Msaada. Mtu nisiemfahamu kadeposit fedha kwenye akaunt yangu

Mr Suggestion

JF-Expert Member
May 2, 2011
605
308
Wadau nina akaunt katika benki moja hapa jijini Dar sasa kumekuwa na mchezo wa mtu kudeposit fedha kwenye account yangu pasipo mimi kumfahamu mtu huyo. Mara ya kwanza aliweka kama milioni 27, nilipoipata meseji nikamtafuta meneja wa benki nikamwelezea akadai fedha zimewekwa kwa local check, baadae zikawa zimetolewa lakini kwa mfumo wa kuzitransfer kwenye akaunt nyingine. wiki hii wameingiza kama milioni 15 hivi sasa nashindwa kuelewa nifanyeje kwani akaunti hiyo ni ya kibiashara, sheria zikoje hapo endapo nikichukuwa mzigo huo bila kumwona meneja
Nawasilisha wakuu
 
Nenda kazichukue fasta uhamishie kwenye akaunti nyingine na ufunge hiyo akaunti. Next time watahamisha na zako (Kama unazo, lol)!
 
unatafuta kufungwa tu wewe,hiyo account yako ni njia ya kupitiahia hela za wizi kama vp ongea na meneja mkatie kidogo la sivyo ukichua kimyakimya utajikuta segedansi. Nitarudi baadae
 
Wanapozitoa wanazi transfer kwa njia gani? Kwa idhini ya nani? Kuna nani mwingine mwenye dhamana ya akaunti hii?
 
Inawezekana ndiyo yale mambo ya money laundering yaani kutakatisha fedha haramu. Ni vizuri utoe taarifa na polisi/Takukuru ili usije kuhusishwa na huo mchezo kwani ikichukuliwa bank statement yako kama ushahidi unaweza kujishtukia unafikishwa Mahakamani kwa kosa lisilokuhusu pale itakapobainika kuna mchezo mchafu.
 
Anti-money Laundering kuna kitengo bank kinaitwa risk management hapo kuna chezo linapigwa hapo hela za kupigwa hizo na maofisa wa benki,ongea nao wakupe hata mil5 la sivyo kawalipoti na message usizivute kwani ushahidi pili print haraka mini-statement ili uwakamate vizuri cheza na apportunity hiyo usilaze damu ingekuwa mimi hapo sikosi mil5
 
Mkuu tupo wawili kwenye hiyo biashara tupo wawili na uwezo wetu si wa milioni hizo 27, so jamaa walizitransfer kwenda akaunti nyingine lakini vijisenti vyetu walituachia
 
Hapo kuna mtu anataka kujenda ushahidi wa kua anakutumia hela. Baadae utafunguliwa mashtaka ya money laundry au corruption!
Hakikisha una record ya pesa hizo zinako enda (ili uoneshe kua hukuzitumia) na kama utaweza jaribu kuzi trace zinatokea wapi.
 
Nikawaripot vipi mkuu, kwani nimekuwa nikimfuata meneja several times lakini ananizingua mara nitashugulikia mara njoo kesho. mimi nikizani labda competitor wangu kibiashara wananichezea chezo ili mwisho wa mwaka nionekane nimefanya biashara nzuri ili TRA wanikamue vilivyo
 
Very simple. Omba bank statement then hizo transaction utaziona zooooote. Na kwa kukushauri, muone mwanasheria manake hainiingii akilini mtu anawezaje kutransfer hela toka kwenye account yako bila consent yako.
 
Deposit yake inafanywa kwa local check so ni ngumu kujua zinatokea wapi MWALI. Hata mimi nashindwa kuelewa kwa nini mzigo huo aniwekee mimi tu au na meneja nae anahusika katika mchezo huo.
 
Inawezekana kuwa kulikuwa na makosa wakati wanapost hizo entries na wakacredit account yako kwa makosa ; wakigundua makosa yao huwa wanareverse hizo entries na wewe ndio unafikiri wame transfer to another account!!
 
Hili suala ni nyeti saana, hasa yategemea wewe ni nani... Wafanya kazi gani yenye majukumu yepi. Sio bure kua pesa iingizwe kwenye a/c then iwe transfered tena bila idhini yako; you have the right to get worried na kulifuatilia hili jambo kwa undani. Ushauri epuka tu ile tamaa ya kusema uzichukue na uzitumie... zaweza leta shida kubwa saana in the long run.
 
Ni kweli hao wanawachezea mchezo wa kusafisha fedha. Muandikie Meneja barua na uhakikishe umemueleza kwamba ikitokea tena kwa mara ya tatu basi utalazimika kuripoti TAKUKURU na taasisi nyengine za fedha. Na utaandika kwenye magazeti na kutoa vielelezo vyote.

Kama wanakuchezea mchezo basi wataogopa kwani reputation ya bank itaharibika.

Tafadhali ni PM nijue ni bank gani hiyo. Kama ni ile ninayoweka vijisenti vyangu nikaviangalie vizuri.
 
Thanks Asha ndio maana nimekuja kutaka ushauri kwenu kwani nahofia sana kwani mambo ya kusimama mahakamani si mchezo, tena katika ulimwengu huu wa sasa.
 
Ningelikuwa ni miye mbona ningezitumbua mpk chuo wangentambua ..ingekuwa a vivid example ya from rags to riches.!
 
No mkuu mwanzo ilitokea kwa hiyo 27m, nikaifuatilia kwa takriban wiki moja, na sasa imetokea kwa hiyo 15M. Je ni kwanini makosa kama hayo yafenyike kwenye akaunti hiyo hiyo, kwanini asitumie akaunti yangu binafsi
 
kaka nami nafikiria hivyo lakini jua kwamba particular zetu zipo pale benki so sioni hiyo kimya kimya itakuwaje na mambo ya security system ya benki itakuwaje?
 
Back
Top Bottom