Utengenezaji wa Sabuni za Aina Mbalimbali: Fahamu Mahitaji, Mchakato wa Uzalishaji na Masoko

Nkoboiboi

JF-Expert Member
Oct 9, 2010
243
63
102408985-crop-58adfb8c3df78c345b0bb87c.jpg


Tafadhali wana JF wenzangu,

Anayeweza kunifundisha kutengeneza sabuni naomba tuwasiliane haraka. Nina soko kubwa.


WADAU WENGINE WENYE KUHITAJI KUFAHAMU BIASHARA HII
Habari wana JF

Naomba msaada kwa mwenye ufahamu au uzoefu wa kutengeneza sabuni za kigoma maatufu kama gwanji au sabuni za magadi maana nataraji kufungua kiwanda kidogo nyumbani kwangu hapa jijini Dar, maana kwa utafiti wangu sabuni miche 20 = sh 30,000 hivyo nataka kujua gharama ya uzalishaji na changamoto zake, natanguliza shukrani kwa wote mtakao toa michango ya mawazo na mtabarikiwa.

Amen
WanaJF,

Naitaji kuanza kutengeneza sabuni za kufulia kama B 29, Star ya Uganda, Komesha n.k, mimi niko Mwanza na tatizo litakalonikwamisha ni soko sababu mwanzo ni mgumu. Naomba niwasilishe kwenu kwa maoni na ushauri zaidi.
Naomba kufahamu bei ya mashine ndogo ya kutengeneza sabuni ya mche . Wana JF kutokana na hali ngumu ya maisha kwasasa nimeona bora niwe mjariamali hii itasaidia kukuza kipato changu na nchi kwa ujumla.

Mimi ni mmoja wa watu tunaosubiri ajira za Mh. Rais Magufuli. Kitaaluma ni mwalimu. Nina hold Bachelor of Commerce in Education. Baada ya kukaa bila ajira tangu 2016 nikaona ngoja nichukue mazo ya watu wengine ili yanisaidie katika kuniingizia kipato.

Wazo lenyewe ni la kutengeneza sabuni ya mche ambayo bado sijawahi kutengeneza hata maramoja. JF kuna wataalam wazuri katika nyanja mbalimbali nikaona ngoja nije kwenu ili nipate msaada wa kimawazo na hata kimiundombinu pia kama utaona inafaa.

Hivyo basi kwaaliye tayari kutuoa maoni ama ushauri na msada mwingine atakaoona unafaa katika kufanikisha project yangu unakaribishwa sana.

Asante
Wakuu habari za leo, heri ya siku kuu ya Eid. Natumaini mu wazima, buheri wa afya.

Lengo la uzi huu ni kupeana elimu juu ya utengenezaji wa sabuni, kwa ajili ya matumizi mbalimbali (ya nyumbani na maofisini) kama vile kufuria, kuoshea vyomba na mengineyo sambamba na hayo.

Kwa wale wenye ujuzi juu ya suala hilii mnakaribishwa ili tupeane idea ili tuweze kujikwamua kwa namna moja au nyingine.

Elimu itakayotolewa hapa izingatie:

1. Aina ya sabuni (ya dawa/kawaida/unga)
2. Mahitaji kwa ajili ya kuanza kutengeneza
3. Hatua za utengenezaji
4. Soko (walengwa wa ununuzi/watumiaji )

Usisite kuchangiaa Kama unafahamu lolote juu ya utengenezaji, toa elimu hapaa pia maswali yanakarbishwa.

Tuwezeshanee wakuu. Pamoja tunajenga taifa letu.

Asantenii, naomba kuwasilisha.
Naombeni msaada kujua soko la uzalishaji sabuni za Miche,Maji na Dawa za kuuwa wadudu:

1. Mashine za utengezaji zinapakana wapi, bei gani na uwezo wa mashine katika kulazalisha kwa siku
2. Malighali inayotumika ni ipi? wananunua wapi? Be za malighafi?
3. Soko kuu la sabuni: zenye kiwango na zisizo na kiwango ni lipi!
4. Viwanda vya wazalendo na viwanda vya wageni?
5. Ushindani wa soko: je, washindani wa kuu ni wa ngapi?
6. Bei za washindani: Reja reja na jumla kwa aina za sabuni zilizopo
7. Je kuna wazalishaji wa kitanzania wanauza sabuni nje ya nchi?
8. Mitambo ama mashine za kutengeza sabuni zinapatikana wapi? zinaagizwa nje? tsh ngapi ama dola ngapi na ina uwezo gani wa kuzalisha?
9. Aina ya malighafi inayopendwa na watumiaji wa sabuni kwa lika ni ipi?
10. Gharama za msingi za uendeshaji wa mashine au kiwanda kidogo cha sabuni ni zipi?
11. Muundo wa uongozi/uzalishaji wa sabuni ukoje?
12. Kwa Dar es salaam, viwanda vya sabuni viko wapi?
13. Taratibu za kupata viwango: TBS na BAR CODE ukoje? gharama ni kiasi gani? ofisi husika?
14. Aina za sabuni zilizopo sokoni za (miche, maji, dawa)
15. Vifungashio vya sabuni za maji na vya sabuni za vipande vilivyo na kiwango vipatikana wapi? gharama ni tsh ngapi kwa bei ya jumla na reja reja?

