Biashara ya Kuchakata na Kufungasha Unga wa Mahindi (Sembe na Dona)

Wakuu nashukuru sana kwa mwongozo wenu.me nimeona hizi za kibongobongo zinaweza kuwa nzuri sana. Hii mada pia imenionyesha jinsi gani vijana tunapambana kukabiliana na wimbi la ukosefu wa ajira.

Thanx sana.
 
Kutokana na tatizo sugu la umeme siku hizi naona pia vinu vya kutumia mafuta je hizi ghalama yake ikoje wadau?

Asanteni.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mawazo mazuri sana!

Je, hakuna uwezekano wa kuziendesha hizo mashine zote tatu (ya kusaga, kukoboa na kushona mifuko) kwa kutumia umeme wa Solar?

Nikiwa na 20M siwezi kuanzisha mradi huu. Njaa yangu ni kutumia pumba kwa ajili ya kutunza kuku wa kienyeji, ng'ombe na nguruwe (a.k.a Noah).
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mkuu kama alivyosema mkuu gimmy`s kwenye post number 3, mashine nzuri ni za kutengeneza locally ni imara. Nilinunua mashine number 100 SIDO moshi ni imara sana. Niko kwenye biashara hiyo kwa muda sasa.

Mashine nyingi ambazo ni imported has kutoka china au india zina Fan ndogo kwa hiyo zinachelewesha sana kutoa unga as a result unatumia umeme mwingi ambayo ni hasara kwako.
 
kutokana na tatizo sugu la umeme siku hizi naona pia vinu vya kutumia mafuta je hizi ghalama yake ikoje wadau..? asanten

Kinu cha mashine hakichagui, yaani kinu kinaweza zungushwa kwa mota za umeme au kikazungushwa na mashine ya mafuta,naaminisha hakuna kinu kilicho kua special kwa umeme/mafuta. Hapo una namna mbili za kufanya.

1) Ununue engine ya mafuta nashauri tafuta engine ya trekta hasa massey fargason,unaweza nunua hata ambayo imetumika hapa bongo ukaifanyia service vizuri itakusaidia sana kuliko hivi vi engine vyakichina havidumu
2) Jichange ununue generator kama zile wanazotumia kwenye minara ya simu ukatumia pindi umeme unapokatika,hizi generator mpya ni ghali ila fuatilia za mtumba zenyewe zitakua nafuu,kuhusu ukubwa wa generator pata ushauri kwa wataalamu wa umeme.
 
Wadau. Nimeisha anza mchakato wa hiyo kitu kwa maana ya jengo ambayo mi nimeiita phase one sasa ndo najipanga kuezeka.

Phase two ni kununua machines ambazo ni full set kusaga na kukoboa pamoja na mizani mikubwa na midogo na packaging materials bila kusahau mahindi ambayo mdo mtaji.

Phase three ni kuanza kazi.

Naomba muongozo au ushauri kwa ambaye either anafanya au anauzoefu na hii biashara japo kwa reaserch ndogo niliyofanya inalipa na nimeamua kuanza at a medium level scale walau nipate market share kias fulan lakin naona changamoto ni nyingi mf kupata mahindi fake, unga au mahindi kuharibika ama kuoza, n.k nk.

Hizo picha ndo mjengo wa kiwanda na bahati nzuri nina eneo kubwa hapa kwangu so nimeona bora nijenge hapa kupunguza gharama na iwe rahisi kusimamia.

Ntashukuru kwa ushauri.

1406877824718.jpg

1406877851108.jpg

1406877872149.jpg
 
Wakati tunasubiri wataalamu wa hiyo kada, mimi ningependa nikupongeze kwa hiyo hatua uliyofikia. HONGERA SANA.

Katika biashara chache ambazo ni very promosing for the future mart demands ni 'food processing'. There's hopes in this enterprise.

Kuna makala flani nilisoma, huko Mwanza kuna kampuni flani ya kupack na kusambaza unga, ilianza na capital ya almost 1.5M lkn ndani ya miaka mi5 ilikua na turnover ya around 8 bn. Nahisi hiyo kampuni ilikua 1st runner ktk shindano la best mid-sized companies in Tz 2014.

Cha msingi ujue demand ya wateja wako, ujue jinsi gani utaweza kupata resouces za kurun biashara yako non-stop, biashara yako ijitangaze, produce more than the needs of your consumers ili uwe aggresive kupanua biashara yako zaidi na zaidi.

Just a few.
 
Ni nzuri hiyo biashara,unaweza kuongezea na unga wa mihogo mchanganyiko na mahindi, pia unga wa uji ambao wanawake wengi wanapata tabu kuuandaa, kikubwa ni soko, ukipata soko la jumla biashara haina tatizo sana, mahindi nakushauri uchukue kwa wakulima, kuna jamaa mmoja msimu wa mavuno ametenga eneo maalumu la kupokelea mahindi,
yeye habagui, kiasi chochote anapokea hiyo inamsaidia kupata mahindi mazuri.
 
Asante sana Ontario na pia nakubaliana na wewe maana watu lazima tule tu hakuna mbadala na mimi naplan kuwa nasambaza unga wa Dona na Sembe na baadae nafikiria kuanza chakula cha kuku kwa kutumia zile pumba za mahindi yaliyokobolewa.

Bhakresa kaweza kwanin sisi tushindwe?
 
Hii biashara nilishawahi ifanya na mzee wangu ni kazi nzuri ukiwa na capital ya kutosha. changamoto zake kubwa ni upatikanaji wa mahind hasa kuanzia miezi ya kumi na mbili mpaka wa nne.

Faida yake sio ya kutisha ila inalipa sana, nyingine ni umeme hasa kwa maeneo ya Dar ni taab sana hii inakulazimu mara nyingi kazi ifanyike hata usiku, pia site yake ingependeza iwe eneo karibia na transformer ili uwe unapata umeme wa kutosha. Kwenye soko pia mwanzo ni mgogoro sana ila ukishakuwa na jina na hasa ukapata wateja kama wacomoro umepeta.

Kitu kingine ni wanafanyakazi, hapa ndio tatizo inabidi upate wafanyakazi waminifu sana na mara ya mwisho ilikuwa kukoboa na kusaga kwa tonne moja ilikuwa ni 2500, hapo bila kushusha mzigo toka garini. Ukija kwenye upande wa kusagia wateja hapo ni wewe tu ila jua mashine nying unazoziona Dar ni za kusagia wateja na hapa kwang mimi ndo naona inalipa sana.

Mwaka juzi tone moja kusaga na kukoboa ilikuwa ni 30000 na ukiwa na kinu kizuri unaweza futa mzigo wa tonne 30 per 24hrs. ila kuna watu temeke wanatengeneza mashine complete set the last time ilikuwa 70mil na per day inauwezo wa tonne60. Mara ya mwisho nilipopita stereo ilikuwa haijaanza fanya kazi. Kwa ujumla ni kazi nzur sana; nikijikusanya lazima na mimi niiifanye, ila in the hot cake ni unga wa ngano sijui wanafanyaje kina Azam.
 
Mkuu binafsi nafanya hiyo biashara. Wazo la Jawilat ni muhimu sana kama utapata wateja wa jumla ili biashara iende haraka. Pia hakikisha hilo jango lako liko karibu na barabarani ili magari makubwa yaweze kupakua mzigo kiurahi. Kwenye biashara hii pumba ni kama Almasi. Kimsingi ndiyo inayo cover gharama zote za umeme, mifuko na wasagishaji. Kama wakuu walivyosema hapo juu, swala la capital ni muhimu kwa kuwa kuna kipindi mahindi yanaadimika kiasi kwamba unaweza usiende sambamba na mahitaji ya wateja wako. Kumbuka lwa of supply and demand.
 
Asante Concordile 101.

Naona.mwenzangu walau una ABC...

Kwangu navuta three phase maana naanza na vitu vikubwa size 100 ya kusaga na roller tatu ya kukoboa na nimejenga nyumba pia ya wafanyakazi of which wataishi pale pale na huo mlango mkubwa wa kiwanda uko sambamba na dirisha la masterbed room hahaha lakin nafikiria kuweka security camera maana always labour ndo changamoto kubwa. Nina store inaweza kuchukua hata gunia 500 za mahindi ila nafikiri inabidi kuyatreat. Ntaomba mwongozo wako mkuu hasa kuepuka mahindi kuoza na unga kupata fungus maana nataka nianze na stock ya walau ton tatu. Pia sijui napata wapi mifuko na lebeling zake na je nilazima usajiri TBS na TFDA?
 
Asante Lutifya.

Ya nashukuru niko barabaran.


Unamaana ni focus zaid kwenye sembe ili nipate pumba sio? Kwa maana dona iwe kidogo kuliko sembe kama nimekupata vizuri.

Concordile na Lutifya vp muko dar? Naomba niwatafute munisaidie maana hata machine nilipita pale Kishen Enterprises na ndo nafikiria kuchukua pale ila mpaka sasa sijapata mzani mkubwa na hata positioning ya hizo machine ni muhimu pia.

Na munafanyaje kuepuka mahindi au unga kutopata fungus? Na pia kupata mahindi bora maana nimesikia aina nyingine haifai
 
Mzee Ngongoseke Shikamoo na hongera sana maana ume focus kwenye kilimo...nami niko njiani mkuu ila ndo nataka nianze na hii ndogo kwanza. Asante kunipa moyo pia.
 
Back
Top Bottom