Msaada: Mtoto hakui tangu azaliwe na hana dalili ya kubadilika

maskio popo

Senior Member
Sep 3, 2015
158
31
habar zenu ndg: kuna dada wa rafiki yangu ana mtoto amempata tangu mwezi wa 6 lakini mpaka leo mtoto huyo bado ni mchanga sana kama kazaliwa siku 5 zilizo pita amekuwa anasumbuka sana amejaribu kwenda hospital ya wilaya ya urambo wakampa majibu ya kuwa mtoto hana tatizo nimekuja hapa ili nipate ushauri wa kitaalam juu ya mtoto huyu. alizaliwa akiwa na uzito kilo 2 na glam 2 lakini mpaka leo miezi 5 ameongezeka glam 4 tu tafadhari tumsaidie huyu dada kwani ametengwa hadi mtu aliye mzalisha amebaki kulia na hana majibu juu ya mtoto wake. hana pesa ya matibabu lakini mimi nijitolea kumpa tsh 100.000 kama kwa ajili huduma ya mtoto wataalamu wa magonjwa ya watoto tafadhar tusaidieni tatizo hili. mwenyezi mungu awape busara na hekima katika michango ya mawazo na utaalamu wenu. NAWASILISHA
 
Mwenye majibu ya huu ugonjwa atupe suluhisho, kwani nami nina ndugu yangu anamtoto hakui wala haongezeki uzito.
Ana miezi zaidi ya saba hajaanza kuota meno wala kukaa.
 
vipi shingo yake imekaza?
je anafanya matendo mengine kama kucheka ,kushika vitu n.k
je ukimtazama unaona ulemavu wowote dhahiri/waziwazi kabla ya vipimo?
 
Shingo haijakaza, ila ngozi ya mwili mzima ka ya kizee ivi.
Matendo mengine anafanya, na ukimwita anageuka, kucheka etc. Ila tu ni hakui kamwili kadogo sana.
Ukimwangilia ghafla utastuka kwa jinsi anavyotazamika, aliugua mda mrefu alipozaliwa. Ila sa ivi haumwi kabisa.
 
habar zenu ndg: kuna dada wa rafiki yangu ana mtoto amempata tangu mwezi wa 6 lakini mpaka leo mtoto huyo bado ni mchanga sana kama kazaliwa siku 5 zilizo pita amekuwa anasumbuka sana amejaribu kwenda hospital ya wilaya ya urambo wakampa majibu ya kuwa mtoto hana tatizo nimekuja hapa ili nipate ushauri wa kitaalam juu ya mtoto huyu. alizaliwa akiwa na uzito kilo 2 na glam 2 lakini mpaka leo miezi 5 ameongezeka glam 4 tu tafadhari tumsaidie huyu dada kwani ametengwa hadi mtu aliye mzalisha amebaki kulia na hana majibu juu ya mtoto wake. hana pesa ya matibabu lakini mimi nijitolea kumpa tsh 100.000 kama kwa ajili huduma ya mtoto wataalamu wa magonjwa ya watoto tafadhar tusaidieni tatizo hili. mwenyezi mungu awape busara na hekima katika michango ya mawazo na utaalamu wenu. NAWASILISHA
Kuna mtoto wa mdogo wa rafiki nadhani alikuwa na tatizo la kutokukua ila walienda kariakoo kuna Dr. Mmoja wa magonjwa ya watoto nadhani anaweza kujua nini tatizo kama sio kutibu moja kwa moja, ila shida kubwa mahari alipo mtoto au mulipo ninyi tabora na Dar ndio labda inaweza kuwashida
 
Naomba Namba ya huyo dr au Jina la hospitali plse.
 
poleni wote! Ushauri fika hosp kcmc mtafute dr wawatoto! naiman hilo tatizo litaisha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom