Msaada kuhusu Udom

Dio

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
1,274
158
Kuna ubishi ambao umetokea leo hapa mtaani kuhusu chuo cha dodoma (udom)
eti wengne wanadai kajenga Bill gate na wengne wanadai kuwa ni mtoto wa mfalme wa Oman kajenga kulipa fadhila baada ya kuchukua wanyama kupeleka kwao,je jamani naombeni kujua kuhusu chuo cha Dodoma.
 
UDOM kimejengwa kwa pesa zetu wenyewe kutoka katika mifuko ya hifadhi za jamii
 
Ukishajua aliyetoa fedha itakuwaje?, utapata shahada?, au muliwekeana dau?, JF itafaidika nini na ubishi wenu wa kijiweni usio na tija?, unaonaje ukuacha kujaza server ya jf kwa unproductive posts? Au umeambiwa ukiwa na post nyingi utapewa hisa kwenye JF?
 
Ila mfumo wa kujenga vyuo vya mass production umepitwa na wakati na hauna quality kwenye output yake. Kwa misingi ya vyuo bora UDSM nayo iko overcrowded kwani kuwaweka wanafunzi 12,000 kwenye compound moja siyo kitu chepesi. UDSM wanaweza kwa sababu ya ukongwe wake, soko la wahadhiri wake, location na umashuhuri kimataifa. Itakuwa vigumu kwa UDOM kupata reputation kama University yenye kutoa matunda mazuri yatakayo compete kwenye soko la ajira ndani na nje ya nchi. Matatizo ninayoyaona UDOM ni kwamba kimeanzishwa kisiasa ili kiorodheshwe kama moja ya mafanikio ya chama tawala bila kujali uwezo wa miundombinu ya kubeba wanafunzi wengi kiasi hicho.

Vilevile haikuzingatia uwezo wa kupta wahadhiri mahiri kwani si rahisi kumtoa Mhadhiri mwenye CV nzuri Dar es Salaam au Mwanza na kumpeleka Dodoma kwa kuwa wahadhiri hawaishi kwa kutegemea mishahara ya vyuo tu bali kwa kufanya shughuli za Consultancy kwenye maeneo mengine ya fani zao. Matokeo yake UDOM itaishia kuchukua wahadhiri walisio na sifa au kwa kiasi kikubwa watawatumia ma TUtorial Asistants kutoa mihadhara madarasani.

Ni miaka isiyozidi mitano UDOM pamekuwa ni uwanja wa mivutano ya kisiasa, migomo ya wanafunzi, maandamano yasiyo na tija na mambo chungu nzima ili mradi tu wanachuo wawe busy baada ya ku boreka madarasani.

Bahati mbaya chuo kimeshajengwa na hatuwezi kurudi nyuma Ila tunaweza kukomea hapo ili tusifike lile la wanachuo 40,0000 kikikamilika. Kuweka wanafunzi 40,000 kwa miundo mbinu hiyo hafifu na hali ya manispaa ambayo chanzo chake kkubwa cha uchumi ni mikutano ya bunge na mikutano ya CCM, then tutakuwa tunaandaa Catastrophe.

Mfumo wa kisasa wa vyuo ni kwa kutumia constituency colleges sehemu mbalimbali Kama vile Tumaini University au SAUT wanavyofanya. Hapa Africa vyuo vikuu ambavyo vina sifa kubwa kitaaluma havina hata ukubwa wa UDSM lakini dunia inabitambua. Angalia University of Ibadan na University of Lagos (Nigeria), University of Witwatersrand na University of Capetown (South Africa), University of Nairobi au Makerere. Vyote hivi havina eneo wala udahili mkubwa kiasi hicho. At best UDOM kieneo inaweza kufanana na UNISA (ambayo ni taasisi ya open university kwa South Africa).

Ushauri wangu wa bure ni kama ifuatavyo;
1. Serikali isitishe upanuzi zaidi wa UDOM
2. Uongozi wa UDOM ufundishe taaluma chache tu ambazo Wanamaker uhakika na wahadhiri na vitendea kazi
3. Miundombinu muhimu hasa maji lazima yawe kipaumbele
4. Serikali ielekeze raslimali zilizobakia kwa ajili ya UDOM kwenye vyuo vingine
 
Ukishajua aliyetoa fedha itakuwaje?, utapata shahada?, au muliwekeana dau?, JF itafaidika nini na ubishi wenu wa kijiweni usio na tija?, unaonaje ukuacha kujaza server ya jf kwa unproductive posts? Au umeambiwa ukiwa na post nyingi utapewa hisa kwenye JF?

we ndo huna akili kabisa
 
Back
Top Bottom