Nataguliza shukrani za dhati kwa msaada wenu.
Heshima kwenu wadau.

Naomba masada wenu kama kuna yeyote anayejua jinsi ya kutengeneza JASIMINI ile ya kusafishia chooni.

Natanguliza shukrani.


MICHANGO YA WADAU MBALIMBALI
VIAMBATA NA MCHAKATO WA KUTENGENEZA SABUNI
Ili iitwe sabuni inatakiwa
- Ngumu kuiisha
- Yenye povu jingi
- Nyeupe

VIAMBATA VYA kutengenezea sabuni
1) Mafuta-mawese, mise, wanyana
2) Maji
3) Caustic soda (costiki soda)

VIFAA VYA KUTENGENEZEA
- Ndoo za plastiki lita 20 nne
- Diaba 1
- Mti wa kukorogea
- Mashine ya kukorogea
- Box la kugandishia
- Mhuri wa biashara
- Mzani wa saa
- Vibao vya kukatia

VIFAA VYA USALAMA
- Mask
- Groves
- Gum boots
- Goggles (miwani)
- Overall
- Ndoo ya maji au mchanga

FORMULA
- Mafuta lt1+caustic soda grm135+maji mls350+sodium siligate prm100

KUCHANGANYA
Pima maji ktk ndoo ya plastic kisa weka caustic soda ktk maji weka kidogokidogo huku ukikoroga mpaka itakapo yeyuka.mchanganyiko huu unaweza kuchemka na kutoa mosh usiogope. acha ipoe kuanzia masaa 8 na zaidi

KUCHANGANYA NA MAFUTA
Yeyusha mafuta kwa kuyapasha joto kidogo ambapo unaweza kuyashika, tia sangi na mimina kidogo2 kuchanganya michanganyiko huku ukikoroga. mimina kwenye box la kugandishia acha igande tayari kwa kukata.Pia weka sodium siligate

KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI YA KUNAWIA MIKONO

Moja kati ya mahitaji makubwa ya watu ikiwemo wafanyabiashara za mama lishe,mabucha na nyingine,ni sabuni ya kunawia. Kutokana na mahitaji makubwa waliyonayo watu na kukosekana kwa bidhaa hiyo wahitaji hujikuta wakitumia sabuni ambazo hazikutengenezwa kwa kazi hiyo kama sabuni za unga,shampoo na sabuni za vipande ambazo huwasababishia madhara bila kujijua.

Leo katika somo letu tutajifunza jinsi ya kutengeneza sabuni za kunawia mikono. Fuatana nami mwanza mpaka mwisho.

MAHITAJI:
Sulphonic acid .soda ash .maji yaliyochujwa vizuri, pafyum, Rangi yoyote inayovutia, sless, chumvi

JINSI YA KUTENGENEZA:
Andaa vizuri chombo chako kwaajili ya kutengenezea sabuni yako kama ndoo au pipa pamoja na kuandaa malighafi zako huku ukizingatia usafi.

Tanguliza kumimina ssulphonic acid vijiko vitano vya chakula kwenye chombo chako. Endelea kuweka soda ash iliyochanganywa na maji vijiko vitatu vya chai.

Weka maji lita tano ukifuatiwa na sless robo lita,chukua pafyum yoyote na uweke kijiko kimoja na nusu cha chai.

Ongeza rangi kijiko kimoja cha chai na uanze kunyunyizia chumvi ambayo huleta uzito na kufanya sabuni yako isiharibike na kukaa muda mrefu.

Koroga vyote kwa pamoja kwa muda wa dakika ishirini na sabuni yako itakuwa tayari.

MAHITAJI NA UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA MICHE

A)MAHITAJI:-
Kostik soda ya unga au ya mabonge
Maji safi
Mafuta ya mise/pamba/nazi/mawese n.k
Rangi ya kutengenezea sabuni za miche(blue/pink/kijani n.k
Marashi upendayo lemon/apple n.k Tanbihi:

Kama unataka kutengeneza sabuni za tiba(virutubisho) utahitaji kuwa na kirutubisho unacho taka kutumia kwa mf:Aloe Vera/Ubuyu/Papai/Mwarobaini n.k Box la kutengenezea sabuni na vibao vya kukatia sabuni vyenye ukubwa wa mche wa sabuni.

Ndoo kubwa za maji angalau 3 na ndoo ndogo 3,conduse ya plastiki kwa ajili ya kukorogea.

Sodium Siliket, magadi soda, Hydrometa nzito pamoja na meza ya kukatia sabuni.

