Msaada: Kwa wale wataalamu wa mambo ya picha na camera

tisa desemba

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
434
114
Wadau, mimi ni mwalimu wa cheti (grade IIIA) niliyehitimu june mwaka jana, kama mjuavyo mpaka sasa hatujui ni lini tutapata ajira za serikali.
kutokana na ukata, nimeamua kuwa mpiga picha (camera man) hapa kijijini nanjilinji, katika pitapita zangu za kusaka wateja nimekutana na hili tangazo la kupiga picha za passport za watahiniwa kidato cha IV 2012, kusema kweli vigezo vyote natimiza ili niweze kupewa hii dili na mwl mkuu ukizingatia mimi ni ex-student wa hapa, ila katika hili tangazo sehemu ya namba 1 (b) (c) na (d) inanitatiza nashindwa kuelewa kama inapatikana kwene setting za camera au kwenye computer wakati wa kuprint....

SAM_8472.JPG

naombeni msaada kwa wanaojua mambo ya pixel na resolution
 
Chukua tenda, hiyo pixel unakuja ku-resize kwenye computer
 
Usiogope chukua tenda fasta hayo yote unasett kuna program kibao za photo editing pixel yeyote unapata chukua chukua wewe,ulimwengu wa TEHAMA hakuna kinachoshindikana hata muhuli wa ikulu unapata
 
Kama unatumia digital camera unaweza ukaset kwenye camera, sema sijui kama kuna camera yenye resolution ndogo hivyo. Hata hivyo hakiharibiki kitu, kama wachangiaji wa mwanzo walivyosema unaweza ukarekebisha baada ya kupiga. Kwahiyo chukua kazi hiyo. . . .
 
nashukuru wadau wote kwa ushauri wenu! nakamata tenda then baadaye nitazitafuta hizo program za ku re-size pixel na resolution.
 
nashukuru wadau wote kwa ushauri wenu! nakamata tenda then baadaye nitazitafuta hizo program za ku re-size pixel na resolution.

Camera yoyote ya digital haina tabu kurudisha chini pixel!! ila kupandisha ndio ina limit!! na kwa kazi hiyo unaweza pata digital camera inayofanya kila kitu bila ya wewe kuhangaika na makompyuta! Kwa mfano Canon Digital unaiprogram kabisa kwenye camera yenyewe na ikipiga inapiga passport size! that means inazitoa nne kabisa kwenye screen! Kazi kwako
 
Aisee bigup kwakuchukua uamuzi wa kutafuta kazi mbadala.
Life is not a straight line.
Kila la kheri
 
Back
Top Bottom