kama
wewe au mwenzako wakati wa kujamiana
ameathirika au la, au una michibuko au
umekatika kwenye ngozi au la kwani
michibuko mengine inaweza isionekane
au kugundulika kwa urahisi.
Njia pekee na
nzuri ni kuacha au kujikinga na vitendo
vya ngono”.
Mtu aliyepata gono awali
anaweza kupata tena.

Jibu tosha
 
Back
Top Bottom