Kanuni:-
kostik kg 1 Maji lita 3 Mafuta lita 6 Sodium siliket grm 500 Magadi soda vijiko vikubwa vya chakula 10 Rangi kijiko 1 cha chakula

Pia utahitaji eneo la kufanyia kazi pamoja na rasilimali watu angalau wawili. Loweka kostik soda kwa masaa 24,

Kisha ikoroge na uipime nguvu yake kwa kutumia hydrometa iwe bomee 25-30bm

Ikiwa imezidi bm 30 haifai kwa matumizi ya binadamu ipunguze nguvu kwa kuongeza maji kiasi na upime tena,

Chukua ndoo ndogo ya maji na uweke mafuta, soda ash,sodium siliket, manukato na uchukue mafuta kidogo uweke kwenye spray (kiasi cha nusu lita) na uchanganye na rangi au virutubisho na ukoroge vizuri

Baada ya kukoroga vizuri changanya na kostik soda koroga tena mpaka ichanganyike vizuri weka nailoni laini kwenye box kuzuia mchanganyo wa sabuni kumwagika (kuvuja)

Anza kupulizia rangi kwenye box na endelea kumimina mkorogo(mchanganyo wa sabuni kidogo kidogo huku ukiendelea kupulizia rangi kwa awamu mpaka mwisho mwisho weka contena la sabuni(box)kwenye sehemu nzuri ambapo ardhi imenyooka na usubiri kwa masaa 24

Bonge la sabuni litakuwa tayari kukatwa na ili sabuni ikauke vizuro anika chini kwenye sakafu lakini tanguliza magazeti na chumba kisiwe chenye kuingiza mwanga wa jua.

VIAMBATA NA NAMNA YA KUTENGENEZA SABUNI YA UNGA

MALIGHAFI
i. Sodash kg 3
ii. Sodium metasaket kg 1
iii. CPP kg 1
iv. Salphonik asid lita 1
V. Optical brighter gm 50
vi. Nausa gm 50
vii. Stivson vijiko viwili vya chakula
viii. Pafyum kijiko kimoja au viwili vya chai
IX. Besen la plastic

JINSI YA KUTENGENEZA
1. Andaa malighafi zote na vipimo vilivyotajwa hapo juu namba moja hadi nane
2. Andaa beseni lako la plastic
3. Andaa mwiko
4. Anza kuchanganya kwa kuweka kimoja baada ya kingine na kuchanganya vizuri
5. Changanya kwa kutumia mwiko wa kujengea
6. Changanya kwa dakika tano hadi ishirini mpaka ichanganyike vizuri
7. Baada ya kuchanganya anika katika kivuli
8. Baada ya kukauka pima na anza kuuza.

Kama hujaelewa waweza kunipigia simu kwa maelezo zaidi kwa simu namba 0743550599 na kwa wale wanaohitaji vitabu vya masomo hayo vipo na vinapatikana kwa njia ya hardcopy na soft copy
Pamoja na vitabu vya ufugaji wa kuku wa kienyeji
MAHITAJI NA MCHAKATO WA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI

MAHITAJI
1. Sulphonic(LABSA)
2. Slec
3. Pafyumu (lemon)
4. Rangi (kijani/ nyekundu/ blue)
5. Chumvi nzuri ya mawe.
6. Glycerin
7. Soda ash light.
8 .Formalin na alka.
9. Maji yaliyokuwa safi .
10. Chombo zaidi ya lita 25.

JINSI YA KUTENGENEZA
1. Chukua sulphonic 1 lita moja weka katika chombo chako cha kutengenezea (lita 25)

2. Kisha chukua slec yako weka katika kile chombo ambacho uliweka sulphonic kisha changanya kwa pamoja.

3. Chukua soda ash nusu kilo kisha iloweke katika maji lita 5 katika chombo kingine pembeni, kisha chukua mchanganyiko wako huo na mimina katika chombo chako chenye mchanganyiko wasulphonic na sles weka maji lita 15 koroga kwa dakika 10 kuwa makini kwasababu utavimba sana.

4. Kisha weka vijiko vya chai 2 mpaka 3 vya rangi kutokana na rangi unayoitaka lakini angalia isizidi sana koroga tena vizuri.

5. Kisha chukua glycerin vijiko 2 vya chai kisha weka katika mchanganyiko wako wa sabuni katika chombo chako na mpaka hapo sabuni itaanza kuonekana.

6. Kisha weka 25ml yani kwa kiasi unachotaka pafyumu (lemon) hii itafanya sabuni yako inukie kwa harufu vizuri.

7. Koroga chumvi ya mawe pembeni kiasi kidogo tu kama vijiko 6 ya chai kisha mimina katika mchanganyiko wako naKisha weka 25ml yani kwa kiasi unachotaka pafyumu (lemon) hii itafanya sabuni yako inukie kwa harufu vizuri

NB: Chumvi ikizidi itafanya sabuni yako kuwa inachelewa kutoa povu kwahiyo kuwa makini sana.

8. Kisha weka alka nusu changanya vizuri na mwisho malizia kwa kuweka formalin kisha koroga tena vizuri (alka na formalin sio lazima sana hata kama hautavitumia sabuni yako itakamilika na itakuwa poa kwa matumizi ).

ANGALIZO
1. Mchanganyiko wako utatoa sabuni lita 25 zikizidi hapo zitakuwa sio nzito kwahiyo kuwa makini.

