Msaada mdada nina m5 naomba soma maelezo unipe ushauri wa biashara

ngarambe

Senior Member
Apr 15, 2012
100
14
Mimi ni mdada wa miaka 26 niko rombo kilimanjaro elimu yangu ni form six,nilikua nimeajiriwa na campuni moja jijini dar es salaam ila kutokana na matatizo ya kazini nimeacha kazi.kwa sasa niko home kilimanjaro wilaya ya rombo- mashati. Nimewaza nifanye biashara gani sipati jibu. Kati ya dar na rombo na sehemu zote nina sehemu ya kukaa bila kulipa kodi. Nisaidie tafadhali
 
kote umekaa, pima na uone wapi utaweza kufanya kazi ya kibiashara ukafanikiwa
 
Umenikumbusha kuna jirani yangu alilete vitu aina hiyo ya kuharibika fuso ikaharibikia njiani mtaji wote ukakata,,,,

ngarambe .... biashara hauamki ukakurupuka ukapeleka mzigo pale ilala au kariakoo hivi hivi ..... nenda pale utapewa na madalali aina ya kiazi na bei ... muhakikishie dalaliutaleta mzigo halafu chukuacontacts zake.... rudi rombo ...go to the groundna angalia wakulima wanauzaje ..... piga mahesabu yako including transportation .... ukiona kunafaida mpigie simu mwambie nakujana gunia kadhaa .... atakusubiri .... ukifika tuu unakaapembeni all ex-works ni za kwake ... baada ya masaa matatu unakwendakuchukua pesa

fuso ikiharibika dalai anauwezo wa kuwasiliananawewe mkafaulisha mzigo kwenye fusonyingine ... yaani fuso inaharibika na wewe unasubiri ipone ... shhit ... huyo si mfanyabiashara

huyo jirani yako alitaka kufanya biashara kimimi mimi ndiyo maana ikalakwake

okay
 
ngarambe .... biashara hauamki ukakurupuka ukapeleka mzigo pale ilala au kariakoo hivi hivi ..... nenda pale utapewa na madalali aina ya kiazi na bei ... muhakikishie dalaliutaleta mzigo halafu chukuacontacts zake.... rudi rombo ...go to the groundna angalia wakulima wanauzaje ..... piga mahesabu yako including transportation .... ukiona kunafaida mpigie simu mwambie nakujana gunia kadhaa .... atakusubiri .... ukifika tuu unakaapembeni all ex-works ni za kwake ... baada ya masaa matatu unakwendakuchukua pesa

fuso ikiharibika dalai anauwezo wa kuwasiliananawewe mkafaulisha mzigo kwenye fusonyingine ... yaani fuso inaharibika na wewe unasubiri ipone ... shhit ... huyo si mfanyabiashara

huyo jirani yako alitaka kufanya biashara kimimi mimi ndiyo maana ikalakwake

okay

LAT shukrani sana kuna mambo uninifungua macho,,,,, nashukuru sana kwa ushauri wako
 
Dada hizo Pesa ni nyingi sana na zinatosha kufanya Biashara kubwa tu,Ila cha kufanya kaa chini orozesha ni vitu gan unavipenda maishani mwako au ndoto zako ni kufanya kitu gani? theni unaweza fanya mchanganuo na kuja na aidea nzuri sana,

Unatakiwa wewe ukae uumize kichwa na kuja na wazo lako, na wazo lako ndo bora zaidi, so wewe fanya hivyo na i hope utakuja na aidea nzuri sana,

Na kwa kila wazo jaribu kufanya some research, ni bora ukaingia ghalama kufanya research kidogo kuliko kuto kufanya, fanya utafiti

Na kuna sector nyingi tu unaweza cheki

1. Agriculture and food processing

2. Tourism

3. Education industry

4. Comnication industry

Na zingine nyingi tu, ila fanya research and come up with good aidea ambayo itakuwa ni sustainable na usitafute aidea ya biashara za kufanya kwa msimu,
 
Nafikiri biashara inatokana na fursa zinazopatikana mahali fulani; jaribu kuangalia maeneo yote unayoweza kuishi kuna mahitaji gani?. Mbona mahitaji ni mengi yanatuzunguka, soma kitabu cha ACRES OF DIAMOND; fursa ya kibiashara iko hapo hapo ulipo sasa, ndio maana Nyerere alisema UCHUMI TUNAUKALIA, yaani bado watu wanatatizo la kupambanua fursa, halafu usiwe mvivu wa kufikiri...!!!, hata ukiambiwa biashara gani ni nzuri hutaweza kuendeleza kwa sababu ya uvivu wa kufikiri.
 
