alovera
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 220
- 173
Naomba kulileta kwenu,ni hivi Mzee wangu (Marehemu) alikuwa na Shamba ekari 50,kati ya hizo ekari 20 zimevamiwa,tulifungua kesi kijijini lakini kijiji hakitukupa ushirikiano hivyo tukaenda Baraza la Kata tukashinda,Mpinzani wangu akaenda Baraza la Ardhi la Wilaya akakata rufaa na akatushinda sababu kubwa aliyefungua kesi hakuwa na uhalali,sababu tulikuwa hatujafungua mirathi mahakamani (Hapa ndipo tuliposhindwa kwa mara ya kwanza).
Mara ya pili tulifuata taratibu zote za kufungua mirathi,na msimamizi wa mirathi nikawa mimi tukafungua kesi Baraza la Ardhi ya wilaya,tukawashtaki aliyevamia pamoja na Serikali ya Kijiji ,tukawapa kijiji notice ya siku 30. Kilichotokea kesi ilivyoendelea ilipofika hearing Serikali ya Kijiji na Mvamizi na Serikali ya kijiji ilitetewa na wakili Mmoja na maajabu kuwa notice tuliyowapelekea walikana kuwa hawakuipokea na tena haikuonekana mahakamani pamoja na kuwa tuliwapelekea na risiti ya kulipa mahakamani tulikuwa nayo. Hivyo wakili wao akaomba shauri litupiliwe mbali na kweli likatupiliwa mbali kwa kuwa tulishindwa kuithibitishia mahakama kuwa notice haikupelekwa kijinini (nikashindwa mara ya pili).Hivi sasa tunapanga kufungua kesi baraza la ardhi la wilaya kwa mara nyingine tena
Msaada ninaomba kutoka kwenu wana Jamvi
1. Je ni sawa kijiji kutetewa na wakili Binafsi pamoja na Mtuhumiwa (Mvamizi)?
2.Utaratibu wa kuishtaki serikali ya kijiji ukoje
3.Naomba ushauri kwa ujumla jinsi ya kudai haki yetu ili tusije shindwa tena kwa technicalities?
Nawasilisha!