2. Kuna baadhi ya malighafi ni sumu kwahiyo tumia vifaa vya kujikinga kama Maski na Gloves.
MWONGOZO WA UTENGENEZAJI NA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO

Hongera kwa mawazo mazuri. Iko hivi: gharama sio kubwa inategemea unaanza na production ya ukuwa gani nakushauri anza kidogo kutegemea na soko lako na pia kwakuwa unaanza kutengeneza itakusaidia kwenye improvement mana utakuta ulikosea kitu au ulizidisha materials simply unaweza anza na 50,000.

Materials ni:

Mafuta dumu la 20litre linauzwa 38,000, caustic utachukua ya kupimiwa interm of kg, blue kwa ajili ya kuipa sabuni rangi zile tunaweka kwenye mashati kipindi hicho wahenga hahhahhah zipo feki na og Ila utadadisi, perfume kwa ajili ya harufu kuna za aina tof. Mfano ya lemon ni we we tu hapo harufu isiyokera muhimu, then hydrometer vifaa unatakiwa uandae vifuatavyo jaba au beseni kubwa ya kukorogea na ubao wa kumwagia mkorogo I mean ujiuji hapa inabidi umtafute fundi seremala akudizainie kibao chenye vyumba vya bars kwa idadi yako unayotaka simple 80 to 100 bars inatosha kishkaji.

Udambwiudambi usisahau kachapa kako

Changamoto zipo sana sana soko sasa hivi watengenezaji ni wengi wakubwa kwa wadogo sabuni ni nyingi pia wapo wanaoagiza kigoma direct sababu kule materials ndo nyumbani hivyo bei imedrop na itadrop sana halo mbeleni wako wanaozalisha mzigo wa kujaza canter wengi tu sasa hivi bei maeneo mengi kwa dar ni Tsh. 25,000 kwa katon ya sabuni 20 wewe huko mnapouza 30 elfu ni wapi au kwa mangi dukani na tatizo LA soko ni pale unapozalisha mzigo mkubwa mfano wa kujaza canter so itakulazimu uuze jumla kwa watu wa jumla bei itakuwa chini so itaminya kafaida.

Halafu ujue sabuni za magadi hazitumiki kivile kama za kawaida kina white wash na ndugu yake jamaa matumizi yake ni local limited.

Changamoto nyingine wapo wanaoproduce feki wanaharibu soko hawa watu.

Muhimu ingia YouTube jifunze zaidi then ingia mzigoni tengeneza kwa ajili yako kwanza hata bar moja then angalia ubora na uimprove kabla hujaanza kuuzia watu maana kwenye mix unaweza zidisha au kupunguza vitu sabuni ikatoka zaidi ya jiwe,laini sana,iwe inaisha haraka na mwisho iwe inamuwasha mtu pindi atumiapo.

Mwisho, ujitahidi kwenye kutafuta masoko endelevu maana kuna watu walisarender kwenye hii ishu. Asante
MTAJI, SOKO NA USHINDANI

Mkuu nina uzoefu wa kutengeneza sabuni za miche. Soko lipo kubwa mmno kwani viwanda havikidhi mahitaji ndio sababu bado tuna import sabuni.

Machine ya kutengeneza sabuni - Ploder ni milioni 7, ya kukata chips milioni 1, na clutcher ya kupikia sabuni ni around 3millioni, ila unaweza kuanzia kupika ktk mapipa ya lita200 (siyo kazi rahisi kutumia mapipa) hivyo unahitaji around milioni11 kwa ajili ya equipment.

Tatizo ni Mali Ghafi. mafuta ya kutengeneza sabuni yanatoka nje ya nchi ,hivyo yanaagizwa na viwanda vikubwa, viwanda vidogo wananunua kwa dili kutoka kwa madalali.

Kuna mafuta ya mise yanatoka Mbeya, na kigoma haya ni rahisi ila kama upo dar gharama ya usafiri ni kubwa.

Competitors
Sabuni ya kiwanda kidogo huwa na ubora zaidi ktk maji ya chumvi/kisima ambayo ndio maji yanayotumika na Watanzania wengi,sabuni za viwanda vikubwa huwa zimechujwa sana (highly refined and processed oils) hivyo hazifai ktk maji ya visima.

Watengeneza sabuni za mikono kutoka kigoma huwa wanamwaga sabuni nyingi ktk soko la Dar, wanarudi a month later kuchukua pesa, hivyo jiandae kushindania nao.

Viwanda vikubwa sabuni zao zinapendwa mjini e.g Dar, Arusha na Mwanza ambako kuna maji ya bomba,hivyo tarajia soko la mikoani na vijijini, ili uwafikie hawa wateja inabidi uunde distribution network ya whole sellers, pale manzese kuna maduka ya wapemba ya whole sale ukiwapelekea mzigo wanakulipa hapo hapo, wao huwa wanawauzia watu wanaopeleka bidhaa za maduka mikoani. e.g pruduct yangu nilikuwa siioni madukani in Dar es Salaam. Nilipodadisi nikagundua ipo very popula in Kibaigwa Dodoma. So niki-supply mzigo jamaa wanaotoka Dodoma hawanunui kitu kingine zaidi hiyo sabuni.