Ngarambe, hongera sana kwa kuwa na mtaji, kwasababu wenzio mawazo ya biashara wanayo lakini mtaji ndio tatizo. Na ninafikiri swala la mtaji vijana wengi wanalitafakari kama kitu kigumu sana kukipata lakin wewe upande huo umeshinda. Mim ninayo machache ya kukueleza katika uanzishaji wa biashara.

Usikurupuke sana, tuliza akili yako kabisa.Kisha angalia wewe unauzoefu na biashara gania? au nisema wewe unapenda biashara gani? Ukisha pata jibu angalia je uwezekano wa kupata bidhaa utakazo uza kwenye hiyo biashara upo? na kama upo soko lake je?

ukisha yajua yote hayo, basi kaachini angalia utatumia sh ngapi katika kuanzisha manake usijeukaanza na biashara ambayo itatumia mtaji wote siku ya kwanza. anza msingi ambao utakubakizia kiasi fulani ambacho kitakuwa kama dhamana yako.

naogopa sana kukwambia fanya biashara fulani lakini naona kwakuwa wewe umeishi dar na sasa uko rombo. fikiria biashara ambayo itakupa uwanja mpana wa kujifunza zaidi mathalani unaweza kuwa unakuja dar unanunua rasta za jumla kkoo unapeleka rombo unauza kwa bei ya jumla. wakati unafanya hayo utakuta kuwa siyo rasta tu hata weaving watu wa huko wanapenda sana unaongeza. istoshe wakati unakuja kutoka rombo utagundua kuwa dar wanapenda maparachchi ya rombo basi unatafuta hata gunia mbili unakuja nazo lakini hapa inabidi uongee na dalali kama ulivyoshauriwa na LAT.

wakati unafanya haya utagundua pia labda english gold huko watu wanazipenda sana sasa wewe unaongezea na hizi unaenda nazo na hizi unatafuta marafiki waalim na manesi unakuwa unawauzia. Usianze biashara ya kuwa na frem kwanza itakugharimu kwa maoni yangu kwani kodi za frem na process za usajili zitakata kama 1mil ya huo mtaji wako.

pia ukiwa unafanya hivi utaendelea kupanua mawazo kidogokidogo wakati unakuza mtaji. naamin nimekuelezea kwa kiasi cha kuelewa mengine utaambiwa na wachangiaji wengine.
 
Jaribu kuuangalia kati ya dar na huko kwenye mlima wetu,biashara gani inalipa na soko lake lipo vipi,pia usiwekeze kiasi chote kwenye biashara moja au kuwekeza kiasi chote katika biashara ambayo utakua umeiona inalipa,bali wekeza kidogo alafu sikilizia faida yake kama nzuri endelea nayo kama mbaya ipotezee...hapo utakua umeepuka na kitu kinaitwa "risk of putting all eggs in one basket"....gudluky
 
Asanteni sana Maphie, Komandoo, Hakuna aka Hakunaga!, GFsonwin, joshcommy,,,,, nashukuru sana ushauri wenu, joshcommy nimependa hiyo "risk of putting all eggs in one basket" thanks much..... Hakuna ungenisaidia hicho kitabu ntapata wapi,,, nitakitafuta soon mkuu wng,, komandoo umenipa na sdector tofauti tofauti,,respect kwako mpendwa, LAT umenifurahisha kutoka rasta mpaka maparachichi,,, asante sana,,,,,, one love,,,
 
Asanteni sana Maphie, Komandoo, Hakuna aka Hakunaga!, GFsonwin, joshcommy,,,,, nashukuru sana ushauri wenu, joshcommy nimependa hiyo "risk of putting all eggs in one basket" thanks much..... Hakuna ungenisaidia hicho kitabu ntapata wapi,,, nitakitafuta soon mkuu wng,, komandoo umenipa na sdector tofauti tofauti,,respect kwako mpendwa, LAT umenifurahisha kutoka rasta mpaka maparachichi,,, asante sana,,,,,, one love,,, nasubiria maoni ya wengine tafadhali
 
Ngarambe,
It is my opinion the e money (mpesa, tigo pesa, airtelmoney & Zpesa) may be good business for you. if that is ideal DSM is suitable. So it's your turn to make a best choice among the advices given by JF members. Adios
 
Ngarambe, It is my opinion the e money (mpesa, tigo pesa, airtelmoney & Zpesa) may be good business for you. if that is ideal DSM is suitable. So it's your turn to make a best choice among the advices given by JF members. Adios
dada yangu kama hayo maeneo yanaumeme jaribu na electronics zinalipa sana
 
Back
Top Bottom