Msaada - mikataba ya kazi

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,631
1,926
Salamu wakuu wa jukwaa hili.

Naomba ushauri kwa jambo lililotokea. Ndugu yangu aliingia mkataba wa kusupply vifaa kwenye taasisi moja ya serikali.
Wakati wa utekelezaji wa mkataba huo kukajitokeza mizengwe kwamba aliyesaini mkataba kwa niaba ya taasisi hiyo hakuwa na mamlaka kisheria kwa sababu mkataba wake wa kazi ulikuwa umekwisha. Jambo hili limeleta msuguano mkubwa hasa kwenye kulipwa fedha zake. Katika kuuliza details tukaambiwa eti aliyesaini mkataba alikuwa ana ajira ya mkataba ambapo uliisha na haukuwa umehuishwa (Renewed) japokuwa mhusika alikuwa ofisini bado.

Wakuu tusaidieni maana ya hili jambo kisheria. Mtu yuko ofisini bila mkataba halafu anasaini mikataba na makubaliano mengine kwa niaba ya taasisi then tunaambiwa mikataba hiyo haikuwa halali. Sisi tutajuaje hayo ya ndani kwao? Ni kitu gani kinapaswa kufanywa kurekebisha hali hiyo?
 
Pole na mkasa uliokupata, Waandikie taarifa ya madai(demand notice) wape siku 21 au 30 wakulipe hizo pesa unazodai, then muda huo uliowapa ukiisha na hakuna kilichofanyika basi kafungue shauri mahakamani ukiomba kulipwa kiasi cha pesa halisi ulichokuwa ukidai pamoja na fidia zingine.
Hayo ya mtu kusaini mkataba kama hakuwa mfanyakazi au alikuwa mfanyakazi wakayaseme huko(kortini) inawezekana ni self defence tu wanatumia.
Haki itapatikana mahakamani, ikiwezekana tafuta mwanasheria akusaidie kudraft hizo document kwa lugha nzuri ya kisheria.
 
Back
Top Bottom