Kama utafungua kiwanda mitaani na siyo ktk industrial zone e.g Pugu Road, EPZA jinpange kupambana na TFDA. Bora ya TBS, Afisa biashara, TRA, mwenyekiti wa serikali za mtaa.

Packaging ya product yako ni muhimu sana,ndiyo maana wachina wanauza vitu vyao kwa wingi wao wanajua packaging and presentation nzuri za quality.

Kwa sabuni ya mche ni kutengeneza mabox nenda Pugu Road kiwanda kinaitwa Commercial Printers wao wanabei nzuri na ni wazoefu kwa ajili ya SME s wenye viwanda vidogo watakufanyia design ya box, inabidi uende na miche yako ili wawe na uhakika wa vipimo vya carton.

Kwa ushauri zaidi wa michanganuo ya biashara na faida muone BABALAO atakushauri vizuri zaidi mpaka jinsi ya kupata mkopo)
USHAURI
Kwa kuanza si lazima uwe na mashine. Sio mtalaamu sana ila mzee wangu alizitengeneza sana miaka ya tisini.

Muhimu ni kipimo cha kupimia acid, sikumbuki kinaitwaje.

MAHITAJI

Utahitaji caustic soda ipo ya magunia na ya maji inauzwa kwa pipa.

Unahitaji mafuta hasa ya mbegu zile za michikichi (mise kwa kiha)

Utahitaji pafyumu na rangi, kwetu kigoma tunatumia blue zile za tulizokuwa tunaweka kwenye mashati ya shule

Utahitaji sanduku mfano wa jeneza ambalo baada ya kuchanganya mchanganyo wako vizuri utaumwaga mule na kuacha igande kwa siku moja

Utahitaji nyuzi zile za nylon ambazo utatumia kukata miche yako bado ya kutoa kwa sanduku

Kwa ushauri nenda Kigoma sehemu moja inaitwa sido ukajifunze tena sabuni zitokazo pale ninang'arisha kuliko hata hizo jamaa.

NB: Challenge yako kubwa itakuwa ni kwenye kupata mafuta ya kuchanganyia maana yale ya mise Kigoma ni kugombania na hata yanayofika Dar ni machache sana.

Kuliko ukatoa letsay milion mbili kununua mashine bora utumie hio hela kununua raw material na kujifunza ili baadae ukishakuwa na soko kubwa ununue mashine kubwa za kisasa.

MIMI SIO MJUZI ILA NIMEKUPA IDEA KUTOKANA NA KUKUA KWENYE MAZINGIRA YA UTENGENEZAJI NA WALA SIJAWAHI TENGENEZA
MAHITAJI NA NAMNA YA KUTENGENEZA SHAMPOO

Malighafi na kazi zake
  • Sulphonics acid -inaongeza povu
  • Soda ash-inapunguza acid
  • Sless-hupunguza povu na kun'garisha
  • Perfume-kuleta harufu nzuri
  • Glycerin-kuleta umafuta na ulaini
  • Ghumvi-kuleta uzito na kufanya bidhaa yako iishi kwa muda mrefu
  • Maji
  • Rangi-kuipa muonekano mzuri bidhaa yako
  • Kifaa kama ndoo au pipa
  • Mti au mwiko mkubwa
  • Gloves
  • Buti
  • Kifaa kitakachoziba pua na mdomo

VIPIMO
  • Sulphonic acid vijiko 4 vya chakula
  • Soda ash vijiko 2 vya chakula
  • Maji lita4
  • Sless roho
  • Glycerin vijiko3 vya chakula
  • Rangi kijiko kimoja cha chai
  • Chumvi robo kilo

JINSI YA KUTENGENEZA
  • Andaa Malighafi zako zote na uhakikishe sehemu ni safi
  • Anza na sulphoic acid weka kwenye ndoo /pipa
  • Fuatia soda ash ila kabla haujaweka kwenye ndoo/pipa hakikisha wailoweka kwenye maji kidogo pembeni ikishakua uji ndio umimine kwenye ndoo/pipa
  • Koroga na mwiko au mti vichanganyike
  • Weka maji Lita 4 na ukoroge dk 10
  • Weka glycerine
  • Weka perfume
  • Weka rangi
  • Weka chumvi kwa kunyunyiza kidogo kidogo

Endelea kukoroga hadi bidhaa yako iwe nzito kama uji kwa dk 15.hapo shampoo yako itakua tayari

Waweza ongeza vipimo vya Malighafi kutokana na wingi utakao

Shampoo yako ipo tayari kwa matumizi

Naomba maswali pale ambapo hamjaelewa

Ahsanteni
UTENGENEZAJI WA SABUNI NGUMU

Mkuu mimi sina mtaji, ila kama kuna tenda, tafadhari niajiri(DAR),

Vilevile sabuni zipo za aina nyingi hivyo utengenezaji na malighafi hutofautiana kidogo, kutokana na na aina unayohitaji!

