Msaada naomba kujua kiswahili cha maneno haya:

Chapa ambayo naipenda na chapa ninayopendelea
 
mkuu "brand that I love" ni kishazi tegemezi au dependent clause ambacho kinahitaji kishazi huru au independent clause kuikamilisha na kuwa sentensi yaani "Brand that I love is available in this shop" lakini ukisema "my favourite brand" hichi ni kikundi nomino au noun phrase na ina maana iliyokamilia. hichi kikundi nomino kimetengenezwa na " pronoun "my" adjective " favourite" na noun "brand".
hivyo sasa "brand that I love kwa kiswahili ni "bidhaa niipendayo au bidhaa ninayoipenda" ukiangalia vizuri hapa utaona kuwa hii sentensi haijakamilika na haina maana kamili.. " bidhaa niipendayo inapatikana duka hili tu" imekamilika na inamaana kamili. "my favourite brand" bidhaa yangu pendwa
nawasilisha.

nwalimu msomi Kashindi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom