msaada, muongozo wa kimawazo

chipegwa

Member
Nov 2, 2010
8
1
Habari zenu wana jf, naombeni msaada wenu wa kimawazo katika hili. mimi ni mjasiriamali nina stationery nimepanga sehemu ambayo ina nyumba kubwa ndani. kutokana na ukubwa wa nyumba na wingi wa wapangaji kukatokea mgogoro kwenye ununuaji luku ila kwa kuwa mimi mfanyabiasha inabidi niwe na umeme kwa hiyo kila unapotokea mgogoro muathirika wa kwanza ni mimi. Nikaongea na mwenye nyumba ili niweke luku ya peke yangu akaliafiki hilo swala, nkaandika barua ya luku separation, nkapeleka tanesco hapo ndipo matatizo yalipoanza, siku ya kwanza wakaipokea nkaambiwa niende kesho yake kufatilia majibu, kufika wakaanza kunambia barua umekosea kuandika nkaomba muongozo skupewa nkaambiwa niende kesho yake nlipoenda nkapewa saveya akakague eneo akajionea hali halisi then akanambia niende kesho yake nkaenda kufika akanambia umekosea kuandika barua ila kwa jinsi hali ilivyo pale kwako unatakiwa kupata luku, kuna dada alikuwa kakaa pembeni akamwambia basi swala ni dogo apewe muongozo wa kuandika barua upya mumpe luku, huyo anaeidhinisha akasema mi skuwepo wakati barua inaandikwa na wala sina ushahidi kama mwenye nyumba karidhia luku kuwekwa na (wakati yeye ndo alipokea barua cku ya kwanza nikaomba muongozo wake hakusema kitu) kukawa hakuna suluhisho. Je mpaka hapo nlipofikia nifanyeje ukizingatia mimi ni mjamzito na kuzunguka nenda rudi siwezi kwa sasa. NAOMBENI MSAADA
 
Back
Top Bottom