SABUNI NGUMU
Sabuni hii inatumika kuondoa uchafu mgumu

Pima maji vipimo 5 ktk chombo cha plastik kikubwa
ongeza sodium hydroxide kipimo 1
acha mchanganyiko uchanganyike vizuri hadi uanze kupoa.
Ongeza mafuta vipimo 6 kwenye mchanganyiko wako huku ukikoroga bila kukoma hadi dakika 60.

Kabla sabuni haijawa ngumu sana, ongeza vipimo 2 vya kaolin iliyochekechwa vizuri kama kaolini haipatikani unaweza kutumia majivu ya kuni yaliyochekechwa vizuri
mimina sabuni kwenye kifyatulio(plastic) na baada ya kuganda ikate vipande kasha iweke sehemu safi ikauke taratibu hadi ndani ya wiki 12 sabuni itakuwa tayari kutumika.

Vipimo vyote ni kufuatana na idadi ya sabuni unayotaka na chombo unachopimia
Mfano unatumia kipimo cha Lt 1,
Utapima maji lt 5 sodium hydroxid lt 1 vivyohivyo kwa vipimo vikubwa!

TAHADHARI-
Sodium hydroxide {NaOH} ni hatari.
Lazima iwekwe mbali na mahali wanakofikia watoto.

*Kama mtoto atameza sodium hydroxide ni lazima apewe maziwa mengi au kikombe 1 cha mchanganyiko wa juisi ya limau/siki na vikombe 20 vya maji.
*Sodium hydroxide hushambulia ngozi, kuwa mwangalifu kila mara unapotengeneza sabuni, nawa mikono vizuri, hali ya unyevu katika hewa huibadili sodium hydroxide kuwa kimiminika hivyo ni rahisi kudhuru ngozi yako.
*Sodium hydroxide hushambulia aina zote za metali, hivyo tumia vyombo vya mfinyanzi hii itasaidia na kama vyombo vya mfinyanzi havipatikani tumia aina nyingine ya vyombo vya plastiki.
Ni lazima sodium hydroxide {NaOH} ihifadhiwe vizuri kwenye vyombo visivyopitisha hewa.

MAANA YA MANENO
Kaolin ni udongo mweupe wa mfinyanzi unaopatikana mtoni. katika Africa hutumika kupamba kuta za nyumba .
Sodium hydroxide NaOH ni kastiki.
 
Upo wapi? Una mtaji kiasi gani? Je, unataka kutengeneza ya maji au kipande,je ni medicated soap au ya kawaida?

Unatarajia kutengeneza kwa machine au mkono? Miimi nilikuwa na kiwanda cha sabuni, tatizo ni mali ghafi kwa Dar-es-Salaam. Kuna mtaalam wa sabuni anaweza kutengeneza sabuni.
Tafadhali wana JF wenzangu anayewezakunifundisha kutengeneza sabuni naomba tuwasiliane haraka. Nina siko kubwa
 
Tafadhali wana jf wenzangu anayewezakunifundisha kutengeneza sabuni naomba tuwasiliane haraka. Nina siko kubwa

Muzeiya karibu sana katika ukumbi wa ujasiliamali katika nyanja hiyo niko bomba ile mzuri waweza kinipata kwa {safariwafungo@yahoo.com} tuwasiliane tuweze fanya kazi mzee, na kwa wale wenye kutaka ku-invest in manufacturing industry and the like please let work together I have a huge exposure academically and in experience wise!
 
Kutengeneza sabuni ni kupata malighaafi kama Alkali, mafuta, n.k Kama uko serious nitakupa formula zote

Mkuu nakubariana na wewe kwa kiasi fulani, ila kuhusu kumpa mtu formula that is not a good idea, kwasababu hizo malighafi zinautofauti mkubwa wa ubora wake kulingana na source yako kwa wakati huo ni ipi au imehifadhiwa vipi, hii ni kwa uchache tu, kimsingi unapoamua kujikita katika bzness is better product yako ikawa consistence within the market, kwasababu ndicho wanacho hitaji walaji.

Sasa kama kuna variation katika malighafi ni ndoto kuwa na consistence katika product yako. Jamani hizi ni fani za watu hivyo ni vyema zikachukuliwa kwa umakini zaidi. Sasa nini kinatakiwa kufanywa, ni kuwawezesha wajasiliamali wawe nauwezo wa kufanya formula project, cost estimation na vitu kama determination of selling price, sasa kwa yule aliye tayari na mkaribisha tufanye kazi and to experience the difference!
 
Mzee wazo lako tamu sanaaa! Upo mkoa gani? Mi ninaweza kukusaidia katika maswala mawili matatu(capital,sehemu ya kutengenezea, tena ipo mjini kabisa, na maswala ya matangazo) kama soko tayari unalo sio tabu. Kama upo tayari niwe biz partner wako nicheki hapa: Charleschami@yahoo.com.
 
Well, one can search more of such soap making formulas online as well but get to know that these are reactive so be careful during its making process.
 
