Msaada: mikopo midogo midogo/kukuza mtaji

Kapuku83

Senior Member
Sep 8, 2012
146
35
Wadau habari,nilikua naomba msaada wenu jinsi ya kuweza kupata mikopo midogo midogo ambayo ina masharti nafuu kwa ajili ya biashara hasa ya kilimo,chakula na ufugaji!mimi ni kijana niliegraduate miaka minne iliyopita,na nimekata tamaha na kupata ajira,hivyo nimedhamiria kujiajiri/kua mjasiriamali!nataka nitumie mkopo huo kama mtaji wa kuanzishia biashara,ila kikwazo kwangu ni dhamana,maana sina nyumba wala kiwanja,nina pori tu la heka mbili lililopo maeneo ya Mikese Morogoro ambalo nina hati za kimila!nataka pori ilo liwe ndio mkombozi wangu kiajira!naombeni ushauri wenu wadau!
 
Mkuu ebu jaribu kucheck na Tanzania investment bank,nasikia wana masharti nafuu sana japo sina uhakika
 
NI kweli TIB waba riba ndogo(4%pa) lakini sio masharti nafuu

Mkuu labda ungesaidia kuahainisha baadhi ya masharti yao angalau wengine tupate mwanga zaidi wapi pa kuanzia,mfano kwa wasio na nyumba wala kiwanja ila wenye shamba au pori wanaweza pata mkopo kweli?
 
Wadau habari,nilikua naomba msaada wenu jinsi ya kuweza kupata mikopo midogo midogo ambayo ina masharti nafuu kwa ajili ya biashara hasa ya kilimo,chakula na ufugaji!mimi ni kijana niliegraduate miaka minne iliyopita,na nimekata tamaha na kupata ajira,hivyo nimedhamiria kujiajiri/kua mjasiriamali!nataka nitumie mkopo huo kama mtaji wa kuanzishia biashara,ila kikwazo kwangu ni dhamana,maana sina nyumba wala kiwanja,nina pori tu la heka mbili lililopo maeneo ya Mikese Morogoro ambalo nina hati za kimila!nataka pori ilo liwe ndio mkombozi wangu kiajira!naombeni ushauri wenu wadau!

Kama una heka 2 mkopo wa nani na mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe? Chukua jembe ingia shamba. Kama eneo lina maji lima mchicha, bilinganya na kunde. Simamia mwenyewe. mchicha ndani ya wiki mbili unavuna. Mikese ni mjini ati unaweza uza. Achana na mitaji. Ila pia sikukatazi. Nenda Pride na Finca hapo Morogoro. Ila pia nenda PASS wanatoa mikopo kupitia CRDB. Ila kwa shamba lako huhitaji mkopo. Unahitaji jembe.
 
Back
Top Bottom