Msaada kwa mkaka

chetuntu

R I P
Jan 10, 2011
949
109
Hamjambo wapendwa, hope wote mmeamka bien, kwa wagonjwa na matatizo mbalimbali poleni. Leo nimepata kisa kimenitatiza kidogo naomba kushare nanyi wapendwa tumsaidie huyu ndugu. Huyu mkaka amezaa na mke wa mtu bila mume kujua na wote wanaendelea kumtunza mtoto sasa ana umri wa miaka mitano. Tatizo mdada anaogopa kusema ukweli kulinda ndoa yake, na mkaka (mwizi) anataka atambulike kwa mwanae japo na yeye ana mke.Mke wa mwizi keshaelezwa kuna mtoto nje kakubaliana na hilo japo hajui ni wapi/ kwa nani. Na familia ya mdada inajua kila kitu.Familia ya kiume na mke wa mwizi imekomaa inataka kumuona huyo mtoto. Mume wa dada hana ajualo. Nisaidieni kaka aanzie wapi, na familia ya mkaka mwizi na mdada ni marafiki toka udogoni..

Nawasilisha.
 
Kama familia ya huyo dada inajua kila kitu, jambo la muhimu ni huyo dada kumueleza mume wake ukweli akishirikiana na ndugu zake, ila awe tayari kwa lolote litakalotokea.
Kwa huyo kaka nae awe jasiri ashirikiane na huyo dada aliyezaa nae kumueleza mume wake kuhusu mtoto....
 
Imekaa vibaya
mwanamke anayezaa nje ya ndoa kupata msamaha kwa mumewe ni ngumu
nahisi harufu ya talaka hapo
 
Hamjambo wapendwa, hope wote mmeamka bien, kwa wagonjwa na matatizo mbalimbali poleni. Leo nimepata kisa kimenitatiza kidogo naomba kushare nanyi wapendwa tumsaidie huyu ndugu. Huyu mkaka amezaa na mke wa mtu bila mume kujua na wote wanaendelea kumtunza mtoto sasa ana umri wa miaka mitano. Tatizo mdada anaogopa kusema ukweli kulinda ndoa yake, na mkaka (mwizi) anataka atambulike kwa mwanae japo na yeye ana mke.Mke wa mwizi keshaelezwa kuna mtoto nje kakubaliana na hilo japo hajui ni wapi/ kwa nani. Na familia ya mdada inajua kila kitu.Familia ya kiume na mke wa mwizi imekomaa inataka kumuona huyo mtoto. Mume wa dada hana ajualo. Nisaidieni kaka aanzie wapi, na familia ya mkaka mwizi na mdada ni marafiki toka udogoni..

Nawasilisha.
mbona mkaka tu ndo anaitwa mwizi kwenye hii post? huu ni ubaguzi wa kijinsia.

ushauri zaidi nitatoa baadae.
 
kabla ya kuketi kitako kumweleza mumewe inabidi afunge na kusali sana
kumwombea mumewe aondekana na hasira itakayomakabili
 
WataUNDO vipi
halafu nashangaa huyo mume hajagundua chochote miaka yote
Inakuwa ngumu sana kwa mwanaume kugundua hasa kama anamwamini sana mke wake. Wanawake wana siri nyingi sana hasa zinazohusu watoto, kuna dada yetu mmoja alipofariki yeye na mume wake, tulishangaa alipokuja jamaa mwingine kudai mtoto kuwa ni wake. Tulikosa la kusema maana mtoto alikuwa ni fotokopi ya yule jamaa, lakini yule mtoto alikuwa anapendwa sana na baba yake aliefariki, sipati picha yule baba angekuwa hai!!
 
Duh!
Hii movie mbona kali hivi.
Steringi lazma adedi.
Mwambie mkaka mwizi asing'ang'anie kufanya hivyo. Huyo mtoto ni mdogo na ikitokea mdada mwizi ndoa yake imevunjika mtoto anaweza kuwa katika wakati mgumu.
Inawezekana mke wa jamaa hana mapenzi kutoka moyoni na huyo mtoto na angeletewa alee sidhani kama angekubali.
Wanachekelea kwasababu wanajua mtoto anahudumiwa huko aliko.
Waache unafki wao kujifanya wana mapenzi na huyo mtoto.
Dada mwizi nae hajatulia. Khaa!
 
Back
Top Bottom