Mimi ni mtumishi wa uma, nimejaliwa kupata mtaji kidogo, nataka nianzishe kiwanda kidogo cha kutengeneza sabuni. Je, ni vitu gani vinahitajika na soko lipo la bidhaa hiyo? Hapa Tz.
 
Mimi ni mtumishi wa uma, nimejaliwa kupata mtaji kidogo, nataka nianzishe kiwanda kidogo cha kutengeneza sabuni. Je, ni vitu gani vinahitajika na soko lipo la bidhaa hiyo? Hapa TZ
Ndugu Mjasiriamali matarajiwa!

Biashara yeyote ni upatikanaji wa "soko" - yaani wanunuzi. Ni kazi yako kufanya utafiti wa kuwepo kwa "soko". Wengine hawatakusaidia sana. Pili, unataka kutengeneza sabuni ya aina gani? - Kwa maana kulingana na matakwa ya "soko" lako! Sabuni ya maji, unga, manukato (na ya aina gani?) na maswali mengi. Je, unaijua stadi ya utengenezaji sabuni? Kama la.

Soma vitabu, ingia kwenye websites kama - "Instructables" au tembelea watengenezaji sabuni wadogo na wakubwa! Nipigie tafadhali - 0784360034

Nakutakia mafanikio mema.

RA
 
Mimi nataka kujikita ktk utengenezaji wa sabuni za miche na za kuogea ila sina utalaamu, nimesikia sido wanafundisha, pia nataka kujua machine za kutengeza sabuni zinapatikana wapi.
 
Mkuu nina uzoefu wa kutengeneza sabuni za miche. Soko lipo kubwa mmno kwani viwanda havikidhi mahitaji ndio sababu bado tuna import sabuni.

Machine ya kutengeneza sabuni - Ploder ni milioni 7, ya kukata chips milioni 1, na clutcher ya kupikia sabuni ni around 3millioni, ila unaweza kuanzia kupika ktk mapipa ya lita200 (siyo kazi rahisi kutumia mapipa) hivyo unahitaji around milioni11 kwa ajili ya equipment.

Tatizo ni Malighafi. mafuta ya kutengeneza sabuni yanatoka nje ya nchi, hivyo yanaagizwa na viwanda vikubwa, viwanda vidogo wananunua kwa dili kutoka kwa madalali.

Kuna mafuta ya mise yanatoka Mbeya, na Kigoma haya ni rahisi ila kama upo Dar gharama ya usafiri ni kubwa.

Competitors
Sabuni ya kiwanda kidogo huwa na ubora zaidi ktk maji ya chumvi/kisima ambayo ndio maji yanayotumika na Watanzania wengi, sabuni za viwanda vikubwa huwa zimechujwa sana (highly refined and processed oils) hivyo hazifai ktk maji ya visima.

Watengeneza sabuni za mikono kutoka kigoma huwa wanamwaga sabuni nyingi ktk soko la DAr ,wanarudi a month later kuchukua pesa, hivyo jiandae kushindania nao.

Viwanda vikubwa sabuni zao zinapendwa mjini e.g Dar, Arusha na Mwanza ambako kuna maji ya bomba,hivyo tarajia soko la mikoani na vijijini, ili uwafikie hawa wateja inabidi uunde distribution network ya whole sellers, pale manzese kuna maduka ya wapemba ya whole sale ukiwapelekea mzigo wanakulipa hapo hapo, wao huwa wanawauzia watu wanaopeleka bidhaa za maduka mikoani. e.g pruduct yangu nilikuwa siioni madukani in Dar es Salaam. Nilipodadisi nikagundua ipo very popula in Kibaigwa Dodoma. So niki-supply mzigo jamaa wanaotoka Dodoma hawanunui kitu kingine zaidi hiyo sabuni.

Kama utafungua kiwanda mitaani na siyo ktk industrial zone e.g Pugu Road, EPZA jinpange kupambana na TFDA. Bora ya TBS, Afisa biashara, TRA, mwenyekiti wa serikali za mtaa.

Packaging ya product yako ni muhimu sana,ndiyo maana wachina wanauza vitu vyao kwa wingi wao wanajua packaging and presentation nzuri za quality.

Kwa sabuni ya mche ni kutengeneza mabox nenda Pugu Road kiwanda kinaitwa Commercial Printers wao wanabei nzuri na ni wazoefu kwa ajili ya SME s wenye viwanda vidogo watakufanyia design ya box, inabidi uende na miche yako ili wawe na uhakika wa vipimo vya carton.

Kwa ushauri zaidi wa michanganuo ya biashara na faida muone BABALAO atakushauri vizuri zaidi mpaka jinsi ya kupata mkopo. :)
 
Kuna hawa jamaa wa Tanzania Business Creation Company wanatoa semina kwa wajasiriamali wanaotaka kumiliki viwanda vidogo vidogo. Mafunzo wanayotoa ni pamoja na utengenezaji wa:

Sabuni za kufulia na kuogea
Sabuni za maji
Shampoo za kila aina
Dawa za viatu
Bleaching agent
Petrolleam jelly etc.
 
thanks,je hizi semina wanazotoa ni kiasi gani kuattend?
Kuna hawa jamaa wa Tanzania Business Creation Company wanatoa semina kwa wajasiriamali wanaotaka kumiliki viwanda vidogo vidogo. Mafunzo wanayotoa ni pamoja na utengenezaji wa:

Sabuni za kufulia na kuogea
Sabuni za maji
Shampoo za kila aina
Dawa za viatu
Bleaching agent
Petroleum jelly etc.
 
