Msaada! Msaada !msaada.

kazi2000

Member
Jan 1, 2012
71
14
Nimatumaini yangu kuwa wote hamjambo na mnaendelea vizuri na majukumu yenu ya kila siku.ndg zangu naomba msaada kwa yeyote mwenye ufahamu juu ya hili anisaidie.wapendwa nina ndugu yangu ana umri kati ya 15,16 au 17,anaitwa shida,ambaye alichukuliwa kijijini ikola wilaya ya sumbawanga vijijini mkoa wa rukwa,na kuletwa mjini tabora kwa minajili ya kufanya kazi za ndani ,yaani house girl.kweli alianza kufanya kazi kwa takriban mwaka 1,ila ilipofika mwanzon mwa mwezi wa 6 nilipigiwa simu toka huko kijijini kwamba binti ametoroka nyumbani yaani tabora na ameelekea dar .nilifanya juhud juu ya hilo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa polis ila mpaka sasa bado sijampata.ila leo nimesikia katika uchambuzi wa magazeti kukiwa na habari inasema ,binti toka sumbawanga atelekezwa dar na mumewe..naomba msaada wa kujua hiyo habari au hata jina la gazeti maana mi niko singda vijijin.
 
Samahani! Ilikuwaje mkamruhusu kwenda kufanya kazi za ndani? Jamani tusipende kuwaachia mabinti kwenda mijini kwenye kazi za ndani kwani huwa ni hatari sana! Wanateswa,wengine wanadhulumiwa na kufukuzwa wasijue cha kufanya,wengine wanabakwa na watu wa hapo anapofanyia kazi,wengine wanauzwa ili wabakwe! Jamani,hata kama ni umaskini tuvumilie tu kwetu badala ya kuwaacha dada zetu wakaenda kukaa tusikojua.
 
ndugu yangu aliyemchukua alitumia nafasi aliyokuwa nayo ya kufamiana na wazazi wa huyo binti.hata mim baada ya kuambiwa nilisikitika sana lakin ndo hivyo sikuwa na nguvu yeyote ya kuzuia jambo hilo lisifanyike.
 
mimi ninapoishi kuna kabinti kadogo sana kanafanya kazi zan dani kwa jamaa. inakera sana ila nashindwa cha kufanya kwani najua future ya hako katoto itaishia pabaya. kabinti kana miaka kati ya 14 na 16 sasa najiuliza shule inakuaje? hivi vitendo ni vya kupigwa vita ndani na nje. ila wewe ili usaidiwe kirahisi weka picha kwani hawa watoto huwa wanabadilishwa hadi majina.
 
Mara nyingi Mahausigeli huwa wanakuwa Mabaamedi, waki-advance utawakuta Jolly Club sokoni. M-trace bar zote town.
 
Back
Top Bottom