Msaada: Namna ya Kumhandle Binti Aliyefeli Form Four

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Habari zenu jamani

Matokeo ya Form Four yametoka na kwa Mara Nyingine tena Shule za Kata zimeendelea kuliza Watu! Mdogo wangu yamemkuta, ingawa alikuwa na ndoto nyingi lakini matokeo yake yamekuja kivingine kabisa, sasa nataka leo nikirudi home NENO LANGU LA KWANZA KWAKE LIWEZE KUMPA MOYO KWAMBA HATA WANAOANGUKA HUINUKA NA KUJIFUTA VUMBI NA KUWEZA KUONGOZA MBIO

Sasa natafuta maneno Mazuri ya Kumfariji and knowing tha JF ni Kisima Cha Busara nimeamua kuliweka hapa na linaweza kuwasaidia hata na wengine ambao Leo wamepania kwenda kutoa Lawama kwa ndugu/watoto wao ambao hawakufanya Vizuri
 
Mwambie

1. Ulijitahidi kadri ya uweza wako, mitihani ni kipimo cha uelewa wako katika masomo husika na ku fail hamaanishi wewe hukuelewa au kutokujua kabisa la hasha, ni kwamba jitihada kidogo inahitajika ili mambo yawe sawa wakati mwingine.

2. Wewe una bahati kufika form four, embu waza wangapi wameshindwa kulipa ada na kushindwa hata kufanya mitihani yao na kupata div 4/3? wangapi wagonjwa? etc.....

3. Mwambie unampenda sana uko nae bega kwa bega kuhakikisha kuwa ndoto yake inatimia

4. Toa mfano wa ndg au rafiki unayemjua ambaye alirudia shule mara kadhaa na akafanya vizuri darasani/kimaisha

5. Kubwa kuliko salini pamoja kwa imani ya dini yenu na kunukuu maneno matakatifu yatakayomtia moyo
 
Mwambie kwamba Kufeli katika Mtihani wa masaa wawili mawili Haina maana NDO Kufeli Maisha maana fainali ya maisha ni uzeeni....
Mfano hai ni huu.. MDOGO WANGU ALIPA Divison 3 form 4... hakukata tamaa.. ak..reset mitihani kwenye private school and akaendelea na form 5 na 6 sasa ni mwanasheria na anazipata Ngawila si mchezo.. wenzake aliomaliza na waliopata Divison one wengine pia ni wanasheria na wengine madaktari ... it will take a slight longer to catch up na classmate wake lakini ipo siku wote watakuwa level playing field .. hivyo asikate tamaa...
Anaweza pia kufanya mambo mengine ya maana na akafanikiwa vilevile, kama lengo lake lilikuwa ni kuajiliwa baada ya masomo anaweza kujiajiri kwa kufanya biashara kama akitafuta mtaji sehemu yeyote ile iwe kwa watu binafsi, Mabanki au Saccos...
Ni hayo tu...
 
Mwambie

1. Ulijitahidi kadri ya uweza wako, mitihani ni kipimo cha uelewa wako katika masomo husika na ku fail hamaanishi wewe hukuelewa au kutokujua kabisa la hasha, ni kwamba jitihada kidogo inahitajika ili mambo yawe sawa wakati mwingine.

2. Wewe una bahati kufika form four, embu waza wangapi wameshindwa kulipa ada na kushindwa hata kufanya mitihani yao na kupata div 4/3? wangapi wagonjwa? etc.....

3. Mwambie unampenda sana uko nae bega kwa bega kuhakikisha kuwa ndoto yake inatimia

4. Toa mfano wa ndg au rafiki unayemjua ambaye alirudia shule mara kadhaa na akafanya vizuri darasani/kimaisha

5. Kubwa kuliko salini pamoja kwa imani ya dini yenu na kunukuu maneno matakatifu yatakayomtia moyo

Asante sana Nguli Maana namna walivyofeli tusipotafuta namna ya ku wahandle litakuwa ni Tatizo la Kudumu
 
Mpe mfano wa mama Getrude Mongela, alipigwa mimba akiwa shuleni , lakini hakukata tamaa akasonga mbele, leo ni mtu miongoni mwa watu.
 
Nashukuru sana Kwa Michango yenu yenye Kujenga na Kutia Moyo
 
kumfariji nini bwana...we kamchalaze bakora ili ajue kuwa umechukia...mtu kila siku ulikuwa unamwambia asome yeye anajifanya nyangema...halafu leo amefeli eti ukamfariji...ndio maana tunazidi kulea ujinga. kule china ukifanya ujinga wa hivyo wanakufunga kwenye kamba juu ya mti ili ujutie dhambi yako na siyo kuelezwa maneno matamu kama vile ulichofanya ni cha maana.....
 
Nashukuru sana Kwa Michango yenu yenye Kujenga na Kutia Moyo

haya mambo ya kumbembeleza mtu aliyefeli ndiyo yanasababisha maendeleo yawe nyuma...mtlipa ada mpaka mchanganyikiwe...kila akifeli mnamfaliji...ok. poa tu...
 
Mpeleke vocation kwa ndugu kama wapo...then kama yupo interested na kureseat then mpe go ahead.
 
Suala sio kumfariji bwana. Plan A ishafeli angalia Plan B.
Faraja yake ni kuona utafanya kitu kwa maisha yake. Faraja ya maneno na outing haitoshi.
Ila kama unataka kumpa maneno ya faraja mwambie kuteleza sio kuanguka, yeye ameteleza tu (hapo atajiona hajafeli)
 
Mwambie asivunjike moyo those are set backs ambazo anatakiwa kuzifanyia kazi ili afikie malengo yake.
 
ah ah ah uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiii my libs mie lol,we ni noma:yo::yo::yo:
Mpe mfano wa mama Getrude Mongela, alipigwa mimba akiwa shuleni , lakini hakukata tamaa akasonga mbele, leo ni mtu miongoni mwa watu.
 
haya mambo ya kumbembeleza mtu aliyefeli ndiyo yanasababisha maendeleo yawe nyuma...mtlipa ada mpaka mchanganyikiwe...kila akifeli mnamfaliji...ok. poa tu...
usipo angalia utampoteza huwa ni wakati mgumu sana na pengine alikuwa anafanya vizuri kwenye masoma ila imetokea kwenye mtihani akafeli....
 
Habari zenu jamani

Matokeo ya Form Four yametoka na kwa Mara Nyingine tena Shule za Kata zimeendelea kuliza Watu! Mdogo wangu yamemkuta, ingawa alikuwa na ndoto nyingi lakini matokeo yake yamekuja kivingine kabisa, sasa nataka leo nikirudi home NENO LANGU LA KWANZA KWAKE LIWEZE KUMPA MOYO KWAMBA HATA WANAOANGUKA HUINUKA NA KUJIFUTA VUMBI NA KUWEZA KUONGOZA MBIO

Sasa natafuta maneno Mazuri ya Kumfariji and knowing tha JF ni Kisima Cha Busara nimeamua kuliweka hapa na linaweza kuwasaidia hata na wengine ambao Leo wamepania kwenda kutoa Lawama kwa ndugu/watoto wao ambao hawakufanya Vizuri

Mliwaze kadri utakavyoweza. Inaonyesha huyu alikuwa na bidii sana na shule na pia aliipenda. Kwa ushauri wangu jinyime ili aendelee form five. Wako walioanguka O'Level na wakaenda A'level katika shule za kulipia na kufanya vizuri sana. Kila la heri Mkuu.

Zamani walikuwa wanapelekwa kujifunza kushona siku hizi wanapelekwa kusomea kompyuta ila mie nakushauri kama ana atlist pass 5 C mbili na D 3 aombe kusoma cheti pale CBE akifanya vizuri atachukua diploma kisha anaweza kuja kufanya degree yake siku hizi options nyingi kuliko zamani.
 
Mwache kwanza kama analia alieeeeeeeeeeee mpaka atulie mwenywe, kisha mpe glass moja ya maji baridi anywe hafu kaa naye katika ukimya ukimwangaliaa tu na badae anza kumshauri kuhusu kushindwa mtihani na kushinda maisha. we mtu mzima bwana!
 
There was a Guy called Abraham Lincoln This Gentleman never Quit na hii ndio CV yake

A common list of the failures of Abraham Lincoln (along with a few successes) is:
  • 1831 - Lost his job
  • 1832 - Defeated in run for Illinois State Legislature
  • 1833 - Failed in business
  • 1834 - Elected to Illinois State Legislature (success)
  • 1835 - Sweetheart died
  • 1836 - Had nervous breakdown
  • 1838 - Defeated in run for Illinois House Speaker
  • 1843 - Defeated in run for nomination for U.S. Congress
  • 1846 - Elected to Congress (success)
  • 1848 - Lost re-nomination
  • 1849 - Rejected for land officer position
  • 1854 - Defeated in run for U.S. Senate
  • 1856 - Defeated in run for nomination for Vice President
  • 1858 - Again defeated in run for U.S. Senate
  • 1860 - Elected President (success)
That gentleman later Become ONE OF THE BEST PRESIDENTS OF UNITED STATES
 
Hata mimi nina dada yangu (mdogo wangu) nilimlipia ada kubwa halafu amezungusha. Nilimnunulia vitabu vyote vinavyotakiwa lakini bado amefeli. Nilijaribu sana kumpa counciling na ushauri na mbinu za kusoma. Ila Tatizo la mabint walio wengi ni wavivu kusoma. Alikua akijua ndio narudi home ndipo huingia mezani na kusoma. Akijifungia chumbani anawasha taa, utadhani anasoma kumbe amelala. Sasa mtu kama huyu ukimbembeleza utakua umemsaidia au umefanya nini? Kikubwa ni kutokua mkali kupita kiasi, kwani unaweza kukatisha mtui tamaa na kufanya maamuzi mazito. Siku hizi watu hawaoni tatizio kupiga wanafamilia shoka, kumeza vidonge, sumu n.k. Ila kila Mtu amejaliwa kipaje chake. Mi nitakachomwambia, umefeli, tuliza akili alafu huko baadae useme fani yako ni nini? Ambayo itakuweka busy na kukuingizia kipato
 
Back
Top Bottom