Mkuu dawa za viatu ndo nini? Hawa jamaa ni Waswahili wenzetu au Wachina?

Kuna hawa jamaa wa Tanzania Business Creation Company wanatoa semina kwa wajasiriamali wanaotaka kumiliki viwanda vidogo vidogo. Mafunzo wanayotoa ni pamoja na utengenezaji wa:
Sabuni za kufulia na kuogea
Sabuni za maji
Shampoo za kila aina
Dawa za viatu
Bleaching agent
Petrolleum jelly etc.
 
Mkuu dawa za viatu ndo nini? Hawa jamaa ni waswahili wenzetu au wachina?

Kweli Wachina kiboko. Kumbe kuna mpaka mayai ya Kichina. Watu wamenunua egg chops na kababu zilizotegenezwa na mayai ya kichina pale royal bakery kawe matokeo yake matumbo yamewauma na wameendesha vibaya sana.
 
Mkuu ninauzoefu wa kutengeneza sabuni za mi
che. Soko lipo kubwa mmno.kwani viwanda havikidhi mahitaji ndio sababu bado tuna import sabuni.

Machine ya kutengeneza sabuni -ploder ni milioni7, ya kukata chips milioni1, na clutcher ya kupikia sabuni ni around 3millioni,ila unaweza kuanzia kupika ktk mapipa ya lita200(siyo kazi rahisi kutumia mapipa)
hivyo unahitaji around milioni11 kwa ajili ya equipment.

Tatizo ni mali ghafi. Mafuta ya kutengeneza sabuni yanatoka nje ya nchi ,hivyo yanaagizwa na viwanda vikubwa ,viwanda vidogo wananunua kwa dili kutoka kwa madalali.

Kuna mafuta ya mise yanatoka mbeya,na kigoma haya ni rahisi ila kama upo dar gharama ya usafiri ni kubwa.\

competitors
Sabuni ya kiwanda kidogo huwa na ubora zaidi ktk maji ya chumvi/kisima ambayo ndio maji yanayotumika na watanzania wengi,sabuni za viwanda vikubwa huwa zimechujwa sana(highly refined and processed oils)hivyo hazifai ktk maji ya visima.

Watengeneza sabuni za mikono kutoka kigoma huwa wanamwaga sabuni nyingi ktk soko la dar ,wanarudi a month later kuchukua pesa,hivyo jiandae kushindania nao.

Viwanda vikubwa sabuni zao zinapendwa mjini e.g dar,arusha na mwanza ambako kuna maji ya bomba,hivyo tarajia soko la mikoani na vijijini, ili uwafikie hawa wateja inabidi uunde distribution network ya whole sellers, pale manzese kuna maduka ya wapemba ya whole sale ukiwapelekea mzigo wanakulipa hapo hapo,wao huwa wanawauzia watu wanaopeleka bidhaa za maduka mikoani.e.g pruduct yangu nilikuwa siioni madukani in daresalaam.nilipodadisi nikagundua ipo very popula in kibaigwa dodoma.so nikisupply mzigo jamaa wanaotoka dodoma hawanunui kitu kingene zaidi hiyo sabuni.

Kama utafungua kiwanda mitaani na siyo ktk industrial zone e.g pugu road, epza :)
jinpange kupambana na tfda, bora ya tbs
afisa biashara
tra
mwen
yekiti wa serikali za mtaa.

Packaging ya product yako ni muhimu sana,ndiyo maana wachina wanauza vitu vyao kwa wingi wao wanajua packaging and presentation nzuri za quality.

Kwa sabuni ya mche ni kutengeneza mabox.nenda pugu road kiwanda kinaitwa commercial printers wao wanabei nzuri na ni wazoefu kwa ajili ya sme s wenye viwanda vidogo.watakufanyia design ya box,inabidi uende na miche yako ili wawe na uhakika wa vipimo vya carton.

Kwa ushauri zaidi wa michanganuo ya biashara na faida muone babalao atakushauri vizuri zaidi mpaka jinsi ya kupata mkopo. :)

mkuu new mzalendo umetoa ushauri mzuri sana kwa huyu ndg yetu. Kweli unauzoefu ktk eneo hilo. Big up bro.
 
Mkuu dawa za viatu ndo nini?
Hawa jamaa ni waswahili wenzetu au wachina?

Kaka hiyo no shoe polish. Inavyoelekea ni waswahili wenzetu na ni mradi wa kanisa liitwalo Word Alive Church lililopo Sinza Mori.

Wanauza mtambo wa kutengeneza sabuni za miche unaotoa miche 150 pamoja na mishumaa 500 kwa siku. Pia watakuunganisha na watengenezaji mitambo wa China na kukusaidia kuagiza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom